John S. Shabani ni
mzaliwa wa kijiji cha Kirando katika kitongoji cha Nyankima, kata ya
sunuka, Wilaya ya Kigoma Vijijini, Nchini Tanzania. Ukoo wake ni waumini
wazuri wa dini ya kiislam (Islamic Religion).
Baada
ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi kirando, alijiunga
na elimu ya sekondari, lakini kutokana na itikadi za kidini, alijikuta
akiwa katika wakati mgumu wa kupigwa vita na wazazi, ni baada ya uamuzi
wake wa kujiunga na Dini ya kikristo. Hivyo John ameishi miaka mingi
akiwa mbali na wazazi wake, lakini hata hivyo hakukata tamaa.
John Shabani:Safari ya kuelekea Sudan |
Mwaka
1992, John akiwa kijana mdogo, alipata ufadhili wa kwenda nchni Kongo
(Zamani Zaire), ambako huko alijifunza muziki na kusoma Chuo cha Biblia
(Bible knowledge), na huko kipaji chake cha kutunga nyimbo na kuimba
kilijitokeza kwa kasi, hata akatokea kupendwa sana.
John
hakutaka kuona mtu yeyote akiwa katika hali ya kukata tamaa, maana
alifahamu madhara yake. Kwasababu hiyo, alianzisha vikundi mbalimbali
vya vijana akiwa na lengo la kuwaelimisha ili kujikwamua katika hali ya
kukata tamaa na kutokujihusisha na vitendo viovu kama madawa ya kulevya,
Ukahaba na anasa za kila aina, mambo ambavyo aliyapiga vita sana.
![]() |
JOHN SHABANI AKIWA NA RAIS JK KIKWETE |
John
ameishi miaka mingi kama yatima, lakini hali hiyo imemsaidia kujifunza
mengi na kuwa na tabia njema, kumheshimu na kumthamini kila mtu, mambo
yaliyompelekea kupata kibali machoni pa wengi hata kuwa mfano wa kuigwa.
Amekuwa msaada kwa Vijana wengi (Ndani na nnje ya nchi) na kuwakwamua
wengi waliokuwa wamekata tamaa na kujihusisha na vitendo viovu. Pia
kutokana na ujuzi wa muziki alioupata na pia kipaji kikubwa alichonacho
cha kutunga, kuandika nyimbo na kuimba, John amekuwa msaada kwa waimbaji
mbalimbali binafsi na vikundi ndani na nje ya nchi, hasa nyimbo za
Injili. Ni mwalimu bora na mshauri kwa waimbaji. Wengi waliopitia kwake
sasa ni waimbaji wazuri na maarufu.
Mwaka
2001 John alifunga pingu za maisha na binti aitwaye Debora Shabani na
mwaka 2002 walipata mtoto wa kike. Alimwita mwanaye Joyce, akiwa na
maana ya kuyasahau maisha ya huzuni na shida na kujitabiria maisha ya
furaha.

![]() |
John Shabani akiwa na Rose Muhando na Bahati Bukuku |
Tarehe 19/03/04, John alirekodi Album yake aliyoiita “Marufuku kukata tamaa”
Album
ambayo imewasaidia wengi waliokata tamaa na kuwapa matumaini mapya.
Album hiyo na nyingine alioirekodi mwaka 2009 inayoitwa “Huu ni wakati wangu”,
zimekuwa msaada mkubwa kwa kila aliye au anayezinunua, zimegusa na
kuinua mioyo ya watu wengi. Kwani amepokea shuhuda nyingi ndani na nnje,
hata za wale waliodiriki kujiua, lakini baada ya kusikiliza nyimbo hizo
waliahirisha. “Nakusii nunua kanda hizo, naamini zitakusaidia”. Pia utakuwa mchango wako kwa kutimiza ndoto na malengo ya John.
John
ametembelea nchi mbalimbali, akijifunza maisha ya watu. Amegundua
kwamba karibu asilimia kubwa ya wanadamu, awe maskini, tajiri, msomi au
asiye na elimu, wenye vyeo au waajiriwa, watoto kwa wakubwa, wanaume kwa
wanawake, awe mzungu au mweusi n.k, wote kwa njia moja au nyingine
wamepitia katika hali ya kukata tamaa au kukatishwa tamaa na jambo
fulani, mtu, watu, hali au mazingira fulani. Ndipo mwaka 2006, alipata
maono na msukumo mkubwa wa kuandika Kitabu ambacho kitakuwa msaada kwa
njia moja au nyingine kwa kila atakayekipata.
Tarehe
26.04. 2009, John alitunukiwa tuzo ya heshima pamoja na cheti
(certicate of appreciation) kwa kutambua mchango wake kwa ajili ya
kuinua vipaji na pia kuchangia kuinua muziki wa Injili Afrika mashariki
na kati. Pamoja na hayo amekua akianzisha makundi mbalimbali kwa ajili
ya kuwaelimisha kuhusu maisha ya kujitegemea, kujishughulisha na
kuhepukana na vitendo viovu kama wizi, ujambazi, utumiaji madaswa ya
kulevya, ukahaba n.k. Tuzo hiyo ilitolewa na kampuni moja maarufu
Tanzania yenye makao makuu jijini Dar es salaam (Christian promoters
Ltd).
John ameanzisha huduma inayoitwa Never give up “Usikate
tamaa” Ambayo anategemea kuisajili wakati wowote. Huduma hii, inalenga
kuinua vipaji, mipango na mbinu za kuwakwamua vijana au watu kujihusisha
na madawa ya kulevya, ukahaba, utapeli wizi, ujambazi nk, mambo
yanayosabisha magonjwa kama vile ukimwi, kufungwa jela au kufa
kabla ya wakati, matokeo yake kuacha wototo wengi yatima na wajane nk.
Pia kutafuta ufadhili kwa ajili ya kuaendeleza vijana ki-elimu pamoja na
kuwawezesha pale inapobidi. Kwa sasa anayo program inayoitwa Touching voice program (Darasa la uhimbaji)
Ni kwa ajili ya kwaya, Band/vikundi na waimbaji binafsi.
-Mwisho-

Comments