|
Madhabahu ambayo imefananishwa na pembe ya ng'ombe. Pembe ilitumuka na wasukuma kuwaita kwenye vikao. |
Najua umewahi kuona makanisa mengi hapa africa ambayo mara zote yamekuwa
yakijifananisha na tamaduni za ulaya kutokana na historia ya kanisa
ilivyo. Makanisa yote yamekuwa yakijengwa kufananishwa na jinsi makanisa
ya KIZUNGU yalivyo na kuitwa majina ya huko yalipoanzia na pia
kuwaonesha Yesu na mitume wake kama wazungu n.k
Sasa, kuna kanisa lipo Bujora Mwanza linaitwa Kanisa la Mt. Cecilia BUJORA Hili ni la kipekee! Lilijengwa na
mzungu lakini kini limejengwa kwa kufuata tamaduni za kisukuma. Kuanzia
jengo na vitu vilivyomo ndani na hata sanamu ndani ni za sura za
kiAfrica pamoja na Yesu mwafrica. Inapendeza sana jinsi ambavyo jamii
hii ya wasukuma ilivyofikiwa na hawa wamishionari. Hebu jionee mwenyewe
hizi picha za kanisa hilo.
|
Hili ndio jengo la kanisa, na hivi ndivyo wasukuma walivyojenga nyumba zao. |
|
ndani. |
|
Viti vya watumishi. Hivi ndio viti vya asili vya wasukuma. Pembeni ni mtungi wa maji kwa ajili ya kubatizia. |
|
Kinanda cha kwaya. |
|
Kaka Godlove ndani ya kanisa. |
Unaweza ukatembelea kanisa hili ambalo lipo Bujora Sukuma Museum, Magu mkoani Mwanza.
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12
Comments