UREJESHO WA KANISA LA KRISTO

na Sam Balele

Urejesho wa Kanisa uko njiani,na jeshi kubwa kwa ajili ya kazi hii ya urejesho limeanza kuandaliwa na mwenye Kanisa. Mafundisho na mapokeo yanayohangaisha Mwili wa Kristo na kuligawa Kanisa la Kristo yote yanaenda kupokonywa nguvu. Mafundisho yaliyo ya Kweli ya Mungu kama alivyokusudia Yeye mwenyewe yanaenda kufahamika na kueleweka kwa wale aliowakusudia ili wasiukose uzima wa milele, kwa maana Mungu alikwishatangulia kuwachagua kabla misingi ya ulimwengu haijawekwa, sasa si unajua kuna wale waliokusudiwa na Mungu na ile hesabu ikitimia ndipo Unyakuo utatokea. Wale watakatifu waliotangulia Bwana Mungu ameshawaambia wawe na subira ili hesabu ya ndugu zao walio hai itimie. Mimi ndomana huwa najiepusha sana na ligi za mapokeo katika madhehebu, kile anachonishuhudia Roho Mtakatifu ndo huwa naaandika na kuwashirikisha wenzangu humu, mtu akishikamana nacho ni faida kwake, yeye atakayeona ni upuuzi na aone upuuzi lakini mimi nakuwa nimetimiza kilichowekwa moyoni mwangu na Mwenye Kanisa.
Nataka kutangaza kuwa Kanisa linaenda kurejeshwa katika MSINGI wake ambao umejengwa juu ya Mitume na Manabii (Waefeso 2:20-22). Hakuna atakayeweza kulizuia hili. Huu mvurugano uliopo sasa ambao unawafungia watu mlango wa kuingia katika Ufalme wa Mungu, unaenda kuisha na Kanisa litakuwa kimbilio la wengi kama alivyokusudia Mungu. Siku za kuona watu 3,000 na watu 4,000 wakiamua kuliamini neno la Injli ya Wokovu na kuokoka zinakuja (Matendo ya Mitume 2:41, 4:4, 5:14). Kanisa linaenda kuwa na umoja kwa wale walio na chapa ya Yesu Kristo, maana ni ukweli usiopingika kuwa watu wengine ndani ya Kanisa ni magugu yaliyopandwa na Adui, na hili alilisema Bwana mwenyewe, kwakuwa walinzi walilala wakati fulani na hili likatokea na ndiyo hayo magugu yaliyopandwa yanalisumbua Kanisa leo. Ila siku zafanya haraka kuja, kila kitu kitawekwa juu ya dari kwa watu wote kuweza kuona, kusikia na kufanya uamuzi sahihi baada ya kuelezwa habari kwa usahihi zaidi.
Roho Mtakatifu yuko kazini hata sasa, akitengeneza watumishi walio mashahidi pia, watakaotenda kazi pamoja nae, Bwana akilithibitisha neno lao kwa nguvu na uweza na udhihirisho mwingi, akiachilia hekima ya Mungu ndani ya askari hawa wa Bwana Yesu. (Marko 15:20, Waebrania 2:4)

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments