TUNAJIFUNZA NINI KWA HABARI YA LAZARO ALIYEFUFULIWA NA BWANA YESU *sehemu ya pili*

Na Mtumishi Gasper Madumla


"Naye Yesu aliposikia,alisema,Ugonjwa huu si wa mauti,bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu,ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo." Yoh 11:4

Basi,nakusalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo wa Nazareti aliye hai;
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...

Neno linasema,"...Ugonjwa huu si wa mauti..."
Yamkini upo ugonjwa kwako,
Yamkini upo ugonjwa kwa mwanao,
Yamkini upo ugonjwa kwa mumeo/mkeo,
Yamkini mtu mmoja anaumwa hapa,
Ooh..Nasema Yamkini yapo mateso kwako,
Yawezekana una kisukari,
Yawezekana una presha,
Yawezekana una pumu,
Yawezekana una maralia isiyosikia dawa,
Yawezekana una uvimbe ndani yako.

BWANA anasema Leo;
UGONJWA HUU SIO WA MAUTI.
Nami leo hii nakutangazia kupona kwako katika jina la Yesu Kristo aliye hai.

Lazaro alipokuwa hawezi,kwa ugonjwa aliokuwa nao,hapo ndipo Bwana alipoanzia.
Dawa ya ugonjwa wa Lazaro ni Yesu mwenyewe,alikadhalika dawa ya ugonjwa ulionao ni Yesu pekee,hakuna mwengine awaye yote,maana imeandikwa;
"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote,kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo." Matendo 4:12.

Ugonjwa ulionao ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu,ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.
Jambo moja jingine tunalojifunza siku ya leo kupitia habari hii ya Lazaro ni kwamba,
MAGONJWA SIO YA MAUTI,BALI YAPO KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU.

*Unaweza kushangaa sana kusikia ya kwamba magonjwa sio ya mauti Bali ni kwa ajili ya UTUKUFU kwa Bwana. Ugonjwa wa Lazaro ulikuwa sio wa mauti,Bali kulipa jina la Bwana utukufu.

Bwana Yesu aliacha ile hali ya Lazaro aliyekuwa hawezi,azidi kukaa katika hali hiyo hiyo na ili LAZARO APITIE HATA MAUTI ili jina la Bwana lipate utukufu na mwana wa Mungu atukuzwe. Si kana kwamba Bwana Yesu alishindwa kuachilia uponyaji kwa Lazaro pale tu alipokuwa hawezi,Bali ilikuwa ni kwa ajili ya utukufu wa Bwana.

Inawezekana yupo mtu kama Lazaro ambaye muda huu anaumwa sana,nami nakuambia leo hii,hali hiyo ipo hivyo ili Bwana ajitwalie utukufu na ili mwana wa Mungu atukuzwe.
Maana pia yawezekana umejaribu kutumia dawa nyingi sana,hata yawezekana umeshakwenda kwa waganga wa kienyeji lakini hali yako bado iko hivyo hivyo tena hali hiyo ndio imekuwa mbaya zaidi,

Lakini leo Bwana asema; ugonjwa huo sio wa mauti,Bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Mungu hutukuzwa hata kupitia magonjwa,
Mwana wa Mungu hutukuzwa hata kupitia magonjwa.
Leo kupitia fundisho hili tunataka tukamtukuze na tukampe Mungu utukufu kupitia kila aina ya ugonjwa,maana Yeye Bwana Mungu ataponya.

Wakristo leo hii tumesahau ya kwamba Mungu huweza kupata utukufu kupitia magonjwa,
Hali hii inadhihilika wazi kabisa pale wagonjwa mahospitalini wanapoongezeka hali yupo Mungu aponyaye.

Haleluya...
Jina la Bwana liinuliwe...

Jambo moja ninalolifahamu,ni kwamba;
Hakuna mwanadamu awezaye kuponya kwa kutumia akili zake,hata kama awe ni mchungaji wa namna gani,
Yeye aponyaye ni mmoja tu,ni Mungu kwa Jina la Yesu Kristo.Hivyo ukiwa ni mtu uliye ndani ya Kristo Yesu,si wewe uponyaye Bali ni Yesu aponyaye aliye ndani yako.

