BWANA YESU
asifiwe watu wa MUNGU.
Ni nafasi
mpya MUNGU amenipa ili tujifunze jambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu,
jambo hilo ni ‘’NDOTO’’
Karibu.
-Jinsi
unavyoonekana katika hali ya mwili inaonyesha ulivyo katika ulimwengu wa roho.
Kamwe huwezi kuwa tofauti na jinsi ulivyo katika ulimwengu wa roho.
-Maarifa
uliyonayo huanzia katika ulimwengu wa roho na sio katika ulimwengu wa mwili
japokua unasoma katika mwili lakini asili yake ni katika ulimwengu wa roho.
-Mambo
yakikataliwa katika ulimwengu wa roho lazima yatagoma pia katika ulimwengu wa
mwili.
-Hali ya
ulimwengu wa roho huongoza ulimwengu wa mwili au ulimwengu huu unaoonekana.
Hebu ona, roho yako inapotengana na mwili hutokea kifo na hakuna mwanadamu
anayeweza kukurudishia tena uhai wako, labda iwe kwa nguvu za kiroho. Na huo
ndio muujiza uupatao kila siku.
BAADHI YA NDOTO KATIKA AGANO
LA KALE.
Abimeleki, kuhusu Sara (Mwanzo 20:3)
Abimeleki, kuhusu Sara (Mwanzo 20:3)
Yakobo,
kuhusu ngazi (Mwanzo 28:12)
Yakobo,
kuhusu Misri (Mwanzo 46:2)
Labani, kuhusu Yakobo(Mwanzo 31:24)
Yusufu , kuhusu wazazi wake na ndugu zake
(Mwanzo 37:5)
Yusufu, kuhusu jua, mwezi na nyota (Mwanzo 37:9)
Mnyweshaji
mkuu wa mfalme, kuhusu yeye mwenywe(Mwanzo 40:9).
BIBLIA IMEANDIKA WAOTA
NDOTO 14.
1.
Abimeleki
(Mwanzo 20:3-6)
2.
Yakobo
(Mwanzo 28, 31:10-11)
3.
Labani
(Mwanzo 31:24)
4.
Yusufu
(Mwanzo 37:5-10)
5.
Mlinzi
mkuu wa gereza (Mwanzo 40:9-15)
6.
Muokaji
mkuu wa mikate(Mwanzo 40:10-23)
7.
Farao
(Mwanzo 41:32)
8.
Wamidiani(Waamuzi
7:13-15)
9.
Suleimani
(1 Wafalme 33:5-15)
10.
Nebukadreza
(Danieli 2 na 4)
11.
Danieli
(Daniel 2 na 7)
12.
Yusufu
(Mathayo 1:20, Mathayo 1:13-22)
13.
Mamajusi
(Mathayo 2:12)
14.
Mke
wa pilato (Mathayo 27:19)
Nawe pia unaweza kuwa mmoja wa waota ndoto wa kizazi chako.
UMUHIMU WA NDOTO.
MUNGU hukuletea ndoto ili kukuelewesha msimamo wako katika
ulimwengu wa roho.
NDOTO NI
MAWASILIANO BINAFSI KATI YAKO NA MUNGU WAKO
Ndoto ni kitendo kinachotokea wakati umelala, hii yaweza
kutokea usiku au mchana, kama utakuwa hujalala siyo rahisi kujua jambo
linaloendelea katika ulimwengu wa roho.
Wakati unapokuwa umelala roho yako huwa na mawasiliano na
roho nyingine zilizo hai au unawasiliana na MUNGU katika ulimwengu wa roho
ambako mambo yote hutokea.
-Mambo yote yaliyoko katika hu ulimwengu wa mwili, yaani yale
unayoyaona asili yake ni katika
ulimwengu wa roho. Hakuna jambo lolote linaloweza kutokea katika ulimwengu wa
mwili kabla halijatokea katika ulimwengu wa roho.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula
Maisha ya ushindi Ministry

Comments