TUNAJIFUNZA NINI KWA HABARI YA LAZARO ALIYEFUFULIWA NA BWANA YESU* sehemu ya mwisho*

Na Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...

Nazungumzia habari ya Lazaro wa Bethania,mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha dada yake. Nalikuambia kwamba yapo mambo mengi sana ya kujifunza,lakini tumejaribu kuchambua yale machache tu,kwa sehemu yake.Kama laiti tutazungumzia kila aina ya mstari kupitia ufufuo wa Lazaro,basi ukweli ni kwamba tusingeweza kumaliza fundisho hili siku ya leo,yamkini fundisho hili lingeisha baada ya miezi mitatu hivi.

Msingi wa fundisho hili umetoka katika kitabu cha Yohana 11:1-44,
Leo tunasoma hapa;

"Yesu akasema,liondoeni jiwe.Martha,dada yake yule aliyefariki,akamwambia,Bwana,ananuka sasa;maana amekuwa maiti siku nne. Yesu akamwambia;
Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?" Yoh.11:39-40.

Tazama imani ya Martha dada yake Lazaro,ilivyokuwa akiyumba yumba,kwa sababu Martha huyu huyu ndiye aliyemuambia Bwana Yesu kwamba anasadiki ya kuwa Yesu ndio Kristo ,Mwana wa Mungu,yule ajaye ulimwenguni,naye ndio huo ufufuo na uzima(Yon.11:27).

Lakini sasa anatia shaka. Biblia inatuambia mtu akisita sita katika imani aweza asipokee kile akiombacho.
Wakristo wa leo tunashindwa kupokea kwa sababu ya KUSITA-SITA kwetu katika njia mbili,ingawa tunaye Yesu kama vile Martha mtu aliyekuwa na Yesu pembeni yake lakini alikuwa na mashaka katika imani yake.

Sasa angalia tena;
Zaidi ya hayo Biblia inatuambia Lazaro alikuwa kaburini yapata siku nne,hivyo wakina Martha wakamwambia Bwana kwamba Lazaro ANANUKA.
Bwana Yesu alikuwa akijua hali ya Lazaro ya KUNUKA,hivyo ilikuwa haitajiki tena apewe taharifa kama hiyo.
Ukweli alikuwa ananuka maana alikuwa maiti muda wa siku nne kaburi,lakini je swali;
Wanapomuambia Bwana kwamba Lazaro ananuka walikuwa wanamaanisha,asifufuliwe?
Au walikuwa wakimaanisha Lazaro asitolewe kaburini?
Sijui kama ulishawahi kujiuliza hivyo.

Haleluya...

Watu waliosema hivyo ni watu walio na Yesu,walikuwa sio watu wa mbali bali ni watu wa karibu. Kama vile leo tulivyokuwa ni watu wa nyumani mwa Mungu,lakini tunawatolea maneno mabaya ndugu zetu,na kuwaambia kwamba wananuka.
Ooh,Bwana utuhurumie...

Nasema hivi;
Watu wa leo ndivyo wasemavyo,ya kwamba "fulani ananuka" wakimaanisha kwamba,fulani hafai kufanyiwa muujiza wowote ule maana -ni ananuka.
Mtu anayenuka ni yule ambaye ameshaharibika,labda ameoza. Uthamani wa mtu huyo hupotea,tena pale uwambiwapo "Fulani ananuka"maana yeke huachane naye. Ndivyo wale ndugu walivyokuwa wakisema mbele ya Bwana Yesu.

Sasa Martha anamuambia Yesu kwamba Lazaro ananuka,ni sawa kama vile anamuambia Bwana Yesu amuache Lazaro pale pale kaburini maana wakimtoa nje ni ananuka.
Ooh...
Nampenda Yesu wa Nazareti ajibuvyo,anamumbia Martha " Mimi sikukumbia ya kwamba UKIAMINI utauona utukufu wa Mungu?.Yoh.11:40.

Kumbe wao walichotakiwa ni kuamini tu,basi. Wala sio suala la kusema "ananuka"
Maneno hayo ambayo Bwana Yesu anamuambia Martha,ndio maneno hayo hayo anayokuambia wewe usomaye ujumbe huu,
Kwamba;
Ukiamini utauona utukufu wa Mungu kwa yale yote yaliyokufa.

Yamkini yapo mambo mengi yaliyokufa kwako,na watu wameshasema "yananuka"
Yamkini biashara yako imekufa na kuzikwa hata watu husema" inanuka,"
Yamkini tumbo lako la uzazi halizai,limekufa na kuzikwa,hata watu wamesema " linanuka,"
Yamkini u mfu katika kila eneo,yaani chochote kile ugusacho hakifanikiwi, "kinanuka"

Lakini leo Bwana Yesu akuambia hayo yote yaliyokufa uyatoe kaburini na umpelekee Yeye,haijarishi wamesema kwamba "yananuka"lakini Bwana atayahuisha,nayo yatafufuka kwa upya,lakini kwanza uamini kwamba Bwana anaweza kufufua.

Haleluya...

Pale Bwana Yesu alipoambiwa ananuka,ndipo pale alipowaambia WALIONDOE JIWE LA KABURI yale mambo yaliyoshindikana kabisa kwa akili zetu za kibinadamu ndio hayo Mungu huanzia.Martha na watu wote hawakuwa na jibu lolote,zaidi ya kusema "ananuka" bali Bwana alikuwa na jibu.

Ili muujiza ule wa kufufuliwa kwa Lazaro utimie,Bwana alihitaji Martha awe na IMANI iliyo kuu. Ndiposa nami nikajifunza kwamba imani ndio daraja la muujiza.

Wapo watu ambao,kiukweli kabisa wamekufa hali wakitembea. Roho zao hazina uzima,watu wa namna hii,tusiwaite " wananuka" Maana Bwana yupo aweza kuwarejesha upya kwa kuwazaa tena,sababu Bwana huzaa mpaka Sasa kwa msaada wa Roho mtakatifu.

Ikiwa Yesu Kristo wa Nazareti alimfufua Lazaro mtu aliyekuwa maiti wa siku nne kaburini,basi Yesu Kristo yule yule aweza kufufua roho yako iliyo mfu,kwa kukuzaa Mara ya pili yaani kuokoka,tena siku ya leo Bwana aweza kuifufua biashara yako iliyokufa. Suala ni kuamini tu,na inawezekana.

Kwa huduma ya maombezi waweza kupiga namba yangu;
0655-111149.

MWISHO.

UBARIKIWE.

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments