PESA na WEWE





Jifunze chanzo cha HELA/UTAJIRI. Matatizo mengi katika JAMII leo yanakuja kwa sababu watu wanadhani chanzo cha PESA ni MIRADI na UJASIRIAMALI na wameweka nguvu NYINGI huko na kusahau MSINGI wa UTAJIRI wao ndio maana inakua TATIZO.

Huwezi kua na hela kama huna NGUVU. Tunaambiwa “utamkumbuka Bwana Mungu wako kwa maana yeye ndiye AKUPAYE NGUVU ya kupata UTAJIRI” (Kumb). Sasa CHANZO cha hela ni NGUVU ambayo Mungu ameweka ndani ya watu kwa form ya KIPAWA (talents). Hakuna UHUSIANO wa hii nguvu na UCHA-MUNGU au UTAKATIFU wako, ndio maana Yesu anasema “ni vyepesi ngamia kupenya tundu la sindano KULIKO tajiri kuingia Ufalme wa Mungu”. Ikimaanisha kwamba unaweza kua na mahela yote na ni Mungu kakubariki kweli ila Mbingu ukaisikia tu kwa akila LAZARO.

Nimewahi kujiuliza sana hivi ni kwaninii kuna watu hata hawamjui huyu Yesu ila wana PESA ndefu na wanapata kila siku, hapo pembeni kuna MPENDWA hana hata ya kupanda daladala anapiga ngoko na jua kali la Dar. Nikagundua SIRI nyingine. Kukua kwa HICHO KIPAWA/NGUVU ya kupata PESA/UTAJIRI inakutegemea wewe mwenyewe na HALI na MAZINGIRA ya MOYO wako ndio yatasema hatua utakazofika. Hebu fikiri yule jamaa anaitwa SEWA HAJI. Katoa tu hela (SADAKA) yake na kujenga hospitali ya Muhimbili hapo, hadi kesho watu wanapata msaada hapo, masikini na matajiri. Huo MOYO wa REHEMA uliomsukuma KUTOA ni MAZINGIRA safi sana ya KUNASA pesa na utajiri kuliko kawaida. Hapo pembeni kuna MPENDWA amezungukwa na WAJANE, YATIMA, na WAHITAJI mbali mbali hata HASTUKI, utasikia anatumia maandiko “asiyefanya kazi kula na asile” kumbe ni UCHOYO tu hapa. Sasa kesho unasikia BAKRESA kagawa mamilioni kusaidia masikini, Mengi kaandalia KARAMU walemavu DIAMOND JUBILEE, nk. halafu unadhani mtakua na NGUVU sawa ya kupata UTAJIRI! Subiri hapo sana utashangaa..

Kwa kadri mtu anatumia kipawa chake kwa UAMINIFU na KUMBARIKI Mungu na wanadamu, kama akina Korinelio, jua ile NGUVU ya KUPATA pesa/utajiri inakua ACTIVATED, inaanza kufanya kazi na kuvuta hela/utajiri. Sasa LENGO (primary goal) la KUFANYA jambo haliwi tena KUPATA pesa ila KUHUDUMIA Jamii na kazi ya Mungu (HUDUMA), huko mbele mambo yanageuka kua MGODI wa DHAHABU! Unashangaa tu hela inakuja, ila UTOSHELEVU unakuja pale unapoona MALENGO ya KIJAMII na HUDUMA yanakua na sio KIPATO kinakua! Ukiona unashangilia kipato kikikua na sio KIPAWA chako KUKUA jua unapoteza ile NGUVU ya kupata HELA taratibu..chunga hapo ni muhimu kujua MOYO wako ndio KITUO cha KUACHILIA na KUPOKELEA kila kitu kwa imani. Mungu awabariki.

Sijakosea kuanza na i. kuhudumia jamii na ii. Kazi ya Mungu (huduma). Huwezi kujifanya busy unapeleka hela kwenye kazi ya Mungu na umesahau wanadamu (wajane, masikini, yatima na wahitaji) hapo pembeni. Kumbuka mfano wa MLAWI na KUHANI walioacha mtu kajeruhiwa hapo wanawahi HEKALUNI na MSAMARIA mwema anapita na kufanya kitu SAHIHI. Huu mfano Yesu alitoa kukupa priority katika UTOAJI. Mungu akupe kuona hii kitu. Ndio maana tuansoma “ninachotaka sio sadaka ila REHEMA” (Mika 6). Ukiwa na Rehema UTAWAHURUMIA watu na kuwasaidia [kuwapa sadaka kama Korinelio] na sio unajifanya busy huko HEKALUNI tu, sawa ni MUHIMU sana kuwekeza huko mahekaluni ila chunga usisahau JAMII.

                                      By Frank Philip

 
 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments