TUNAJIFUNZA NINI KWA HABARI YA LAZARO ALIYEFUFULIWA NA BWANA YESU*sehemu ya tatu*


Na Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
Nasema,
Haleluya...

Yapo mambo mengi sana ya kujifunza kupitia habari ya Lazaro yule aliyefufuliwa na Bwana Yesu.Tumejifunza mengi katika fundisho hili,lakini leo pia tunaenda kujifunza zaidi.
Kumbuka kwamba andiko letu la fundisho hili linatoka kutoka kitabu cha Yoh.11:1-44.Na siku ya leo
Tunasoma;
"Basi Tomaso,aitwaye Pacha,akawaambia wanafunzi wenziwe,Twendeni na sisi,ili tufe pamoja naye."Yoh.11:16.

Anachokisema Tomaso kwa wanafunzi wenzake ni kitu kikubwa sana. Kama ukisoma haraka haraka unaweza kuona kwamba ni jambo dogo,
Sikia asemavyo;
"...Twendeni na sisi,ili tufe pamoja naye."

Pendo lililopo kwa Tomaso lilikamata moyo wake,kiasi kwamba aliona ni bora wote waende kufa pamoja na Lazaro. Kawaida ya mwanadamu ni kuogopa kifo,lakini kawaida hii haikuwa kwa Tomaso aitwaye pacha.

Kanisa la leo limeshindwa kwenda kuwatembelea mgonjwa.Watumishi wa makanisa ya leo huomba na kuhubiri sana madhabahuni,Lakini wengi wameshindwa kuwatembelea wagonjwa,ambao wagonjwa hao ni wapendwa wenzao. Mafundisho na maombi huishia madhabahuni tu.Yaani utakuta mchungaji hana muda wa kwenda kwa mngonjwa ambaye ni mpendwa mwenzake.

Ila Tomaso akasema hapana!
"...Twendeni na sisi tufe pamoja naye."Yoh.11:16
Tomaso analifundisha kanisa la nyakati hizi za mwisho,kwamba kuhubiri na kuomba madhabahuni au ndani ya kanisa tu,HAITOSHI!
Bali inabidi nasi twende tufe pamoja nao.
Biblia haikusema kwamba Bwana Yesu aliwaambia,au aliwahimiza waende kwa Lazaro aliyekuwa hawezi mpaka kufa,Bali tunaona mguso wa ile taharifa uliwataharakisha wakina Tomaso mpaka wakaona kama hali yenyewe ndio hivyo basi ni bora waende wakafe pamoja na Lazaro.

Leo ipo shida,
Wakristo mpaka wafanye maamuzi ya kwenda kwa mgonjwa au kwenye msiba,basi ni lazima Mchungaji atumie nguvu nyingi sana kuhimiza,kusisitiza juu ya hilo.

Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...

Sikia;
Si kana kwamba wanafunzi wa Yesu,pamoja naTomaso walikuwa hawajui mauti ya Lazaro,maana Yesu alikwishawaambia yakwamba Lazaro hajalala Bali amekufa. Lakini ingawa walitambua hivyo,hawakusita kwenda ili wafe pamoja naye.
Hii si hali ya kawaida.
Tazama hapa;
Na baada ya Tomaso aitwaye pacha kuwaambia wanafunzi wenzake kwamba waende wakafe pamoja na Lazaro,hauoni hata mwanafunzi mmoja kati yao akiweka shaka juu ya maneno hayo,
Wala huoni wanafunzi wakijibishana juu ya maneno hayo.

Jambo moja la msingi tunalojifunza siku ya leo ni kwamba,
YATUPASA KWENDA KUFA PAMOJA NAO
Kufa pamoja nao haimaanishi tukafe na sisi,Bali inamaana kuwa; twende tukalete uhai halisi kwa yule aliyekufa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
Wapo watu waliokufa Kiroho na kimwili pia,
Ipo misiba,
Yapo mauti,
Yapo magonjwa,
Yapo mateso,
Lakini neno linasema twenda tukalete uzima juu hayo yote kwa jina la Yesu Kristo.

Tunasoma;
"Basi Yesu alipofika,alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu,kadiri ya maili mbili hivi." Yoh.11:17-18.

Haleluyaaa...
Nakuambia;
Haleluyaaa...
Oooh.. Nampenda Bwana Yesu...

Biblia inatuambia Lazaro amekufa,na tayari wameshamzika yaani yupo kaburini,na ishu si tu kuwepo kaburini Bali ishu ni amezikwa sasa ni siku ya nne,ndipo Bwana Yesu anafika.
Hapa ndipo nikisomaga nabaki mdomo wazi kwa kushangaa matendo makuu ya BWANA MUNGU.

Palikuwa na umbali kutoka Bethania kwenda Yerusalemu kama maili mbili hivi,Lakini umbali huu haukumsumbua Bwana Yesu. Hapa tunafundishwa kwamba kazi ya Bwana Mungu haina umbali,maana kama Yesu ang'eangalia umbali,basi ni dhahili asing'elienda.

Maili mbili sio umbali mdogo,tena umbali huo ni umbali ambao Bwana Yesu aliotembea kwa miguu.
*Mungu atusaidie sana,siku za leo watu huchoka kutembea kwa ajili ya kazi ya Bwana.Yaani kutembea kidogo tu,watu hulalamika!

Ni ombi langu kwako siku ya leo,twende tukapeleke injili kwa watu wote.Mungu akusaidie uweze kusaport injili kwa kujitoa wewe mwenyewe,au kuinjilisha kwa mali zako,
Maana hata maandiko matakatifu yanatuambia tumuheshimu Mungu kwa mali zetu...

ITAENDELEA...

Ikiwa bado hujaokoka,
Ikiwa unahitaji maombezi,
Basi usisite kupiga namba yangu hii;
0655-111149.

*Usikose muendelezo wa fundisho hili mahali hapa,maana leo tumejifunza jambo kubwa sana japo ni kwa ufupi tu.

UBARIKIWE.


 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments