TUNAJIFUNZA NINI KWA HABARI YA LAZARO ALIYEFUFULIWA NA BWANA YESU*sehemu ya tano.*

Na Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu apewe sifa....
Haleluya....
Nakusalimu katika jina la Bwana...

Najua yapo mengi tumejifunza kwa habari ya Lazaro wa Bethania,ambaye alifufuliwa na Bwana Yesu.
Hakuna muujiza mkubwa katika Biblia kama huo wa mtu kufa,kisha kukaa siku nne ndani ya kaburi,kisha kufufuliwa.
Najua kuwa ipo miujiza mingi iliyotendeka na kuandikwa katika Biblia.Lakini huu wa Lazaro ni mkubwa sana,maana waweza kufikiria kwamba maiti ya siku nne hunuka,na inakuwa imeshaharibika kabisa,lakini pata picha ya kufufuliwa kwa Lazaro hapo utaelewa kwamba kwa nini ninakuambia ni muujiza mkubwa.

Hukiwa ni msomaji wa Biblia wa kawaida tu,utaona fundisho litokalo kwa habari ya Lazaro ni hadithi tu,au ni jambo la kawaida tu. Lakini Mimi ninakuambia hivi;
Habari ya Lazaro inatufundisha sana,na sio muujiza au jambo la kawaida

Leo tunasoma;
"Yesu akamwambia,Mimi ndimi huo ufufuo,na uzima yeye aniaminiye Mimi,ajapokufa,atakuwa anaishi.Naye kila aishie na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je Unayasadiki hayo?" Yoh.11:25-26

Maneno hayo Bwana Yesu alikuwa akimwambia Martha,lakini Martha wa leo anayeambiwa maneno haya ni mimi na wewe. Bwana Yesu anajitambulisha kwetu rasmi ya kwamba Yeye ndio UFUFUO na UZIMA.

Kumbe mtu yeyote yule aliyekuwa amempata Bwana Yesu anakuwa amepata UFUFUO na UZIMA.
Hii ikiwa na maana kuwa yeye aliye ndani ya Bwana Yesu huwa ndani ya ufufuo na pia huwa ndani ya uzima.

Tabia mojawapo ya mwanadamu ni kuchukia kifo. Hakuna mtu apendaye kufa ingawa ipo siku yamkini atakufa. Sasa leo,Bwana Yesu anatambulisha UZIMA udumuo milele.
Kile ambacho tunaambiwa siku ya leo ni kwamba ;
Mtu awaye wote amuaminiye Yesu,ajapokufa atakuwa anaishi.
Swali langu kwako ;
Anawezaje kuishi yeye aliyekufa?

Ndiposa nikijiuliza swali hilo,gafla najikuta nimtafute zaidi Bwana Mungu anipe mafunuo zaidi. Ndiposa Bwana hunipeleka katika andiko hili;
"Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini;kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake,na kwa hiyo,ijapokuwa AMEKUFA,ANGALI AKINENA." Waebrania 11:4.

Kumbe sasa,yeye aliye ndani ya Kristo ajapojufa kimwili huishi tena kiroho. Hivyo basi kupo kufa kimwili,ambako mwanadamu atauacha mwili wake,Lakini mwanadamu huyo huyo aliye ndani ya Kristo kamwe hatakufa katika mauti ya pili,
(Ufunuo 21:8) maana ipo mauti ya pili.
Upo uzima ndani ya Yesu Kristo,nasema hivi;
Upo uzima ndani ya mmoja tu,Yesu Kristo.

Kipindi ambacho Adamu na Hawa walipokula mti wa ujuzi wa mema na mabaya,walifukuzwa bustanini (Mwanzo3:24).Adamu, Alifukuzwa ili asije akanyoosha mkono wake akala matunda ya mti wa uzima,hivyo Adamu akatoka bustanini akiwa mfu kiroho,ule uzima aliokuwa nao hapo awali ulibadilika.

Sasa Angalia,
Yesu amekuja na UZIMA,Akiwakilisha ule mti wa uzima ambao kwa huo Adamu aliukosa. Hapa tunafundishwa kwamba mtu yeyote asiyeokoka hana uzima wa milele,hufanana na Adamu,maana kile alichokikosa Adamu naye mtu huyo amekikosa,
Sasa Yesu ameleta uzima kwa wote wamwaminio,hao wamwaminio wajapokufa ,huishi milele.

Haleluya...
Bwana Yesu asifiwee...

Tazama tena,Bwana Yesu anakuuliza, JE UNAYASADIKI HAYO?
Hapo ndipo ipo shida kwa mkristo wa leo. Suala ni kuamini kwanza,maana yeye mwenye kushindwa kuamini hayo kamwe hawezi kuwa na UZIMA.Angalia namna Habili alivyoweka IMANI yake kwa Mungu tu,
Biblia inasema ,kwa imani Habili akamtolea Mungu sadaka zilizonona,ijapokuwa amekufa,angali akinena.
Mtu anenaye ni yule mwenye UZIMA,UHAI. Habili alinena angali amekufa,sababu ya imani iliyo jiungamanisha na Mungu.

Yesu anamwambia Martha umbu lake Lazaro maneno mazito sana. Alichokihitaji Bwana Yesu kutoka kwa Martha ni IMANI.
Alikadhalika, Bwana anachokihitaji kutoka kwako ni IMANI ndani yake.

Lazaro ambaye hatunaye,lakini habari zake tunazo sababu zinatuvusha kiimani.

ITAENDELEA...

Kwa huduma ya maombi na maombezi,usisite kunipigia;
0655-111149.

UBARIKIWE.


Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments