Kanisa la Pentecostal Asemblies of GOD (PAG)
Vijibweni soweto chini ya mpakwa mafuta wa BWANA Mchungaji Eliza Kihwili
limetimiza mwaka mmoja tangu lifunguliwe December Mwaka 2012. Katika
ibaada ya shukrani mchungaji Eliza alisema anamshukuru sana MUNGU kwa
neema yake licha ya kuanza kwenye mazingira magumu lakini BWANA
alitengeneza njia pasipo na njia kwani hadi sasa wanalo eneo la
kuabudia, wanavyo vyombo vya mziki na mafaikio mengine ikiwemo
kuongezeka kwa waumini kwani walianza familia moja lakini sana wako
zaidi ya 20, na changamoto yao ni ujenzi wa kanisa ambao unahitaji
Milioni 20, mpendwa kama ukipenda kuifanya kazi ya MUNGU pamoja na
mtumishi huyu basi unaweza kutoa mchango wako kwa kuwasiliana nae kwa namba 0715929231 au wasiliana nami kwa
namba 0714252292 na tutakuunganisha moja kwa moja na mchungaji Eliza.
zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo la ibaada ya shkrani. MUNGU
akubariki sana
 |