BWANA YESU
asifiwe rafiki popote ulipo.
Nakukaribisha
sana katika ujumbe huu mhimu wa kujua na kufahamu juu ya taifa la Israel. Ndugu rafiki wa
Maisha ya ushindi hakika utabarikiwa na kujifunza kitu muhimu sana .
Karibu.
"Magen David" au nyota ya Daudi ni ishara ya Uyahudi, |
Israel ni
taifu la MUNGU, nikisema ni taifa la MUNGU ni kwa sababu MUNGU mwenyewe
alilichagua taifa hili. Tunaona mataifa mengi mfano ya kiafrika yalitokana na
Berlin conference au mkutano wa Berlin wa mwaka 1984 chini ya uenyekiti wa mkuu
wa taifa la ujerumani Bismark ambapo wakuu wa mataifa ya ulaya waliligawa bara
zima katika nchi ndogondogo kwa leo lao la kutawala katika makoloni hayo, hata
Tanzania, Kenya, Uganda,Burundi, Rwanda, Zambia,Msumbiji, Kongo na hata Malawi
ndipo yalipoanzia katika mkutano huo, vivyo hivyo mataifa mengine kama marekani
au Brazil yalianza kutokana na mipango ya wanadamu fulani katika dunia hii
lakini tukiizungumzia Israel tunazungumzia taifa ambalo halikutokana na vikao
wala mikutano yeyote ya kibinadamu bali MUNGU mwenyewe ndie alipanga huko
mbinguni, Hivyo Israel ndilo taifa pekee ambalo kuwepo kwake kuwa taifa ni
mipango ya mbinguni. Na chanzo cha taifa
hili ni kuitwa na MUNGU kwa Ibrahimu (Mwanzo 12 :1-3, BWANA akamwambia Abramu,
Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka
nchi nitakayokuambia. Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki na
kulikuza jina lako; nawe uwe baraka. Nami nitawabariki wakubarikio, naye
akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa).
BWANA YESU
asifiwe! Huo ndio ukawa mwanzo wa taifa hili la MUNGU, Kumbe ukiwalaani Israel
utalaaniwa na ukiwabariki utabarikiwa, aliyesema ni MUNGU wala sio mwanadamu.
Kumbe mimi Peter Michael Mabula natakiwa kuwabariki Israel kama neno la MUNGU
linavyosema na wewe ndugu yangu hakikisha unalibariki taifa hili na kuliombea
pia.
Tunafahamu
Ibrahimu alimzaa Isaka ambaye ndiye aliyebeba kusudi hili la MUNGU baada ya
Ibrahimu na Isaka akamzaa Yakobo ambaye alilibeba kusudi hili la MUNGU. Na
Yakobo akazaa watoto 12 ambao baadae walikuwa makabila 12 ya Israel.
-Jina
ISRAELI linatokana na jina la pili
alilopewa Yakobo na Malaika baada ya mashindano yake na Malaika wa MUNGU huko
Penuel. Israeli maana yake ni ‘’aliyeshindana na MUNGU Mwanzo 32:28). Hilo jina ISRAEL alilitoa
MUNGU kwa kwa baba mkuu wa taifa hili la Israel.
-Waisrael
huitwa wayahudi, MYAHUDI ni jina linalotokana
na jina la YUDA mwana wa 4 wa
Yakobo(Mwanzo 29:35, Maana ya Yuda ni sifa kuu) na kwa jina la kitaifa yaani
wayahudi mwanzo lilihisu watu wa kabila hilo tu yaani kabila la Yuda au Wayuda
au wayahudi. Baada ya kugawanyika kwa ufalme (950 K.K) lilikuwa na ufalme wote
wa kusini yaani Benjamini na Yuda (2
Wafalme 16:6, Yeremia 32:12), na baada ya kurudi kutoka kifungo cha Babeli(538
K.K) Lilikuwa ni jina la makabila yote 12 (Mathayo 27:29,37)
Bendera ya Israeli |
-Pia
waisraeli wanaitwa waebrania, Jina WAEBRANIA linatokana na jina la Eberi(Maana
yake ‘’mtu wa ng’ambo’’ Mwanzo 10:21,24, Mwanzo 11:14-15), na inaonekana kama
jina hili linahusiana na uhamiaji wa ukoo wa Ibrahimu tusioujua uliotoka ng’ambo ya mto yordani, Eberi
alikuwa alikuwa wa saba kabla ya Ibrahimu, pia alikuwa babu mkuu wa washemi
wengine kama vile Ofiri na Havila(Mwanzo 10:25-30), kwa hiyo neno waebrania hapo mwanzo lilihusu ukoo mkubwa kabla ya
Ibrahimu Tazama Mwanzo 14:13, Mwanzo 39:14,17, Mwanzo 43:32. Katika unabii wa
Balaamu (Hesabu 24:24), Eberi anatajwa pamoja na Ashuru, Baada ya muda mrefu
jina hilo liakawa la taifa moja la agano la kale, likitofautiana na makabila
mengine ya ukoo huo mkubwa( Kutoka 5:3, 1 Samweli 4:6, Yoha 1:9)
Israel ni
muhimu sana kwa kanisa na waenda mbinguni wote ambao wanampa BWANA YESU maisha
yao.
ISRAELI NI KATIKATI YA DUNIA.
-Israeli
inasemwa kuwa ipo katikati ya
dunia(Ezekieli 38:12c-wakaao katikati ya dunia.
) yaani Israeli ni kama daraja la kati ya mataifa makuu
katika ulimwengu wa kale, ni mahali ambapo bara kuu 3 za duniani zinakaribiana
sana yaani Afrika, Ulaya na Asia. Ndio maana mataifa ya Misri, Uashuru na
Babeli yalipigana vita ili kulipata daraja hilo.
-Israeli
ilifaa zaidi ili kutoka huko injili
ipelekwa duniani maana Yerusalemu iko kati ya mataifa (Ezekieli 5:5 BWANA MUNGU asema hivi; Huu ndio Yerusalemu; nimeuweka kati ya mataifa, na nchi zauzunguka pande zote.
-)
KAZI YA
ISRAELI
1.
Israeli ilikuwa mpokeaji wa ufunuo wa MUNGU na
makao makuu ya Mwokozi YESU KRISTO wetu alipokua duniani.
2.
Israeli
ilikuwa chanzo cha kanisa la
KRISTO(Yohana 4:22-Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. ) pia Warumi 11:16-24
3.
Ilitakiwa
kuandaa njia ili injili iyafikie mataifa yote yaani iwe mfereji wa ufunuo wa
wokovu duniani kote.
4.
Israeli
lilikuwa taifa lililotengwa na mataifa mengine, yaani lilikuwa taifa la tofauti
kabisa na mataifa ya kipagani.
5.
Israeli
ni taifa la ufunuo, linalomjua MUNGU wa
pekee aliye hai.(Zaburi 83:18 -Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.
).
6.
Israeli
ni taifa ambalo MUNGU aliwajulisha mapenzi yake
kupitia Manabii na watumishi wake mbalimbali.
7.
Israeli ni mzaliwa wa kwanza wa mataifa yote, ni lango kwa mataifa mengine yote.
Hakuna aliye kama MUNGU wa israeli, na ni watu walio na ukipekee mwingi
na unaweza kuona hata kipindi Hitler kiongozi wa ujerumani akiwatesa waisraeli
katika vita kuu ya pili ya dunia ni kwa sababu ya vipaji vya kipekee
walivyonavyo waisraeli maana kwa miaka michache madaktari wataalam walikua wao,
na watalaamu wa mambo mengine mengi walikua ni wao hivyo kiongozi huyo akaana
kuwa kuwaacha hawa waishi watachukua idara nyeti za taifa huku wakiwa watumwa.
Na hata leo Marekani kuna waisraeli ambao ni wataalam wa hali ya juu katika
sekta nyeti kwenye taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani na ukiibariki Israeli
hakika unabarikiwa na wewe kama ilivyo kwa marekani.
Naamini kwa sehemu umejifunza kitu cha muhimu sana kuhusu Israeli, na
hakika hawa ni wa kipekee na ndio maana MUNGU hakuwahi kuita MUNGU wa taifa
lolote ila ni MUNGU wa Israeli.
Kanisa pia ni uzao wa Ibarahimu wa jinsi ya rohoni na warithi sawa sawa
na ahadi (Wagalatia3:7-14.Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
Na andiko, kwa vile lilivyoona
tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani,
lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa
yote watabarikiwa.
Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.
Kwa maana wale wote walio wa
matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa
kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati,
ayafanye.
Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.
Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo.
KRISTO alitukomboa katika
laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana
imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika YESU KRISTO, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.)
MUNGU wa Israeli awabariki sana na kama hujaokoka ndugu fanya hivyo leo
maana hakuna uzima wa milele kwingine nje na BWANA YESU (Yohana 14:6-YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi.
, PIA Matendo
4:12-Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina
jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa
kwalo.
), BWANA YESU anakuhitaji ndugu ambae hujampokea maana alikufa mara moja
ili wewe uwe hai milele katika yeye. Mpe maisha yako leo.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu
yako Peter Michael Mabula
Maisha
ya ushindi Ministry.
0714252292
HAKUNA ALIYE KAMA
MUNGU WA ISRAELI.
Amen.

Comments