Tafuteni kwanza ufalme wa MUNGU.

Mwinjilist Daudi Makubi
"Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa" ( Mathayo 6:33)
Kutokana na maneno haya ya Yesu Kristo,tunapata msingi wa tatu ambao ukiuelewa na ukautumia,unaweza ukawa na uchumi mzuri sana!Msingi huo ni huu: Tafuta kwanza ufalme wa Mbinguni na haki yake, na hayo yote unayoyatafuta katika uchumi utapewa na kuzidishiwa."
Ukisoma
Mathayo 6:24-34
utaona ya kuwa Yesu alipokuwa anasema "na hayo yote mtazidishiwa" alikuwa na maana ya mavazi, vyakula na mahali pa kulala. Kwa tafsiri iliyo laini na nyepesi ya
Mathayo 6:24-34,
Yesu Krsito alitaka watu wake tujue ya kuwa,Mfumo wetu wa maisha na matokeo ya kuishi kwetu,kunaonyesha ya kuwa kuna kitu ambacho mioyo yetu inakitafuta.Inaonyesha ya kuwa mipangilio ya vipaumbele vya maisha yetu,kuna kitu tunachokitafuta tena baada ya kuona ya kuwa tumekipoteza.Kwa hiyo kwa kufundihsa alichofundisha katika

Mathayo 6:24-34,
Yesu Kristo anasema na mioyo ya watu ya kuwa
1. Mpangilio wa vipaumbele (priorities) vyenu vinavyosukuma utafutaji wenu wa maisha umekosewa.Mlitakiwa mtafute kwanza ufalme wa Mungu.

2. Mnachokitafuta sicho chenyewe ambacho mioyo yenu ilikipoteza katika maisha. Kwa hiyo mioyo yenu inabaki kusumbukia(worry) maisha haya,kwa kuwa haipati kile ambacho hasa ndicho inachokitafuta.

3. Kwa kuwa vipaumbele vya maisha yenu havijalenga kupata hasa kile machotakiwa kukipata,...mioyo yenu bado inadai kuendelea kuhangaika kutafuta hata baada ya ninyi kupata kile mlichofikiri kitaridhisha mioyo yenu baada ya kukipata...na kumbe si chenyewe.

4. Matokeo ya mipangilioo ya vipaumbele vya utafutaji wenu,ni kuwa na maisha ya kitumwa na ya kujisumbua na ya mahangaiko,na yaliyojaa hofu ya kesho itakuwaje?!

5. Mnatafuta maisha kwa kuwa mnadhani mlipoteza maisha wakati hamkupoteza maisha,bali mlipoteza ufalme wa Mungu ambamo ndani yake kuna maisha mnayoyatafuta.

Kwa Hiyo ikiwa unatafuta maisha mazuri,NInakushauri kama Yesu alivyosema,usitafute maisha mazuri,bali tafuta kwanza ufalme wa Mungu utapata maisha unayoyatafuta. NInaamini utafanya "homework" yako ya kutafuta katika Biblia ufalme wa MUNGU ni mfumo wa maisha yenye mpangilio ya vipaumbeke vya namna ya KIMUNGU.
Ameeeeeeen!


                      By Mwinjilist Daudi Makubi


 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments