MASWALI MATATU YENYE MAJIBU MUHIMU KWA WATU WOTE

BENDERA YAKE YESU SASA INAPEPEA.inapopepea magonjwa yanawatoka watu, mapepo yanawatoka watu.
Peter Michael Mabula , Maisha ya ushindi Ministry


Mara kwa mara maswali matatu hujitokeza kwenye mawazo
ya watu, na si ajabu yanajitokeza. Kwa maana majibu yake ni
ya maswali hayo muhimu sana.
Maswali hayo ni:

(a) Je, njia ya mbinguni ni katika msingi wa kifo cha Kristo
pekee katika msalaba wa Kalvari miaka elfu mbili
iliyopita na sisi tunahitaji kukubali hilo? Jibu la kiroho
kwa swali hili ni “Ndiyo” pasipo shaka lolote.

(b) Je, njia ya mbinguni baada ya maisha ya hapa duniani
inategemea msingi wa matendo yetu, jinsi tulivyofanya
vibaya au vizuri wakati tukiwa duniani? Jibu la Biblia
hapa ni “Hapana” na limetajwa bayana mara nyingi
katika maandiko.

(c) Je, kuingizwa kwetu mbinguni siku moja ni matokeo
ya jumlisho la jibu (a) na (b) hapo juu? Mwandishi
hakufanikiwa kabisa kupata andiko ambalo linaunga
mkono jibu la “Ndiyo” na hakuna yeyote aliyewahi kutoa
hata moja, kwa ufahamu wangu.

Mwisho wa yote, ni kile ambacho neno la MUNGU aliye hai,
lisilokuwa na kosa linavyosema ndicho cha kutilia maanani,
na sio maoni au ugunduzi wa mwanadamu yoyote au kundi la
watu bila kujali jinsi wanavyoonekana waadilifu.

MUNGU akubariki sana kwa tafakari hii na kama hujampa BWANA YESU maisha yako , wakati muhimu wa kufanya hivyo ni leo.



                                 Peter Michael Mabula
                              Maisha ya ushindi Ministry


 
 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments