KUISIKIA SAUTI YA MUNGU




Na Snp Josephat Gwajima.Ufufuo na uzima


Mara nyingi tunamwomba Mungu lakini hatufahamu kuisikia sauti yake anaposema nasi Kuna namna kadha wa kadha za kuisikia sauti ya Mungu.
i. Katika maono
ii. Katika ndoto
iii. Katika neno la Mungu
iv. katika njia ya manabii wake
v. sauti ya ndani ya Roho Mtakatifu
vi. Kupitia mzingira
vii. kupitia walimu wa Neno la Mungu

1. kuisikia sauti ya Mungu katika maono
i. Mungu aliongea na Nabii Ezekieli kuhusu Bonde la mifupa mikavu, naye akaitabiria ikawa jeshi la watu hai.
Ezekieli 37:1-14

ii. Mungu alimtokea Yohana katika maono akiwa katika kisiwa cha Patmo. Ufunuo 1:9-20

2. Kuisikia sauti ya Mungu kupitia ndoto
Mifano ya watu walioisikia sauti ya Mungu katika ndoto.

i. Abimeleki – Mungu aliongea na Abimeleki kumuonya kwa habari ya Sara mke wa Ibrahim naye hakumkaribia asimtende Mungu dhambi Mwanzo 20:1-3

ii. Malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto kwamba asiogope Mariam kwa kuwa mimba ilikuwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mathayo 1:20

3. Kuisikia sauti Mungu kupitia Neno la Mungu
Mifano ya watu walioisikia sauti ya Mungu kwa njia ya Neno la Mungu

i. Paulo na Sila walinena neno la Mungu na yule mkuu wa gereza akampokea Yesu. Matendo 16:29-33

ii. Bwana alimwita Samweli alipokuwa kijana 1 Samweli 3:20-21

4. Kuisikia sauti ya Mungu kupitia unabii.

i. Mungu aliongea na Mfalme Daudi kupitia unabii, 2Samwel 12:1-14
ii. Mungu aliongea na Mfalme hezekia kupita nabii Isaya. 2Falme 20:1-6

Faida alizopata Hezekia baada ya kuitii sauti ya Mungu
• aliponywa magonjwa yake
• aliongezewa miaka 15 ya kuishi Duniani
• Yeye na mji wake waliokolewa na kulindwa

5. Kuisikia sauti ya Mungu kupitia mazingira na matukio
Maisha yetu ya kila siku yanajumuisha mazingira na matukio ya kila siku Mifano ya watu waliosikia sauti ya Mungu kupitia mazingira na mtukio

i. Mungu alisema na Yona kwa kupitia tufani wakati alipokataa kuitii sauti ya Mungu iliyomuekeza kwenda Ninawi. Mungu akaleta Dhoruba katika mrikebu aliyotumia kwenda Tarshishi. Yona 1:4; 7-11. ndipo Mungu akaandaa samaki ammeze ili kumrudisha Ninawi Yona 1:15.

ii. Mungu aliongea na Baalam kupitia Punda baada ya Baalam kwenda njia iliyokuwa kinyume na maagizo ya Mungu. Hesabu 22:20-22

6. Kuisikia sauti ya Mungu kupitia sauti ya ndani ya Roho Mtakatifu.




i. Mungu aliongea na Philipo kwa Roho Mtakatifu aende kumwongoza Mkushi towashi aliyekuwa akisoma chuo cha nabii Isaya. Matendo 8:29-32

ii. Mungu aliongea na Yohana kwa Roho mtakatifu kwa habari ya makanisa saba ya efeso. Ufunuo 1:10-13
Mkutano wa mchungaji Gwajima Tanga.

  

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments