BWANA YESU
asifiwe ndugu.
Karibu
tujifunze kuhusu kanisa la KRISTO duniani.
Kanisa la
KRISTO ni kundi la watu ambao.
1.
Wamekombolewa kwa damu ya YESU KRISTO.
Waefeso 1:7-‘’Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
‘’
2.
Wametengwa na dunia.

3.
Huamini injili.
Yohana 20:31- ‘’ Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo,
Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.
‘’
4.
Hufuata
mafundisho ya KIKRISTO.
Tito 2:11-14.''Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
ambaye alijitoa nafsi yake
kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe
milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.''
JINSI YA KUWA
MSHIRIKA WA KANISA.
Ili kuwa mshirika wa kanisa la KRISTO, sharti kubwa zaidi ni kwamba mtu
azaliwe mara ya pili. Yohana 3:3-5.'' Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
''
Hatua 3 za lazima
a.
Imani katika KRISTO na katika damu yake
isafishayo dhambi. Yohana14:6-''Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. '',
Yohana 3:6 na 16.
Matendo 16:31-''Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.''
,
Waefeso 1:7 na 1
Yohana 1:7 na 9.
b.
Toba ya kweli Matendo 3:19-21''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani;
ambaye ilimpasa kupokewa
mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na
Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.''
Mathayo 9:13- Maana yake ni
kuungama dhambi zetu zote kwa MUNGU na kuziacha .
c.
Ukiri wa wazi wa imani katika KRISTO. Warumi 10:9-13'' Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa
chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua
katika wafu, utaokoka.
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.
Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.''
na Mathayo 8:38 Kubatizwa na
maji ni njia moya ya kumkiri BWANA YESU kwa uwazi.
KAZI YA KANISA
DUNIANI
1. Kuhubiri injili kwa kila kiumbe. Mathayo
28:19''Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.'' . Na 1 Petro 2:9-10.'' Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. ''
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.'' . Na 1 Petro 2:9-10.'' Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. ''
2. Kudumisha ile kanuni ya Biblia juu ya
utakaso na maisha mema mbele ya ulimwengu. Waefeso 5:25-27'' Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
'' na Mathayo 5:13-26.
3. Kuwa tayari kutenda mema siku zote. Tito 2:14''ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote,
na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi
katika matendo mema. ''
, Wagalatia 6:10'' Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
'' na Mathayo 5,
16,44,45.
Ndugu kumbuka kuwa dhehebu lolote la kikristo
bila KRISTO mwenyewe ni Ubatili.
Ndugu zangu Hii ndio saa ya Wokovu,
hivyo kama hujampatia BWANA YESU KRISTO maisha yako basi nafasi ya kufanya
hivyo ni leo.
Omba maombi hata mafupi na utaokoka kisha acha dhambi zote na tafuta kanisa la kiroho.
Omba maombi hata mafupi na utaokoka kisha acha dhambi zote na tafuta kanisa la kiroho.
Sema
‘’BWANA YESU, niko mbele
zako mimi ni mwenye dhambi, lakini leo naamua kukufuata wewe BWANA YESU, Natubu
dhambi zangu zote, ninazokumbuka na nisizozikumbuka, Futa jina langu kwenye
kitabu cha hukumu na uliandike jina langu kwenye kitabu cha uzima, tangu leo
nimeoka, naufunga ukurasa wa dhambi na kuanzia sasa ninafungua ukurasa wa
kumcha MUNGU nikiwa ndani yako BWANA YESU. Nipe ROHO MTAKATIFU ili aniongoze
kuanzia sasa. Asante BWANA YESU kwa kuniokoka, niongoze BWANA na niwe mbali na
kuonewa kuanzia sasa, navunja maagano yote ya shetani niliyoingia, najitenga na
laaza za ukoo na roho za mizimu katika jina la YESU KRISTO, nishindia vyote
BWANA. Katika jina lako takatifu BWANA YESU nimeomba, nimeamini na nimepokea.
AMEN’’
Baada ya maombi haya Tafuta
kanisa la kiroho wanapohubiri kweli ya MUNGU na wanakiri WOKOVU tena wanaikemea dhambi hadharani,
waeleze na watakuombea na kukuongoza kisha utaukulia Wokovu wa BWANA YESU
pamoja na washirika wengine.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika KRISTO.
Peter Michael Mabula
(Maisha ya ushindi Ministry)
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika KRISTO.
Peter Michael Mabula
(Maisha ya ushindi Ministry)

Comments