MWAMINI CHALUGAMBA: MWANA MAMA ALIYEAMUA KUIBUA VIPAJI VYA WAIMBA NYIMBO ZA INJILI

 Mwamini Godfrey Chalugamba
Mwamini Godfrey Chalugamba imemchukua takribani mwaka mmoja kuanzisha studio ya nyimbo za dini. Akiongea na Injili Forever Blog anasema amekuwa akivutiwa sana na uimbaji hasa wa Injili kitu ambacho kilimsukuma kuanzisha Studio ijulikanayo kwa jina la ALFA ONE LOVE PRODUCTION inayopatikana eneo la Yombo kilakala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. Tangu ameanza mpaka sasa kuna waimbaji wanne waliorekodi Album ambao ni Suzy Shango, Salome Mbulinyingi, Olga Haule, Mtumishi wa Mungu Gilbert na Rogers akifahamika kwa jina la The Gorgeous.




 Olga Haule


Rogers a.ka THE GORGEOUS
Pia kuna waimbaji wengi walio imba nyimbo moja moja au mbili kwa maana ya sio Album.

Kuhusu ubora wa kazi na bei viko tofauti kwa maana ya bei ni ndogo ila ubora uko juu lengo likiwa ni kuibua waimbaji wapya katika ulimwengu wa nyimbo za Injili pia Mwamini huwaunganisha waimbaji wake(wanao rekodi kwake) na redio mbalimbali zinazo tangaza nyimbo za dini za Jijini Dar es salaam na mikoani ikiwemo Iringa na Morogoro. Pia mmiliki huyo wa studio anamaono ya kuanzisha uzalishaji wa Video pia ili kuhakikisha waimbaji watakao rekodi hapo waupate ubora ule ule kwenye Video pia.

Kwa namba za mawasiliano za mmiliki huyo wa Studio ni +255714265757
 
 
                                                   


Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments