KANUNI KUMI ZA MAOMBI



LUKA 11:1-4
1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].
1. , Baba [yetu uliye mbinguni} Lazima ujue unayemuomba yeye yuko mbinguni hivyo maombi yako elekeza kwake yeye tu ambaye ndio aliyetuumba.

2. Jina lako litakaswe –Unatakasa jina hilo kwa maana ni tofauti na majina mengine au ni safi kupita yote hivyo lina dhamani kubwa kuliko yote

3. Ufalme wako uje-Maana huo ufalme wake uko mbinguni hivyo lazima ushuke hapo ulipo maan ufalme wa hapa sio wake unashikiliwa na shetani hivyo kunakuuita ushuke hapo ulipo na kukuzingira hivyo unakuwa unaita nuru yake hapo ulipo.

4. Mapenzi yako yatimizwe – Mapenzi yake yatimizwe jinsi yeye apendavyo na sio wewe upendavyo unajua unapoomba kitu lazima kuwe na ushawishi wa kile kitu unachohitaji hivyo kuna ushawishi wa jambo lile kwa Yule unayehitaji akupatie kwa kumsifia kumbembeleza kumuomba kwamba kweli utakitunza na kukilinda kile unachohitaji kumueleza nini madhumuni yako ya kuomba na unatarajia kufanyia nini akikupatia na jinsi kitavyokuwa na manufaa kwako.

5. hapa duniani kama huko mbinguni – Hayo manufaa yawe kwako hapa duniani na mbinguni je utabaki kuwa wake akikupatia je utashirikisha wengine baada ya kupata je kunafaida kwako na kwengine na watarudisha shukrani kwake na kuwa wake hao utakaofaidika nao nk.

6. Utupe siku kwa siku riziki yetu – Ukishafikia hapo unatakiwa uombe kubaki nayo au kubaki nayo hayo maombi kila siku kwa kungangania ili usinywangwaye na adui ni kama vile kuweka mambo au vizingiti vya kuzuia yasing’olewe na adui maana yeye yuko na anahitaji kuiba kutoka kwako.

7. Utusamehe dhambi zetu –Kujitakasa kwa kufanya toba juu yako na familia na jamii kwa ujumla maana hapa anaongelea dhambi zetu na sio dhambi zako kuna tofauti ya toba yako binafsi naya jamii nzima.

8. kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye – Fanya toba ya kusamehe wale walio kukosea kwanza ili upate kibali nawe cha kuwa huru maana nira ile uliyoweka kwa mwenzako nawe imewekwa kwako leo hivyo unapoondoa nira kwa mwenzako nawe kwako inaondolewa.

9. Na usitutie majaribuni – Omba usiingie katika majaribu maana huko kuna kushindwa kutoka hivyo ni vizuri kuweka kinga ya kutokuingia ili uweze kushinda vita hivi ambavyo adui yuko kila mara akilite majaribu juu yetu kwa kuwa yeye ni baba wa majaribu.

10. lakini tuokoe na yule mwovu – Maana si kwa nguvu zetu tutashinda bali kwa mkono wenye nguvu wa Bwana maana anasema tumtegemee yeye tu maana atatuokoa na adui na atatuvusha katika hatari na kutulinda ijapokuwa tutakula sumu lakini tutaishi maana yeye ndiye aliyefanyika laana kwa ajili yetu ili tukombolewa kwa kufa katika kifo cha laana pale msalabani ili kwa laana yake sisi tuhesabiwe haki ni kwa kumkiri tu na kumkata shetani tunapopata ule wokovu mkuu katika kristo Yesu.

                                                 AMENI

                                       by Salvation Choir Hebroni
 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments