UMUHIMU WA KIJANA KANISANI


1 Yohana 2:14-17-
.....Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 





1. Kujishughulisha na mambo ya Kanisani kwake, kuwaza jinsi kutakavyopendeza.

2. Kujishughulisha na Baba yake wa Kiroho (Mchungaji) 2Tim, 1: 2 – 4.

3. Kuomba juu ya Kanisa / kufundisha / kuwaleta watu kwa Yesu.

d. Kuwa mkarimu Kanisani na nyumbani, Mf, Rebeka,Mariamu, Mwanzo 24: 13 -26.

4. Kujitolea kifedha,Kiakili ,Muda (Mf, Dorkasi, Warumi 12: 1)

  5. Kanisa lenye nguvu ni lile Vijana wao wanajitambua.

  6.  Kanisa lenye matokeo mazuri linatokana na Familia zinazolijenga Kanisa.

  7.  Kijana akikosa mwelekeo anaharibu mwelekeo mzima wa Kanisa.

  8.  Vijana wachache tu wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana Mf, Vijana watatu (3) Shedraki, Meshaki na Abednego (Danieli 3: 16 – 19 mst 28 -30.

  9.  Kijana aliyebadilika moyoni mmoja tu anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana, Mf, Danieli 6: 24 – 28.

  10.  Alionyesha Mungu wake na Mfalme na jamii yote ikamwinamia Mungu wake.

  11.  Biblia inasema mtu asiudharau ujana wako, 1Tim, 4: 12.

  12.  Kijana asipojitambua na kuwajibika atadharauliwa tu kama hakuna kitu umekifanya Kanisani kwako kinachoonekana.

  13.  Una ulichokifanya kwa Baba yako wa Kiroho? (Mchungaji).

  14.  Una ulichokifanya katika jamii ya kwenu?.

  15.  Penda kijana ukiwepo mahali uwepo kwa faida, usiwe hasara bali uwe faida.

  16.  Huwezi kuheshimiwa kama hakuna kitu unachomfaidisha nacho Mungu.

  17.  Kijana Joshua alikabidhiwa jukumu la kuwaingiza watu Kanaani kwani alikuwa Kijana aliyejituma, aliye tayari anayepatikana, (Hesabu, 27: 18, Kutoka, 17: 8 – 10).




MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka, ni vyema sana kuokoka muda huu yaani kumpa BWANA YESU maisha yako na kujitenga kabisa mbali na shetani, kumbuka zamani hizi ni za uovu sana , dunia imeharibika sana, Tunamhitaji BWANA YESU ili tusiende jehanamu maana hakuna njia nyingine ya kwenda uzima wa milele ila ni njia ya YESU KRISTO pekee (Yohana 14:6, Matendo 4:12). kama unahitaji msaada zaidi wa kiroho, kama maombezi, ushauri na kubadilishana mawazo nipigie kwa namba hiyo hapo chini. 
AMEN.

MUNGU awabariki sana

Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula
         
                       0714252292


 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments