HARUSI YA KANA (Wedding in cana of Galilee)*sehemu ya mwisho*

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
ipo NEEMA ya pekee tena siku ya leo kwako,ikiwa ni siku ya mwisho ya fundisho hili zuri.
*Kumbuka msingi wa fundisho hili hunatoka katika kitabu cha Yohana 2:1-11.

Na leo tunamalizia katika mstari huu hapa chini,tunasoma;
“ Akawaambia,
Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,” Yoh.2:8-9

Bwana Yesu anawaambia wanafunzi wake wateke na kumpelekea mkuu wa meza,kile walichokiteka haikuwa divai bali yalikuwa maji ndiyo waliyateka.
Maji ndiyo yalionekana yakitekwa na kupelekwa kwa mkuu wa meza na wala sio divai.
Yamkini wanafunzi wake Bwana walitegemea kwamba wataambiwa wampelekee mkuu wa meza divai iliyokuwa tayari,lakini badala yake wanaambiwa wampelekee maji.

Jambo hili ni jambo la kiimani tena linashangaza kweli kweli.Kwa lugha nyingine ni kwamba;
Bwana Yesu alikuwa anawafundisha somo la IMANI,maana imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana (Webrania 11 :1).
Kwa kutumia macho ya damu na nyama,wanafunzi waliyaona ni maji,lakini katika muonekano wa kiroho hayakuwa maji.
Hivyo wanafunzi hawakuiona divai kipindi kile walipoambiwa wateke maji ndani ya yale mabalasi kisha wampelekee mkuu wa meza,lakini Yesu alikuwa na hakika na jambo litarajiwalo,na ni bayana na jambo lisiloonekana kwa macho ya damu na nyama.

Sasa angalia;
Ingawa wanafunzi hawakuiona divai hapo awali pale walipoambiwa wayateke maji na kumpelekea mkuu wa meza lakini waliendelea kuwa watiifu nao wakayachota yale maji na kuanza safari ya kumpelekea mkuu wa meza.
*Yesu hakuyatazama yale maji kama maji bali aliyaona yamepata kuwa divai tayari.Na hiyo ndio IMANI iliyokamilika

Haleluya….

Ndiposa nikalinganisha hilo agizo la Yesu kwa wanafunzi wake na lile agizo alilowaambia wale wokoma kumi,
tunasoma;

“ Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu,
alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.
Na alipoingia katika kijiji kimoja,
alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
wakapaza sauti wakisema,
Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.”Luka 17:11-14

Je unafikiri pale wakoma walipoambiwa waende kujionesha kwa makuhani walikuwa tayari wametakasika?

JIBU ;
Hapana,wakoma kumi walipoambiwa waende kujionesha kwa makuhani bado walikuwa na ukoma wao ule ule. Lakini walipoisikia ile sauti ya Bwana,wao wakaliamini lile neno,
nao wakaanza safari wakiwa ndani yao wamelihifadhi neno la UPONYAJI,tena wakiwa wameshafungua mioyo yao.
Wakoma hawa walikuwa na IMANI ya uponyaji baada ya kulisikia neno la Bwana Yesu.

Maana ipo imani ya uponyaji ndani ya mwamini,tunasoma hata kwa habari ya Paulo alipokuwa akihubiri huko Listra,
gafla akamuona mtu mmoja ambaye alikuwa hajawai kwenda kwa miguu yake kabisa,Biblia inasema alipomtazama akamuona kwamba ana imani ya KUPONYWA;

“ Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa.
Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana IMANI YA KUPONYWA , ( faith to be healed,)
akasema kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda. ”Matendo 14:8-10

Paulo hakuhitaji kumuombea huyu mtu,bali alichokifanya ni kuhubiri neno la Kristo lenye uhai na uponyaji tele ndani yake,kisha lile neno lilipopata nafasi ndani ya huyu ndugu,ndipo Paulo anamwambia sasa ,
“ Simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda. ” Matendo 14:10

Haleluya…
Nami nikatia ufahamu nilipoisoma habari ya harusi hii ya Kana ,
nikagundua ;
siri ya muujiza wangu,
Siri ya mafanikio yangu,
Siri ya kumuona Mungu katika maisha yangu ya utumishi,
Siri hiyo ni kulisikia na kulitunza neno la Bwana.
Ndiposa milango iliyofungwa itafunguka yenyewe.

Haleluya,..
Groly to God,groly God….
Jamani Hakuna kama Yesu,
Nampenda Yesu wangu….

Biblia inasema yule mkuu wa meza alipoionja ile divai ,akashangaa maana tangu azaliwe hakuwahi kunywa divai nzuri namna ile.Mkuu wa meza akavumilia wee! mpaka akashindwa akaona hata!
Ngoja amuite bwana harusi na kumuuliza;

“ akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.” Yoh.2:10

Kwa lugha nyingine,huyu mkuu wa meza amechanganyikiwa baada ya kuionja divai aliyopewa na wanafunzi wa Yesu,
maana aliona divai ile iko tofauti kabisa na ile aliyokuwa akinywa hapo awali,aliona raha kweli kweli na bubujiko la ndani pale alipoionja divai mpya.

Nami ndiposa nikajifunza ;
Kwamba ndani ya Yesu kuna raha,na bubujiko la kweli,kuna maisha ya utele na wala hakuna kutindikiwa kamwe.

Mpendwa nakusihi kwa neema ya Kristo usichelewe wala usijicheleweshe kumpa Yesu maisha yako,
Sababu hakuna mwingine popote pale wala chini ya jua hili kama Yesu.Sasa fanya maamuzi ya KUOKOKA siku ya leo na utaona hiki nikuambiacho.
Usisite kunipigia,
wakati wa kuokoka ndio sasa

Piga namba yangu hii
• 0655-111149.

UBARIKIWE.

MWISHO.


 


 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments