NENO LA KRISTO KWA KIJANA MWENZANGU

Na Sam Balele


MHUBIRI 11:9-10 imeandikwa hivi;

Wewe, kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako; LAKINI UJUE WEWE YA KWAMBA KWA AJILI YA HAYO YOTE MUNGU ATAKULETA HUKUMUNI. Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini wako; kwa maana ujana ni ubatili na utu uzima pia.

Biblia yaonekana kutoa ruhusa kwa kijana kuyafanya yale yaliyo moyoni mwake, kujifurahisha na yote yaliyo ndani ya uwezo wake na wakati mwingine hata yaliyo nje kwa namna yoyote ile ili mradi kuuchangamsha moyo wake. Na ndivyo vijana wengi wafanyavyo mchana na usiku, 24/7. Kwa neno la leo inaitwa KULA BATA. Biblia inatoa "green light" ukisoma hiyo verse 9a, lakini pia imetoa angalizo katika verse 9b, ambalo wanadamu wenye nia ya kupotosha hua wanakwepa kuisoma hiyo verse 9b.

WELL, endelea kula bata, endelea kuuchangamsha moyo wako wakati wa ujana wako ili uje umkumbuke Mungu ukishakuwa mzee na umekongoroka hata kumtumikia tena inakuwa ni kwa pole pole na udhaifu wa mwili kibailojia. Endelea tu Ruhusa unayo lakini pia Onyo ama Angalizo unalo.

Sasa unajua Mungu si dhalimu hata kidogo, amejaa haki kotekote, ndo sababu ametoa ruhusa, na pia ametoa onyo. Amekupa free will yaani nguvu ya uamuzi BINAFSI ili uchague mwenyewe lipi uonalo lina faida katika umilele wako KABLA hii dunia unayolia bata haijafikwa na tamati yake. Ukisoma katika Mhubiri 12:1, utaona pale anatoa angalizo lingine akisema; "Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala haijakaribia miaka utakaposema, mimi sina furaha katika hiyo [miaka]."

Mungu anawataka vijana wamtumikie, watumikie KUSUDI lake hapa duniani. Wayafanye yale yaliyo mapenzi yake. Mwimbaji Zaburi akaimba katika Zaburi 119:9, 10; " Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata Neno lako [Neno la Mungu]", akaendelea kuimba; " Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako, nisije nikakutenda dhambi."

Neno la Mungu ni Yesu Kristo, ukisoma Yohana 1:1 imeandikwa; " Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu" na 1 Yohana 5:8 imeandikwa; "Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba,Neno na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Mwimbaji Zaburi aliimba, akisema "Neno lako nimeliweka moyoni mwangu nisije nikakutenda dhambi."

Neno la Mungu ni Yesu, katika Ufunuo wa Yohana 3:20, Bwana Yesu anasema; '"Tazama nasimama mlangoni, nabisha hodi." Amesimama katika mlango wa moyo wako kijana, anabisha hodi, wakati huu angali ukiwa kijana, amekuwahi mapema kabla hujawa mzee na umechoka mwili kwakuwa ana KUSUDI na wewe kijana. Ana WITO na kazi ya kukupa ufanye kwa ajili ya Ufalme wa Mungu hapa duniani. Sasa Mungu Baba ameweka mbele yako ile Ruhusa ya kula bata na kuuchangamsha moyo wako au Kuitika hodi ya Mwana wa Mungu Yesu Kristo ili usije ingia hukumuni, kama ilivyoandikwa katika Ufunuo 20:11-15.

Unapoitika mwito wa Mungu Baba, jina lako linaandikwa katika Kitabu cha Uzima, hivyo kamwe hutoingia hukumuni na wana wa uasi na ukaidi wa kizazi hiki. The power to decide imewekwa kwako; KULA BATA ama HUKUMUNI. Amua leo kuepuka hukumu kwa kumfungulia Bwana Yesu mlango wa moyo wako. Yeye akiwa ni Neno aingie moyoni mwako kwa njia ya Roho Mtakatifu. Uanze kuishi maisha ya Wokovu kwa uaminifu wote kwa neema ya Mungu, ukidumu ndani ya Neno la Mungu na usaidizi wa Roho Mtakatifu. Ukidumu katika tumaini la urithi wa uzima wa milele kwa njia ya Yesu Kristo.

Kijana mwenzangu usifanye mzaha wala dhihaka, haya mambo ni serious business, DINI, imepunguza sana uzito wa haya mambo na kufanya tuyaone ni hadithi za Biblia lakini nakwambia haya mambo ni SERIOUS BUSINESS. Ni dua yangu kwako usomaye hii post, Mungu akufungue macho yako uone hali halisi, na moyo wako utiwe ufahamu ili ufanye uamuzi wa kuiponya roho yako na hukumu ya Mungu yaani hiyo mauti ya pili.

Amua leo, kumpokea Yesu na kuachana na mambo ya dunia hii. Hii dunia inapita pamoja na mambo yake yote, starehe zote zinapita, kujichangamsha kote kunapita, KULA BATA kote kunapita. Mwisho wa siku ni hukumu na hutakuwa na udhuru mbele za Mungu, kwakuwa vijana wengine kama mimi tutakuwa mashahidi wa uamuzi sahahi tuliofanya, hali wewe ukifanya uamuzi usio sahihi na kuikumbatia dunia na mambo yake. Mimi ujana wangu nimeamua kumpa Yesu Kristo na nitakuwa mtumishi na shahidi wake kwa watu wangu na mataifa. Nimechangua fungu lililo jema. Starehe na uchafu mwingi nimefanya, labda kukuzidi hata wewe. Sasa nawe Mungu akupe rehema uchague fungu lililo jema.

Amua leo kumpokea Yesu Kristo, upokee Wokovu wa roho yako, UANZE SAFARI.

Sema sala hii
Bwana Yesu, nimesikia kubisha kwako hodi mlangoni pa moyo wangu. Ninafungua mlango saa hii na kukuruhusu uingie ndani ewe Neno la Mungu. Karibu ndani ya moyo wangu kwa Roho wako Mtakatifu. Ninatubu dhambi zote nilizotenda kwa mawazo ya moyo, maneno ya kinywa na matendo ya mwili wangu. Nakuomba unisamehe, unitakase kwa damu yako niwe safi kuanzia leo. Futa jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima. Nakukabidhi ujana wangu na maisha yangu yote kuanzia saa hii. Naomba unimiliki niwe mali yako, niongoze na moyo wangu upendezwe na njia zako tu. Asante Bwana Yesu kwa upendo wako. Mimi sasa nimeokoka. Nakukabidhi maisha yangu uyatawale Bwana.

Kama umeisema sala hii, basi amini kuwa umeokoka, umepokea zawadi ya wokovu kutoka kwa Mungu Baba. Sasa umeanza safari na Bwana Yesu; ikiwa umeanza safari basi wahitaji kuwa karibu na wasafiri wa aina yako. Hivyo kuwa karibu na mtu aliyeokoka upate msaada zaidi. Pia waweza kuwasiliana nami kwa msaada zaidi.

Namba: 0653 200451
Mungu akutie nguvu katika kufanya uamuzi sahihi angali ukiwa kijana. Usisubiri uzeeni.


 
 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments