WAHUDUMU WA AGANO JIPYA KATIKA ZAMA HIZI.



2 Wakorintho 3:5,6
"Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa Agano Jipya, si wa andiko bali wa roho, kwa maana andiko huua bali roho huhuisha.

Neno lolote lisemwalo na yeyote anayejiona na kujiaminisha kuwa ni mtumishi wa Mungu ama anamtumikia Mungu, neno hilo si lake na wala halijitoshelezi katika yeye mwenyewe. Hilo neno anenalo ni la Bwana na utoshelevu wake watoka kwa Bwana. God speaks through His servants and He makes everything sufficient, apostle Paul knew this and he wrote it down. Ni Mungu aliyewafanya Musa na manabii kuwa wahudumu wa Agano la Kale na kazi yao waliifanya vizuri Mungu akichukuliana nao katika madhaifu yao, sasa sote tunajua hata nabii Musa alikuwa na udhaifu wake, hata nabii Eliya alijichanganya sehemu fulani na kujiona ni yeye tu ndo yeye, Mungu akamwambia anao watu wengine 7,000 waliokuwa upande wake japo hawakuwa pamoja nae nabii Eliya wakiandamana nae katika huduma yake. Huyu ndiye Mungu sasa.

Na ni Mungu huyu huyu aliyewafanya hawa wenzetu kuwa wahudumu wa agano lile la kale, ndiye huyo huyo pia aliyewafanya wenzetu wa Kanisa la Kwanza kuwa wahudumu wa Agano Jipya. Agano la kwanza likiwa ni la andiko, la mambo ya mwilini na kushikwa kwa jinsi hiyo. Agano la pili likiwa la roho, la mambo ya rohoni na kushikwa kwa jinsi hiyo. Agano la kwanza likiwa ni kivuli cha Agano la pili, amri katika la kwanza ziliandikwa kwa ubao, amri katika la pili Mungu alisema kupitia mhudumu wa agano la kale, nabii Yeremia kuwa zitaandikwa katika moyo (Yeremia 31:31-34), na hapa ndipo inapokuja tafsiri ya Roho Mtakatifu ndani ya mwanadamu, ile sheria ya Roho wa Uzima, yaani kuongozwa na Roho, ambapo nia ya mwanadamu inahifadhiwa na amani ya Mungu (Wafilipi 4:7). Wale wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndo wana wa Mungu, hao wanaotenda kazi na Roho wa Mungu hao ndo wahudumu wa Agana Jipya (Matendo ya Mitume 5:32). Sasa unajua si wote wasemao Bwana Yesu Bwana Yesuni wahudumu wa Agano Jipya, mengine ni magugu na ndiyo yanaleta mkanganyiko kama ilivyokuwa katika Agano la Kale, magugu yalikuwemo, kuna mmoja lilikuwa na ujasiri wa kuvunja nira aliyojivika nabii Yeremia na kutoa unabii mzito. Sasa wewe angalia mafundisho yanayowatoka moyoni mwao kama yamefunga ndoa na Biblia.

Ikiwa yeye aliye mhudumu katika zama hizi za agano jipya hatoi habari ya Agano Jipya, nayo habari yajulikana nayo ni hii katika Warumi 1:16 na Mathayo 28:19,20; hapo lazima uwe na maswali, sasa siyo umshambulie kwa maneno, la hasha bali uwe na maswali na utulie na kupambanua katika Roho na si katika mob psychology ama hadithi za vijiweni na magazeti ya udaku. Mambo ya Mungu yanafumbuliwa na Mungu mwenyewe ndomana anasema zijaribuni roho, na ili uzijaribu roho ni lazima uwe vizuri na Roho Mtakatifu kinyume cha hapo utakuwa unatumia hekima na maarifa ya kibinadamu kupambanua mambo ya jinsi ya roho na ni lazima utakwama tu na kufanya usiyopaswa kufanya kama sasa wanavyofanya wengi kwavile utaweka vipimo vya kibinadamu.

Unahubiri nini katika zama hizi za Agani Jipya? Agano la kale limemzungumzia Bwana Yesu Kristo, ujio wake na kazi yake ya wokovu wa mwanadamu. Agano Jipya limebeba utimilifu na udhihirisho wa yaliyosemwa juu ya Yesu Kristo katika Agano la Kale. Agano Jipya ni juu ya Ufalme wa Mungu hapa duniani, na ufalme wa Mungu ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu (Warumi 14:17). Haki ni kusamehewa na kufutiwa dhambi zote na kukirimiwa utakatifu, amani ni kupatanishwa na Mungu na kukirimiwa uzima, furaha ya Mungu ni nguvu kwa mwanadamu kuweza kuishi maisha ya ushindi ndani ya Yesu Kristo na kuwa mtakatifu ampendazaye Mungu hapa duniani (Zaburi 16:3)

Katika wahudumu wa Agano Jipya waliotangulia na kuwekwa kumbukumbu katika Biblia, hakuna hata mmoja aliyehubiri dhehebu. Kwa mfano,wahudumu Paulo na Barnaba walianza pamoja huduma (Matendo 13:1-3), lakini badae walipart ways baada ya kuvutana juu ya Marko (Matendo 15:36-41), Biblia haisemi kuwa walianza kukashifiana juu ya huduma zao, sasa leo kwanini kunakuwa na kashfa na chuki na matukano ikitokea hali kama hii?. Udhehebu na uhuduma umeota mizizi na kukithiri, UHUDUMU wa Agano Jipya umemezwa na udhehebu/uhuduma na watu wanajitosheleza wenyewe na kujiona bora kuliko wengine. Aliyetoshelezwa na Mwenye Agano Jipya kwa usemi na kwa nguvu na uweza hawezi kufanya vituko vinavyofanyika leo. Sasa yawezekana mhudumu alianza vizuri na BWANA uhudumu wake lakini sasa anafanya kwa utoshelevu wake na hapo lazima kutazalisha shida tu, hii ilimtokea mfalme Sauli, mhudumu katika Agano la kale, alianza na BWANA, katikati akajikwaa, badala ya kurekebisha na BWANA yeye akataka kurekebisha na nabii Samweli, mhudumu mwingine mfalme Daudi alikosea na akawa mwerevu na kurekebisha na BWANA na si nabii Nathan na akaendelea kutumika na BWANA na utoshelevu wake uliendelea kutoka kwa BWANA.

Mhudumu wa Agano Jipya anahudumia Agano Jipya na ujumbe wake sikuzote ni Ujumbe wa Agano Jipya , nao ni INJILI YA AMANI, amani kati Mungu na mwanadamu, na mwanadamu na mwanadamu. Bwana Yesu alimpendeza Mungu na wanadamu, maana yake alikuwa na amani na uhusiano wenye afya na siha njema na Mungu pamoja na wanadamu.(Luka 2:52, Warumi 14:18).


Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments