KUFUNGA NI NINI?

Na Sam Balele
Kuna mtu aliwahi kunisumbua sana wakati fulani, ilipofika wakati wa utaratibu wa kidini yao kufunga akaniambia anapumzika kunisumbua, akimaliza kipindi cha mfungo ataresume usumbufu wake. Now this is not fasting, huku ni kujishindisha njaa tu. Ukiamua kuacha njia mbaya/wicked ways ni uamuzi wa kudumu, wa moja kwa moja, uamuzi endelevu ukiwa chini ya Neema ya Mungu ili usitumbukie tena katika wicked ways na kumtenda Mungu dhambi.



Usishinde njaa tu. Ukifunga ni lazima uwe na muda mrefu wa kutulia katika prayer ili uongee na Mungu. Asilimia kubwa ya watu wamekuwa wanajishindisha njaa tu. Nasema hivyo kwakuwa mtu anafunga kwa ajili ya ku-observe na kutii taratibu fulani za kidini ama kidhehebu. Kufunga ni lazima kuwe na lengo ambalo majibu yake ni lazima yapimike na kuonekana. Lazima kuwe na matokeo kutokana na kufunga kwako, lakini kama unafunga tu sababu ni utaratibu uliopo kila mwaka katika majira fulani, to me I regard that as fruitless, unless kuwe na objectives na mwisho wa mfungo ni muhimu kutarajia results na kupima kama mfungo umeleta hayo majibu kutoka kwa Mungu. Kinyume cha hapo unafunga kidini/kidhehebu hivyo unajishindisha njaa tu.

 
Wewe hiyo fasting yako ikoje? Je inaendana na Neno la Mungu [Biblia]? Ama inaendana na mapokeo yaliyomo katika Dini yako au Dhehebu lako?
King David said this in:
Psalms 35:13; But as for me, when they were sick, my clothings was sackcloth; I humbled myself with fasting and my prayer would return to my own heart.
Zaburi 35:13; Bali mimi, walipougua wao, nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga, maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.

Mfalme Daudi alifunga kwa sababu mtoto wake alikuwa anaumwa. Alifunga na kufanya maombi kwa bidii na juhudi ili Mungu amponye mtoto wake aliyekuwa mgonjwa. Ila results hazikuwa positive kwake kwakuwa still mtoto wake alikufa. You can see that he had an objective to fast, and he prayed and expected results, when he saw the results he stopped praying. Fasting goes with Prayer, also being expectant of something from God. So why do you fast? When you fasted the last time, what was the need? Did you see vivid results?

Nina mfano hai, a very recent personal experience. Leo namalizia mfungo ambao nilikubaliana ndani ya roho yangu kuufanya kwa muda wa siku 3 mfululizo, bila kula wala kunywa chochote kile, nikiwa na needs zangu za kumwambia Mungu. Nilianza Jumanne asubuhi na ninatarajia kumaliza kesho asubuhi ili kutumiza masaa 72. Katika mfungo huu uliombatana na MAOMBI, Mungu amenipa majibu ya needs zangu nilizopeleka kwake, majibu nimeyapata jana, na leo ilikuwa ni siku ya kutoa shukrani na kuomba zaidi neema na rehema za Mungu katika yale majibu aliyonipa. Sasa huku ndiko kufunga, this is fasting, FASTING THAT GOES WITH PRAYER.

Kufunga siku 40 ama 30 bila kuwa na muda wa kutosha kutulia chini kuomba mbele za Mungu, kwa muda wa kutosha, ukipeleka yale unayohitaji Mungu akufanyie, ni kujishindisha njaa tu. Ni fasting ambayo mimi naita ni ya kidini/kidhehebu. Japo najua kuwa kuna aina 2 za Fasting, ile ya wengi [corporate fasting] na ya mmoja mmoja [individual fasting].

Point nayotaka kustress hapa ni kuwa lazima ujue kwanini unafunga? Unapata faida gani kwa huko kufunga kwako? Je huko kufunga kama ni kwa watu wengi, wazijua objectives zake? Na kama wazijua, je huwa unapata muda wa kutosha kuomba na kuzipeleka mbele ya Mungu ili azitolee majibu? Na ikiwa ni individual fasting ni lazima ujue why unafunga? Mahitaji ya kufunga kwako ni nini? Je unatenga muda wa kuomba vya kutosha, angalau li saa limoja? Ama unafunga tu kwa mapokeo ya dini yako au dhehebu lako? Kama unafunga kwa style hiyo ndugu yangu, pole kwa vile unajishindisha njaa tu na hakuna faida unayopata hapo. Na ikiwa unaacha njia zako mbaya wakati wa mfungo na baada ya huo mfungo wako ulioufanya unarejea katika zile njia zako mbaya tena, hapo nako unacheza tu rafiki yangu, tena unachofanya ni kumdhihaki Mungu kabisa, na Mungu amesema katika Neno lake [Biblia], kuwa mwanadamu atavuna anachopanda. Wewe panda tu hayo mapokeo ya dini yako na hilo dhehebu lako uone utakachovuna.

Mungu atusaidie kuweza kuenenda sawasawa na mafundisho yake yanayoambatana na Neno lake tu[BIBLIA]. Ni lazima ujue na uelewe kuwa kuna mafundisho ya Roho Mtakatifu na mafundisho ya wanadamu, mafundisho ya mashetani. Kama hayo mafundisho hayana msingi katika Biblia Takatifu, basi hayo si mafundisho ya Mungu, ni mafundisho ya mashetani, mafundisho ya wanadamu. Huo ndio ukweli hata kama utakasirika, someone has to say it and am saying it now. 1TIMOTHEO 4:1-3.



 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments