![]() |
Mch Dr Philemoni Tibanenason |
Mch
Dr Philemoni Tibanenason ni Mwangalizi mkuu wa Kanisa la Pentekoste
Tanzania(KLPT),na kwa sasa ni mchungaji wa kanisa la KLPT lililoko Mnazi
mmoja jijini Dar es salaam.Hapa Mch Dr Philemoni Tibanenason anaeleza
namna alivyotoka Bukoba hadi kufika jijini Dar es salaam.
“Katika
Miaka ya Sabini Nilikaa Bukoba nikifanya Huduma kwa miaka
miwili,Bukoba(Kagera) ndio mkoa nilioanzia huduma, katika kipindi hicho
nilikuwa na miaka 26,na mke wangu alikuwa na miaka 20.Siku moja nikiwa
nimelala yalikuja maono yakinitaka niondoke Bukoba niende eneo lingine
ambalo ni mbali sana na Bukoba yaani Dar es salaam.Nilipoyaona hayo
niliwaambia watu waliokuwa karibu nami ikiwa ni pamoja na waumini kwamba
Imenipasa kwenda kule Mungu alikotaka niende”
Sikulijua
hilo kama lingepokelewa kwa hisia tofauti na waumini niliokuwa nao
kipindi hicho,hasa ikizingatiwa walikuwa wakinipenda kwa namna ambayo
sikuwa najua kwa sababu gani.Nilijua huenda wangefurahia na kunipa
mkono wa kwa heri , lakini walisema wasingependa kunipoteza kwamba
niende mbali na wao.Ilinilazimu kuwa na subira kukaa na kumwachia Bwana
ili yeye kwa uwezo wake afanye mwenyewe, lakini nikizidi kumsihi Mungu
kwamba mapenzi ya Mungu yatimizwe na si kama nitakavyo mimi bali kama
atakavyo yeye.
Jambo
la kushangaza baada ya kupita muda fulani mke wangu alienda kwenye
maombi na huko kulikuwa na watumishi wengine. Alipofika huko hakukuwa
na mtu aliyekuwa akijua maono yangu ambayo Bwana alisema na mimi ya
kwamba nihame Bukoma na kuelekea Dar es salaam. Na kipindi hicho
washirika wangu walikuwa hawataki nihame.
![]() |
Dar es salaam Ilivyo sasa
|
Baada
ya Swali hilo mke wangu alikuwa kimya kisha na baada ya kumaliza maombi
alirudi nyumbani na kunishirikisha.Aliponiambia habari hizo nikasema
kwa kweli kwa namna yeyote ile, iwe kwa Miguu,au gari ni lazima nianze
safari mara moja ya kwenda Dar es salaam.Washirika niliokuwa nao wao
waliendelea kushikilia msimamo wao kuwa kuwa hawataki niondoke.Kwa
mazingira hayo hawakuwa tayari kunipa nauli walikazania niendelee
kuhubiri eneo hilo.
Nilikaa
chini na kujiambia ikiwa nitawasikiliza wao nitakuwa simsikilizi Mungu
aliye hai,niliangalia namna nitavyoweza kupata pesa za nauli za kunitoa
Bukoba hadi Dar es salaam, lakini sikuweza kuiona.Hivyo nikashauriana
na mke wangu kuwa tuuze kitanda ili tuanze safari mara moja, kwa Neema
ya Mungu nilifanikiwa kupata shilingi 100,kwa kipindi hicho pesa hiyo
ilikuwa ni kubwa kiasi kwamba hadi kufika Dar es salaam ilitughalimu
kiasi cha shilingi 45/= tu.
Tulipofika
Dar es salaam na mke wangu tuliwakuta wamishionari tuliofanya nao kazi
na wakati wanaondoka walituachia waumini 10, nakumbuka kipindi hicho
hakukuwa na wahubiri wengi kama kipindi hiki.Kipindi hicho Askofu Moses
Kulola,Masalu,Emmanuel Lazaro sambamba na Titus Mkama ndio waliokuwa
wakijitoa mhanga kuihubiri injili jijini Dar es salaam.Kipindi hicho
Jiji la Dar es salaam lilikuwa limefunikwa na Uislamu na wakati Mwingine
ilikuwa ni hatari kutembea huku ukiwa umeshika Biblia.
Katika
Miaka hiyo ya Sabini makanisa ya wokovu jijini Dar es salaam yalikuwa
Temeke na Ilala na tulikuwa tukifaanya kazi ya Mungu kwa Nguvu,Upendo na
Ushirikiano mkubwa.Tulifanya kazi hiyo kwa muda mrefu ilipofikia Miaka
ya Themanini ndipo Mikutano ya Injili ilianza.
Comments