Kutoka KPC Kawe;Apona mguu uliokuwa umewashinda madaktari India

Mchungaji Elly Boto akifundisha kabla ya maombezi
MUNGU ndie mwamuzi wa mwisho kwa wateule wake.
Nasema hivyo kwa sababu mama huyu katika ibada ya kuanza mwaka katika kanisa la Kawe Pentecostal Church MUNGU alitenda jambo ambalo hapana mwanadamu hata mmoja anayeweza kulitenda. Mamlaka ya jina la YESU KRISTO ilipotamkwa ushindi wa ajabu ulitokea. Maisha ya ushindi tulikuwepo na tulishuhudia nguvu hii ya MUNGU iliyomponya mama huyu, simulizi yake ni hii aliyoitoa kanisani hapo 
''BWANA YESU asifiwe, namshukuru MUNGU sana tena sana maana nimekuwa naumwa mguu kwa miaka mingi  na nimetembea hospital kubwa zote Tanzania lakini sikupona nilianza na Bugando Mwanza wakashindwa, nikaenda KCMC wakashindwa nikaja TMJ hata hawakuona huo ugonjwa zaidi ya kuona uvimbe, nikaenda Muhimbili hospitali ya taifa lakini vipimo vyote havikuona ugonjwa zaidi ya kuona uvimbe, nimekuwa na mika zaidi ya 4 siwezi kutembea peke yangu na hata nimekuwa kero kwa ndugu na majirani, baada ya kutoka muhimbiri walinishauri niende India maana huko kuna wataalamu sana nikaende lakini hata huko hawakuona ugonjwa nikarudi baada ya hapo nilikata tamaa na kusema basi itakavyokuwa na iwe maana nimetumia gharama kubwa sana lakini hata nafuu tu sikupata, baada ya hapo nikawa naenda kwenye maombezi na nakuhakikishia kwamba nimetembea kwa watumishi wengi wa MUNGU na kwenye makanisa makubwa lakini nilipata tu nafuu ila bado sikuweza kutembea pekeyangu. baada ya kushindwa kabisa kupona nilikata tamaa, lakini leo kwa sababu kanisani kwetu hakuna ibaada Mama huyu akaniambia tuje hapa ili tuanze mwaka 2014 kwa maombi maana leo ndio tarehe 1, nikakubali wakanibeba na hadi nimefika hapa, maombezi yalipoanza nilianza kuona utofauti na baada Mchungaji aliponiwekea mkono na kuniombea hakika nimepona , na mwanzo nilidhani kawaida tu lakini pale mchungaji aliponiambia nitembee kuzunguka kanisa ili kuhakikisha kama nimepona ndipo nilipomshangaa sana BWANA YESU maana ameniponya, naweza kutembea peke yangu na hata kukimbia pekeyangu maana mmeona nilivyokuwa nakimbia , hakika YESU ni BWANA na MUNGU hutokea pale akili ya kibinadamu inapofika mwisho . maana nimeombewa sana na kama hospital nimeenda sana na hata India panapoaminika nimeenda lakini sikuponya, MUNGU ashukuriwe aliyenipenda leo na kunikumbuka na kuniponya ili na mimi nianze mwaka 2014 nikiwa salama . Hakika asante BWANA YESU kwa wema wako. nimepona tena nimepona kabisa namshukuru sana MUNGU na nawashukuru watumishi wake wa mahali hapa , nitakuwa nakuja kila nikipata nafasi MUNGU awabariki sana''  
  Baada ya maombezi hayo mtumishi wa MUNGU Rev. Elly Boto ambaye alipata neno la ufununuo kuhusu huyo mama alimshukuru MUNGU kwa kumwombea baraka mama huyo na yule aliyemleta na kusema kwamba MUNGU atamrudishia mama huyo yote yaliyopotea ikiwemo kwenda India ambapo ni gharama kubwa.

Ndugu kama unahitaji maombi au ushauri wa kiroho mpigie mchungaji Elly Boto kwa namba 0719640642 au 0752965812. pia unaweza kumpigia mzee kiongozi wa kanisa hilo kwa namba 0657361222. ni bure kabisa picha zaidi za tukio hilo ni hizi.

baada ya kupona akishuhudia jinsi MUNGU alivyomponya

baada ya kupona anasimama peke yake bila kusaidiwa na mtu hakika BWANA YESU KRISTO anaponya

Baada ya kuhakikisha amepona kwa kutembea kuzunguka kanisa , mama huyu akishuhudia


aliyemleta anakuja kuthibitisha uponyaji na pia anashukuru  maana amepunguziwa mzigo wa kumbeba mgonjwa kwani kuanzia sasa atakuwa anatembea pepke yake

Mchungaji akiwabariki wote aliyekuwa anaumwa na aliyemleta




 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments