TUNAHUBIRI NINI?

na Sam Balele


Kila kitabu katika Biblia kina sababu ya kuwemo ndani ya Biblia. Kuna kitu cha kujifunza kutoka katika kila kitabu ndani ya Biblia. Roho Mtakatifu ana lengo jema kwa kuwapa waandishi hekima ya kuandika. Kitabu cha Matendo ya Mitume ni kitabu chenye faida sana, kinaonyesha tabia na mwenendo na utendaji wa Kanisa unavyopaswa kuwa. Kanisa la kwanza lilikuwemo katika kipindi ambacho madhehebu pia yalikuwako, ndomana Injili ya Yesu Kristo ilipohubiriwa sawasawa na Agizo la Bwana watu waliamini na kuachana na mapokeo ya madhehebu yao na kumuamini Kristo, wakashikamana na Yesu Kristo na siyo dhehebu liitwalo kanisa. Madhehebu yaliyowazi kipindi hicho ni lile la mafarisayo na masudakayo, na walikuwa wanatumia vitabu vya torati na manabii kama ambavyo Kanisa la kwanza lilikuwa linatumia katika kumhubiri Bwana Yesu Kristo. Sasa unajua Kanisa kuna sehemu linaitwa dhehebu la Wanazorayo ukisoma katika kitabu cha Matendo ya Mitume na Paulo ndo alionekana kama kiongozi wa hilo dhehebu, lakini Paulo hakuhubiri dhehebu na wala hakuanzisha dhehebu, the only thing Paul preached was Jesus Christ and His merciful and gracious gift of Salvation, Watu wasioamini ndo walimuona kuwa ni kiongozi wa hilo dhehebu waliloiita la wanazorayo (kwa wasomaji wa Biblia watakuwa wanalijua hili). Injili waliyohubiri wenzetu ukisoma kitabu cha Mitendo ya mitume ndo Injili ipaswayo kuhubiriwa hata leo. Walimhubiri Yesu, walihubiri Wokovu, yule mlinzi wa gereza alipowauliza Paulo na Sila afanye nini ili aokoke...walimpa jibu moja tu ambalo ndilo lilikuwa message ya Injili waliyohubiri wenzetu. Soma Matendo ya Mitume 16:30-31.

Ukisoma hilo andiko hapo juu utaona kuwa hawakumwambia shika torati ama shika manabii, ama shika kitu fulani bali walimpa jibu moja tu, soma hapo utaona,nataka usome hivyo soma, tafuta Biblia usome. Sasa yaweza kuonekana kuwa walimpa jibu rahisi sana tena fupi na halikuwa na namba namba lakini nakwambia lile halikuwa jibu rahisi,ni jibu kubwa mno ukianza kufunua maana yake, sasa hebu rejea habari hii katika Mathayo 19:16-22. Kumuamini Yesu ni kumfuata Yesu, ukimfuata Yesu anajifunua kwako, kwakuwa utakuwa ndani yake naye ndani yako kwa jinsi ya Roho Mtakatifu. Ukiwa hivi ndipo unakuwa na personal relationship na Yesu na huo ndo mpango wa Mungu kwani yeye ni Mungu wa uhusiano, aliwatembelea Adamu na Hawa jioni wakati wa jua kupungua to fellowship with them, sasa yawezekana aliwatembelea sikuzote jioni ama aliwatembelea jumamosi tu lakini mimi naamini aliwatembelea kila siku pale bustanini, kila siku jioni wakati wa jua kupunga to fellowship na uumbaji wake. Hawa walikuwa wamezaliwa na Mungu na Mungu alifellowship nao sana tu, lakini badae likatokea anguko, wakamtenda Mungu dhambi na wanadamu wote wakahesabiwa dhambi including you and me na hao watakaozaliwa kesho. Ndipo hapo linapokuja suala la kuzaliwa mara ya pili, ambalo Bwana Yesu alimwambia farisayo Nikodemo katika Yohana 3:3. Kuzaliwa mara ya pili ni kurejeshwa kwa imani katika uhusiano ule uliokuwako kati ya Mungu na mwanadamu kabla ya anguko, ukisharejea hapa basi fellowship yako na Mungu haiwi limited to days and hours, whether it is saturady or sunday, yes the Romans changed a few things, history iko wazi but that does not stop God to fellowship na walio wake, fellowship nae jumamosi, fellowship nae jumapili, fellowship nae monday, fellowship nae jumanne, fellowship nae jumatano, fellowship nae alhamisi, fellowship nae ijumaa...the whole week. Huyu ndiye Mungu wa bustani ya Edeni. Zaidi ya hapo ni kushindana kiitikadi tu.

Sheria ilikuja ili niijue dhambi, na nilipoijua dhambi bado hiyo dhambi ilinishinda kwakuwa ufahamu wangu wa dhambi haunifanyi niishinde dhambi, ndomana hapa mtu anashika sana kitu fulani lakini katika kushika kwake huko bado unaona kiburi, majivuno, kujikweza, dharau, kujiona bora, na mengineyo ambayo ni dhambi, sasa utaenda kwa Mungu yupi na uchafu wote huo hata kama umeshika Amri 10. Bwana Yesu alilijua hili ndomana akamwambia yule kijana UZA VYOTE ACHA YOTE NIFUATE MIMI. Kuzishika amri za Mungu yahitaji neema, amri za Mungu ni mzigo mzito, imagine kuzini tu si lazima ufanye kitendo alisema Bwana Yesu, hata kuua si lazima uue hata kuchukia tu ni sawa na umeshaua. Nani anaweza kuzishika Amri za Mungu hapa duniani? Ni Yesu pekee aliweza na Biblia inasema alizishika na hakutenda dhambi, sasa ukishakuwa na Yesu ndipo mengine yanawezekana na si kabla ya hapo, ndomana Paulo na Sila walimpa yule mlinzi wa gereza JIBU LILE kwakuwa waliijua siri. Mafundisho yako mengi duniani lakini si yote ni sahihi na si yote ni ya Roho Mtakatifu hata kama yamekuja kwa maono, na ndoto na unabii, kwani hata "dini ya baba mdogo" imetokana na maono ya malaika Jibril, sasa mimi sijui juu ya hizo nyinginezo ila lazima kutakuwa na viumbe vya roho vilivyohusika, na Shetani ni COPYCAT mzuri tu.

TUACHE POROJO SASA TUHUBIRINI INJILI KWA JINSI ILE ROHO MTAKATIFU ALIVYOWEKA KUMBUKUMBU KATIKA KITABU CHA MATENDO YA MITUME. KANISA LA KWANZA HALIKUWA NA POROJO NA MALUMBANO YASIYO NA FAIDA. HISTORY YA NANI ALIFANYA NINI IACHWE KWA WANAHISTORIA, WEWE KAMA NI MTUMISHI WA MUNGU NA SHAHIDI WA YESU KRISTO BASI CHEKI WALE WALIOTANGULIA WALIHUBIRI KWA JINSI GANI. IKIWA WALIKOMAA NA AGENDA FULANI BASI IJUE HIYO AGENDA KWA KUANGALIA MAHUBIRI YALIYOKUWA RECORDED IN THE BOOK OF ACTS AND PREACH HIVYO. CHEKI MAHUBIRI YA PETER, STEPHEN, PHILLIP AND PAUL AND YOU WILL SEE THE MAIN AGENDA. AND PREACH THAT AGENDA, THAT MESSAGE.

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments