BWANA YESU
asifiwe, karibu.
Matendo 4:12
‘’Wala
hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini
ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.’’
Ila ni jina
YESU KRISTO.
Ila ni jina
la YESU KRISTO.
Ila ni jina
la YESU KRISTO.
Walikuwepo
mitume wengi ila hawakuweza kuokoa.
Walikuwepo
manabii wengi hawakuweza kuokoa.
Walikuwepo
watu maarufu ila hawakuweza kuokoa.
Walikuwepo
walimu wa dini ila hawakuweza kuokoa.
Ila ni jina
la BWANA YESU pekee ambalo tunaweza kuokolewa kwalo.
Biblia
inaweka wazi juu ya nani ambaye anaweza kuwafanya wanadamu wasiende jehanamu
Warumi
10:9-13. ‘’Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa
kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua
katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa
kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye
hatatahayarika. Kwa
maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni BWANA wa wote,
mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
kwa kuwa, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA.’’
kwa kuwa, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA.’’
Ndugu zangu BWANA YESU anaokoa na ukiamini hakika
unaokoka maana hakuna uzima kwingine.
Yohana 14:6
Biblia inasema ‘’ YESU akamwambia, Mimi ndimi njia , na ukweli na uzima; mtu
haji kwa BABA ila kwa njia ya mimi.
BWANA YESU leo anasema.
‘’Njooni
kwangu nyote, wenye kulemewa wenye kulemewa na mizigo nanyi nitawapumzisha.
Wenye mizigo
ya magonjwa, njooni kwangu nami nitawapumzisha.
Wenye mizigo
ya madeni njooni kwangu , nami nitawapumzisha.
Wenye mizigo
ya kuteswa na wachawi njooni kwangu nami nitawapumzisha.
Wenye
kuonewa na mapepo, njooni kwangu , nami nitawapumzisha.
Wanaoteswa
na mizimu na roho za ukoo, njooni kwangu nami nitawapumzisha.’’
KWANINI
BWANA YESU PEKEE?
Ni BWANA
YESU pekee wa kuokoa kwa maana MUNGU alimtoa kwa ajili ya ukombozi wa
mwanadamu, ukombozi wa mwili na roho pia.Yohana 3:16-18 ‘’Kwa maana jinsi hii
MUNGU aliupenda ulimwengu , hata akamtoa
mwanawe pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili
auhukumu ulimwengu, ulimwengu uokolewe
katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi,
asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa MUNGU.
BWANA YESU
alidhihirishwa ili azivunje kazi za shetani(1 Yohana 3:8b).
Ndio maana
ukiwa ndani ya KRISTO umekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama yamekuwa
mapya. -2 korintho 5:17.
MUNGU akubariki
sana.
Ni mimi
ndugu yako.
Peter M
Mabula
Maisha ya ushindi
Ministry

Comments