SI KILA JAMBO LINA FAIDA

Na Sam Balele


Siyo kila kitu mtu akitendacho ama akifanyacho kwa wakati fulani ni dhambi [sin], la hasha, yawezekana si dhambi [sin] kabisa; ila yawezekana ikawa ni kosa [wrong doing] ambalo litampelekea kutenda ama kufanya dhambi [sin]. Kwa mfano kitendo cha mtu kuangalia movie series ya Supernatural yawezekana isiwe dhambi, lakini ni ikawa ni kosa ambalo laweza kumpelekea akatenda dhambi kutokana na elimu potofu ambayo mtu anajifunza mule, ambayo yapingana na elimu sahihi ya Mungu itokanayo na Biblia. Mfano mwingine ni kuangalia Pornography, yawezekana kabisa hicho kitendo cha kuwatch pornography kisiwe dhambi, sababu mtu atasema nionyeshe andiko linalozuia kuangalia sex movies kutoka katika Biblia; hivyo kuangalia yaweza isiwe dhambi katika hekima hiyo, lakini kuangalia huko kukawa ni kosa [wrong doing] ambalo litasababisha mtu atende dhambi baada ya kujiwakisha tamaa na kuishia katika vitendo vya uchafu wa ngono kama punyeto, usagaji, uasherati na uzinzi.

Ndiposa Biblia inasema, kuwa, "All things are permissible but not all things are beneficial." Unapoangalia movie series ya Vampire diaries, inakufundisha nini na kukupa faida gani in relation to God's. If it does not, tupia kule. Unapoangalia movie series ya Heroes inakufundisha nini juu ya Mungu? If it does not tupia kule. Unapoenda kukesha Mafian lounge, Level 8, Escape, Savanah lounge etc, inakufundisha nini juu ya Mungu? Inakujenga nini kiroho in relation to God's? If does not tupia kule. For instance; Unapofanya kazi ama biashara safi na halali, inampa Mungu utukufu na inakufundisha kitu juu ya Mungu, kwa sababu Mungu amesema...'Asiyefanya kazi na asile".

Jikague yale uyatendayo ikiwa unakiri kuwa wewe ni mwanadamu unayemfuata Mungu wa kweli. Kila utendalo ni lazima liwe linakufundisha kitu juu ya huyo Mungu, ni lazima liwe linamtukuza Mungu aidha in the process ama in the end. Kama Mungu hatakuzwi katika lile jambo mtu atendalo basi hilo litendwalo lapaswa kutupwa nje,lapaswa kutupwa kule mbali kabisa, kwa sababu japo laonekana ni la kawaida na halina athari, laweza kuwa sababu na uchochoro wa Dhambi, na mshahara [wages] wa dhambi [sin] ni mauti [death].

BIBLIA inasema hivi katika MITHALI 16:9
"MOYO WA MTU HUIFIKIRI NJIA YAKE; BALI BWANA HUZIONGOZA HATUA ZAKE"

ZIFIKIRI NJIA ZAKO. ZIFIKIRI NYENDO ZAKO.HAKIKISHA ZIKO SAHIHI NA BWANA MUNGU ATAZIONGOZA HATUA ZAKO. KINYUME CHA HAPO, SHETANI ATAZIONGOZA HATUA ZAKO NA MWISHO WAKO HAUTOKUWA MZURI. MUNGU ANAKUKUMBUSHA KILA IITWAPO LEO. FANYA UAMUZI SAHIHI NA ITAKUWA HERI KWAKO MWANADAMU.
 


 
 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments