Wapendwa katika Kristo Yesu Shalom!Nyakati hizi kama maandiko yanavyosema ni za hatari 2Timotheo 3:1.Kweli ni za hatari kwani kasi ya kuwatafuta na kuweka imani kwa wanadamu imesababisha watu kutanga tanga.Wanafikiri Yesu yuko mbali nao bali wako karibu na wanadamu wanaowatukuza na kujenga imani kwao,lakini wanadamu hao wakishindwa wanakata tamaa.Kwa sababu wameweka kwao kuwa watamaliza shida na matatizo yao.Funguka mponyaji na mmaliza shida na matatizo yetu yote tukijenga imani kwake.Yesu yuko karibu sana nasi tukivunjika
mioyo yetu na kupondeka roho zetu.Zaburi 34:18.Mama mmoja aliyekuwa
anaumwa aliweka imani yake kwa Bonke hivyo mtumishi alipokuja akawaambia
watoto wake wampeleke kwani Bonke atamponya,lakini kinyume hakupokea
uponyaji akakasirika na kukata tamaa kuwa kama mtumishi huyo kashindwa
kumponya basi hakuna atakaye mponya.Lakini akili za Mungu hazichunguziki
na hazina mipaka.Kanisani kwake uliandaliwa mkutano na mhubiri
asiyevuma alitumika,watoto wake walikuwa wameokoka wakambebeleza
ahudhurie japo aliendelea kubisha lakini walimwambia si Bonke wala huyo
wa sasa hakuna awezaye kuponya bali Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye
hai.Mama alibadili mwelekeo wa imani na kujenga imani kwa Yesu
alipoombewa tu alipokea uponyaji wake.Tuache kuweka imani kwa wanadamu
bali kwa Bwana Yesu tu Yeremia 17:5.Tuache kutanga tanga tukitafuta
uponyaji kwani uko kwetu wenyewe tukiweka imani kwa Yesu tutamwona na
kupokea uponyaji na kutuondolea shida na matatizo yetu kwani pasipo
imani haiwezekani kumpendeza Mungu Waebrania 11:6.
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments