HARUSI YA KANA (Wedding in Cana of Galilee)*sehemu ya pili*

Na Mtumishi Gasper Madumla


Nakusalimu mpendwa katika jina la Bwana Yesu;
BWANA YESU ASIFIWE...
Haleluya...

Karibu katika sehemu ya pili ya fundisho hili zuri,lenye kukupa misuli ya imani wewe umpendaye Bwana Yesu Kristo. Hakika uta-enjoy sana siku ya leo kwa chakula hiki.
Harusi hii ya Kana imepata nafasi ya kuandikwa katika kitabu kitakatifu,
Biblia kwa sababu ya kile kilichobebwa ndani ya harusi hii.
La kama si hivyo basi ising’eliandikwa,lakini mpaka imeandikwa basi ujue yapo mambo mengi ya kujifunza.

Tumeona Bwana Yesu pamoja Na wanafunzi wake,na mama yake wakiwa wamealikwa harusini. Basi kumbe suala la kualikana kwenye maharusi halikuanzia hivi leo,
lilikuwepo hata enzi za Bwana Yesu,lakini suala la kuzamia katika harusi(yaani kwenda kwenye harusi pasipo kualikwa) hilo suala ndio jipya,ni la siku hizi ,
maana zamani huwezi "kuzamia" katika harusi,kwa kuwa tumeona Yesu mwenyewe pomoja na wanafunzi wake wakiwa wamealikwa.

Pale harusi hii ya Kana ya Galilaya ilipokuwa imenoga,gafla tunaona shida inajitokeza,shida ya kuishiwa divai.
Kwa taratibu za Wayahudi,DIVAI ilikuwa kinywaji muhimu sana pindi wafanyapo sherehe.
(Wine was the special pure juice from the grape,normally used in various Hebrew festivals)

Divai sio kileo,
Divai ilikuwa mojawapo ya kinywaji kilichoagizwa kitolewe mbele ya Walawi,(Walawi walikuwa ni watu maalumu waliotengwa kwa ajili ya kazi ya Bwana)Kumb.18:1-5.

Haleluya...

Sasa,
Tazama shida ya kutindikiwa kwa Divai ikijitokeza ndani ya harusi ya Kana.Tunasoma;
" Hata divai ilipowatindikia,mamaye Yesu akamwambia,Hawana divai" Yoh.2:3.

Mamaye Yesu anatufundisha kwamba ikiwa utatindikiwa kwa jambo lolote lile katika maisha yako,
Basi umkimbilie Bwana Yesu tu,Maana Yeye Yesu Kristo atayatindua yale yote yaliyotindika kwako.

Sasa sikia;
Mamaye Yesu hakumkimbilia
Simoni aitwaye Petro,
Wala hakumkimbilia Andrea,
Wala Yakobo wa Zebedayo,
Wala Yohana wa Zebedayo,
Wala Filipo,
Wala Barthomayo,
Wala Tomaso,
Wala Mathayo mtoza ushuru,
Wala Yakobo wa Alfayo,
Wala mama Yesu hakumkimbilia Thadayo;
Wala hukumkimbilia Simoni Mkananayo,
Wala mama huyu hakumuendea Yuda Iskariote,
Maana alijua hawa wote hawana UWEZA kama ule uliokuwa ndani ya Bwana Yesu,

BALI ALIMKIMBILIA YESU WA NAZARETI,akituonesha kwamba hiyo ndio njia ya kweli,maana hakuna aendaye kwa Baba pasipo njia hiyo (Yoh.14:6)-Yesu ndio njia,Kweli,na uzima.

Chakushangaza sasa;
shetani amepotosha fahamu za watu,hata watu kumgeukia mamaye Yesu na kumuomba,
wakati mamaye Yesu mwenyewe anatuonesha njia ya kuiendea na kuomba.
Shetani hana akili kabisa!

Funguka!
Ukaelewe hili,kwamba ni Yesu Kristo pekee anayestahili kuombwa na sio kumuomba mama yake,Mariamu,au mwingine awaye yote.
Mimi nashindwa kumuelewa mtu abadilishaye ukweli huu,maana hata mamaye Yesu mwenyewe ametuonesha yule astahiliye kuombwa,
• kwa nini basi umkimbilie mama yake Yesu,wakati Yesu mwenyewe yupo?

Haleluya..
Jina la Bwana lipewe sifa...

Tunasoma hapa tena,
"Yesu akamwambia, Mama,tuna nini mimi nawe?Saa yangu haijawadia." Yoh.2:4

Unaweza ukajiuliza hivi;
Sasa inakuwaje Bwana Yesu anamjibu mamaye hivyo?
Kwamba mama yake anamuomba jambo,lakini hatuoni Yesu akifanya muujiza pale pale alipoombwa,badala yake naye anamuuliza " tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia"

Hata mimi nilijiuliza hivyo,sijui wewe kama ulijiuliza.
Ndiposa nikagundua kwamba;

UPO WAKATI WA BWANA WA KUJIDHIHILISHA.
• Yaani upo wakati wa kudhihilisha nguvu ya Bwana Mungu.

Bwana ana muda wake wa kujidhihilisha,muda wa Mungu sio sawa na muda wa mwanadamu,vile tupangavyo sio sawa apangavyo Yeye Mungu. Ndio maana Yesu anamwambia mama yake " Saa yangu haijawadia"
Mara nyingi tunapenda Mungu atutendee mambo makubwa kwa muda na wakati tuliojipangia sisi wenyewe,
lakini ni tofauti na vile mungu atakavyo,tazama wale waliokuwa katika harusi ya Kana walitamani muujiza ufanyike muda ule ule,lakini Yesu anamjibu mama yake kwamba WAKATI WANGU BADO.

Ni mara ngapi tunaomba Mungu atutendee ili na lile,lakini kumbe wakati wake bado wa kudhilisha muujiza wake.Ndiposa nikatia akili na ufahamu niliposoma habari hii ya harusi ya Kana.

Kulikuwa na wakati ambao Wayahudi walikuwa wakitafuta kumuua Yesu huko uyahudini,ndugu zake Yesu Kristo wakamwendea Bwana Yesu na kumtaka aende uyahudini ili wanafunzi wakaone ishara na miujiza yake,lakini yeye akawajibu;

“ Maana hata nduguze hawakumwamini.
Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo.” Yoh.7:5-6

Yamkini wewe umekuwa kama mmoja wa ndugu yake Yesu unayetaka Bwana akujibu pale tu uombapo mbele zake,Au
Yamkini umeomba sana pasipo hata kujibiwa,mimi nami nakuambia usikome kuomba maana yawezekana wakati wa Bwana wa kujidhihilisha kwako bado haujafika,wewe endelea kuomba na wakati wa Bwana utakapowadia basi kila kitu kitakuwa sawa…

ITAENDELEA…

• Kwa huduma ya maombezi;
0655-111149.

UBARIKIWE.

 
 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments