KUZALIWA MARA YA PILI NI NINI?



BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze kuhusu kuzaliwa mara ya pili.
Nikodemo hakuelewa maana ya kuzaliwa mara ya pili kama jinsi ambavyo wengi hawafahamu leo.  Nikodemo aliuliza:

YOHANA 3:4:
"Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee!  Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?"  Jibu ni hapana!  Kuzaliwa mara ya pili siyo kurudi tumboni mwa mama yako.  Kuzaliwa mara ya pili ni hivi:
Yesu Kristo anaitwa Adamu wa pili au mtu wa pili aliyetoka mbinguni.  Adamu wa kwanza alitoka katika udongo na alipojaribiwa na shetani, alifanya dhambi.  Adamu wa pili au Adamu wa mwisho, Yesu Kristo, alipojaribiwa na shetani, hakufanya dhambi kamwe.  Kama atulivyoichukua sura ya Adamu wa kwanza na tukawa watenda dhambi, basi kwa imani katika Kristo, Yesu, tunazaliwa mara ya pili na kuchukua sura ya Adamu wa mwisho, Yesu Kristo; mwenye uwezo wa kushinda dhambi.  [SOMA 1 WAKORINTHO 15: 45, 47-49; WAEBRANIA 4:15].  Tunakuwa tumezaliwa kwa Roho yenye kuhuisha.  Hapo mwanzo tumboni mwa mama zetu tulizaliwa katika mwili, tukachukua sura ya yule wa mwili Adamu, sasa tunazaliwa kwa Roho na kuchukua sura ya yule wa Roho; Yesu Kristo. [YOHANA 3:6].  Kwa sababu hiyo, kama jinsi Yesu Kristo alivyokuwa na uwezo wa kushinda dhambi, sisi nasi tunakuwa na uwezo huo pia.  Matokeo haya yanatufanya tuishinde dhambi na kuhesabiwa haki ya kuingia mbinguni.

HATUA SITA (6) ZA KUFUATA ILI KUZALIWA MARA YA PILI, KUHESABIWA HAKI, NA KUOKOLEWA KUTOKA KATIKA GHADHABU YA MUNGU

1.         UKUBALI KWAMBA WEWE NI MWENYE DHAMBI, UMEMWASI MUNGU, NA
UNASTAHILI HUKUMU
Umekwisha fahamu kwamba wewe ni mwenye dhambi kwa kuzaliwa na kwa kutenda.  Ndivyo ulivyo.  Huwezi kukataa.  Maisha yako yanakushuhudia mwenyewe kwamba uko mbali na mapenzi ya Mungu.  Ukiri wazi jambo hili kama walivyofanya watu hawa katika Biblia:
2 SAMWELI 12:13:
"Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi .........."

1 SAMWELI 15:24:
"Ndipo Sauli akamwambia Samweli, nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA..."

YOSHUA 7:20:
"Akani akamjibu Yoshua akasema kweli nimefanya dhambi juu ya BWANA Mungu wa Israeli nami nimefanya mambo haya na haya."

ZABURI 32:5:
"Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotevu wangu.  Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA ............."

2.         USIKITIKE KABISA KWA DHAMBI ZAKO, UZIUNGAME NA KUWA TAYARI KUZIACHA KUANZIA SASA NA UWE TAYARI KUOMBA MSAMAHA

ZABURI 38:18:
"Kwa maana nitaungama uovu wangu, na kusikitika kwa dhambi zangu."

MITHALI 28:13:
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."

LUKA 18:13:
"Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi."

1 SAMWELI 15:25:
"Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu ................"




2 SAMWELI 24:10:
"Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma ....... Naye Daudi akamwambia BWANA, nimekosa sana kwa haya niliyofanya; lakini sasa, Ee BWANA, Nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa."

EZRA 10:1:
“Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu wakamkusanyikia katika Israeli wote kusanyiko kubwa sana la wanaume na wanawake na watoto maana watu hao walikuwa wakilia sana.”

EZEKIELI 18:30 - 31:
".....Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote ...... Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya ......."
 MUNGU akubariki sana ndugu

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments