![]() |
Amewataka waumuni wa kikatoliki kujiunga na mfumo wa dijitali. "Internet... inatoa nafasi ya mafanikio mengi. Hiki ni kitu kizuri bila shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,'' alisema Papa.
Papa mwenyewe ana akaunti kwenye Twitter ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni kumi.Katika ujumbe wake kwa dunia nzima ambao hutolewa kila mwaka, Papa amesema kuwa mfumo wa dijitali, unapaswa kuwa mtandao wa watu wala sio nyaya tupu.
Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu kukutana na kujuliana hali.
Kadhalika amewataka waumini wa kikatoliki kutodhani kuwa ni mawazo yao na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati wakiwasiliana na watu wa dini nyinginezo.
CHANZO: BBC SWAHILI
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12
Comments