Watu wengi wasomapo habari ya Lazaro hufikiri ya kwamba ilikuwa ni habari rahisi,yaani namna ya tukio hili lilivyokuwa.
Unajua yakwamba;
Yesu alikuwa Uyahudi,alafu akatoka huko Yeye na wanafunzi wake,alipokuwa mbali na Uyahudi ndipo akapelekewa taharifa ya kuumwa kwa Lazaro ,
Swali langu kwako;

*Kwa nini asing'epewa taharifa hizo alipokuwa huko Uyahudi?
Au
Je Lazaro alikuwa haumwi pindi Bwana Yesu alipokuwa Uyahudi?

Haleluya...

Hayo ni maswali muhimu sana kwa habari hii ya Lazaro Jibu;
Mungu aliruhusu hali hiyo itokee hivyo ili jina lake likapate UTUKUFU huko Uyahudi,na kila sehemu,
Maana tunasoma;
"Basi aliposikia ya kwamba hawezi,alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo." Yoh.11:6

Umeona hapo namna ya mpango wa Mungu,ili utimie.
Biblia inasema Yesu aliposikia ya kwamba Lazaro hawezi hakumuendea muda ule ule Bali alika bado siku mbili pale pale.

Ooh...Ninaipenda habari hii ya Lazaro,inanifundisha jambo kubwa sana katika utumishi wangu kwa Mungu,
Ya kwamba ;nipatapo taharifa yoyote ile iwe nzuri au mbaya,
Basi sitakiwi nichukue maamuzi yoyote yale kwa kutumia akili zangu mwenyewe,
Bali yanipasa kutulia sehemu ile ile nilipokuwa mpaka Roho mtakatifu aamue ndani yangu na Kunipa direction/muelekeo wa nini kifanyike.

Biblia inatuambia Yesu aliposikia yakwamba Lazaro hawezi hakuamua kuzifuata akili zake binafsi Bali alikaa kwanza mahali pale pale akisubiri Roho mtakatifu aingie kazini.

Mara nyingi tunakosea sana kwa kuongozwa na akili zetu kwa kumuacha Roho mtakatifu atuongoze.Utakuta Mtumishi anapelekewa taharifa ya mgonjwa fulani,gafla utakuta anafunga safari kumuendea kwa maombi pasipo hata kuuliza kwa Roho mtakatifu Yeye mwenye kukusaidia juu ya ufumbuzi na uponyaji wa huyo mgonjwa.

Haleluya...

Sasa sikia hii;
*Kuumwa kwa Lazaro kulikamata moyo wa Bwana Yesu.
Unajua ni kwa nini?

Kwa sababu hii,tunasoma;
"Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema,Bwana,yeye UMPENDAYE hawezi." Yoh.11:3

Taharifa hizi za ugonjwa wa Lazaro zilimgusa Bwana Yesu kwa sababu Lazaro alipendwa na Bwana Yesu,kumbe....
Tunahitajika kupendwa na Bwana Yesu,kiasi kwamba tupatapo shida,msiba,magonjwa..N.K
Bwana Yesu atutetee.

Yaani pale inatokea wewe upo katika hatari ya kufa,Bwana Yesu apewe taharifa na mmoja kwamba
"...yule umpendaye hawezi..."
Naye Bwana Yesu akitazama hiyo taharifa aone ukweli wa taharifa hiyo kwamba yupo mmoja nimpendaye ambaye ndio wewe.

*Mungu atusaidie siku ya leo,tuwe miongoni mwa yule ambaye Bwana ampendaye.
Ikiwa upo ugonjwa kwako,nami ninakumbia;
Ugonjwa huo sio wa mauti,bali ni kwa ajili utukufu wa Mungu ili mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.

ITAENDELEA...

*Kwa huduma ya maombezi;
0655-111149.

UBARIKIWE.

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments