![]() |
Mama Joshuab akishuhudia uponyaji, na anayemhoji ni Mchungaji kiongozi wa Ufufuo na uzima Arusha Frank Andrew |
Esther au mama Joshua aliletwa kanisani Ufufuo na Uzima Tawi la Arusha akiwa ameshikwa na ukichaa, kwa muda wa wiki mbili.
Baada ya maombezi, alifunguliwa na kushangaa, maana alikuwa hajui amefikaje kanisani na kusema kuwa muda wote huo alijiona yupo baharini.
Kwasasa amewekwa huru kabisa na ameungana na familia yake. Sifa, utukufu, heshima na enzi ni za Bwana...
MCHAWI AKAMATWA NA HIRIZI
MCHAWI AKAMATWA NA HIRIZI
![]() |
Hii ni moja ya hirizi ambazo amekutwa nazo mchawi aitwaye Christina, alipotekwa kanisani. Ufufuo na Uzima Arusha. |
Katika tukio jingine mchawi aitwaye mmoja aitwaye Christina,
alitekwa kanisani. Ufufuo na Uzima Arusha... Mungu ni mkuu, binti huyo
alisema kuwa alirithishwa uchawi na bibi yake. Baada ya maombezi
amewekwa huru kutoka katika vifungo vya uchawi.

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12
Comments