HAKUNA KOSA LISILO SAMEHEKA CHINI YA JUA.

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Haleluya...

Wapo watu wasemao "Kwa kosa hili,siwezi kukusamehe kabisa"
Wengine husema " nimekusamehe lakini sitakusahau"
Wengine utawasikia wakisema " Nilikusamehe mara moja,lakini kwa hili kosa siwezi kukusamehe kabisa,sababu umerudia tena "
Wengine huwachukulia hatua ya kuwaua wezi,na vibaka,wakisema "hatuwezi kuwaacha hai watu kama hawa vibaka..."

Watu wa namna hiyo siyo watu wa mataifa peke yao wasemayo hayo,bali pia wapo Wakristo wasemao hivyo.
Lakini swali la kujiuliza;
Je ni kweli ndivyo tulivyoagizwa na Kristo?

Sasa tuchungulie kile ambacho Bwana anasema;
"Kisha Petro akamwendea akamwambia,Bwana,ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe?hata mara saba?
Yesu akamwambia,sikuambii hata mara saba,bali hata saba mara sabini." Mathayo 18:21-22

Oooh,
Nampenda Yesu wa Nazareti

Yesu Kristo anajibu swali lililoshindwa kujibiwa na wanadamu. Anasema "samehe hata saba mara sabini"
Ukichukulia hesabu ya kawaida,ni sawa anasema samehe zaidi ya mara 490,
Akiwa na maana kwamba hakuna kikomo cha kusamehe.

Yesu anamwambia Petro kiwango cha kusamehe cha hali ya juu ambacho mwanadamu wa kawaida hawezi kusamehe katika hali hiyo pasipo kusaidiwa na Roho mtakatifu.

Ngoja nikupe mfano huu,alafu jipime kama ungelikuwa wewe,Je ungeweza kusamehe;
Sikia hii,

Mtu mmoja alikuwa na mke. Mkewe alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mchina,naye alikuwa akifanya kazi sehemu nyingine.
Ikatokea mke wake akawa anatoka nje ya ndoa,naye huyo mume akaambiwa juu ya mke wake. Akiwa anamuuliza yule mke wake,mke wake akawa anakataa kabisa.
Basi maisha yakaendelea hivyo hivyo katika hali ya kuwindana,(yaani mume alikuwa akimtegea mkewe amfumanie,naye mke wake akaanza kumpeleleza kwa siri)

Sasa siku moja yule mama akawa mjamzito. Mume akawa ana muhudumia kama kawaida,akijua ni mimba yake.
Sasa kasheshe ilipojifungua!
Nakuambia yule mama akajifungua mtoto wa kichina.
Kha!
Mwe!

Mambo yakaumbuka,
Kumbe mkewe alikuwa akitembea na boss wake mchina.
Mume kuja kumuona mtoto hospitalini,kumbe ni mtoto wa kichina!"

Haleluya...

Sasa chukulia wewe ndio huyo mume,JE UNGEWEZA KUMSAMEHE MKEO,NAKUENDELA NA MAISHA KAMA HAPO AWALI?

Sasa leo tunaambiwa tusamehe wale wote waliotukosea pasipo manunguniko yoyote yale,.
Ukweli ni kwamba,
Yapo mazingira mengi magumu ambayo kwa hali ya kawaida huyawezi,Bali ni kwa msaada wa Roho mtakatifu baada ya kuokoka.

Nami nasema;
Hakuna kosa lisilosameheka chini ya jua hili.

Yesu ametuambia tusamehe zaidi ya hesabu isiyoweza kuhesabika.
Sijui kama unanipata vizuri hapa;
Kosa lolote lile linasameheka hata kama liweje.

Msihi Bwana awake neema hiyo ya MSAMAHA ndani yako. Neema hiyo ikikaa ndani yako,basi kila kosa kwako halitakuwa kosa.

UBARIKIWE.

 

 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments