JIFUNZE YA KUSAMEHE NA KUSAHAU

Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya,
Utangulizi:                                

Yeremia 1:4  Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.  Tangu tumboni Mwa mama mzazi  ndipo tunapoanzia kujifunza Mambo mbali mbali,kwa kuhisi hali ya mazingira tunayotarajia kuja kuishi,

 Tunapofika ulimwenguni tunaendelea kujifunza kwakuhisi,kuona,kusikia, kila kitu, kutofautisha ni pale utapopata Neema ya Mungu kwakuwa tunaishi katika falme mbili, unapokuwa bado tumboni unaishi katika falme tatu, Mungu,mzazi,shetani japo falme kuu bado inabaki kuwa ya Mungu

Falme kuu mbili  zinazofanya kazi hapa Duniani,

Ø  Ufalme wa Mungu- (Nuru)

Ø  Ufalme wa Muovu-(Giza)

Ni vizuri ukafahamu hilo kwanza kabla ya mengineyo Mengi ,Ufalme wa Mungu Unasimamiwa na Mungu Mwenyewe Katika Utatu Mtakatifu Mungu Baba,Mwana,na Roho Mtakatifu, katika mambo yote matakatifu,

Ufalme wa Muovu (Shetani)nao unasimamiwa na Shetani mwenyewe na majeshi yake,Katika mambo maovu yote,

Falme hizi zote zina fanya kazi katika Ulimwengu wa ki-Roho na kujidhihirisha katika Ulimwengu unaoonekana kwa Macho ya Damu na nyama, kwa sababu Maalumu, na Hizi falume zinashindana kila wakati,

 Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

Mema yote au Mabaya yote  yanafanyika kupitia Falme hizi nilizozitaja hapo juu, Mwanadamu asipotumika katika Mema basi atatumika katika Mabaya,asipomtumikia Mungu atatumikishwa na Shetani, usiposababisha makwazo utasababishiwa,

 

 

Katika maisha tunayoishi Hapa Duniani kwakuwa tu wapitaji basi na makwazo hayana budi kutokea  ila tunajifunza, kama vile ambavyo mtu Mwema anavyoweza kujifunza ubaya akawa Mtu muovu ndivyo ambavyo mtu mubaya anavyoweza kujifunza wema na akawa mtu mwema inategemea unajifunza kwa nani, kwa Mungu au kwa Shetani

Mwenye sifa ya kusamehe dhambi Maandiko yameweka wazi ni Yesu kristo peke yake hivyo ni Vema tukajifunza kwake, 

Mathayo 11:29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Ø  Utu wema

Ø  Upole

Ø  Unyenyekevu wa Moyo

Ø  Kupata raha  nasfsini tunajifunza kwa Yesu kristo,

Ø  Mungu anataka ujifunze leo itakusaidika ikiwa utakuwa tayari kujifunza,

Ø  utayari wako ni wa muhimu Sana  ruhusu mabadiliko yaanzie kwako,leo

 

Watu wengi sana wanaokosewa  Wanasamehe sana lakini kusahau tukio au kwazo lililosababisha msaha utoke  ni vigumu sana kusahau, Na hili ndilo jambo linalowatesa kila inapoitwa leo,  kutosahau kosa baada ya kusamehe nikuendelea kuutunza Ugonjwa  badala ya kutibu, Hata kanuni ya Mungu anaanza kutusamehe kabla hajatuponya magonywa yetu,

Maandiko matakatifu yanatufundisha nini juu ya msamaha

Zaburi 103:3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
4Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,
5 Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;
6 Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa

Hakuna mtu anayeweza kupokea uponyeji kutoka kwa Mungu kama hajasamehewa kwanza maovu aliyoyatenda , Haijalisi umemkosea nani lakini kwakuwa ni uovu uliomchukiza Mungu unahitaji kusamehewa au kusamehe na kusahau  ili uwezekuponywa,

Madhara ya kimwili yanayosababishwa na kuto kusamehe na kusahau

v  Upweke

v  Sura kupoteza Mvuto

v  Kuto mwamini Mungu,kuto kuhudhuria ibada

v  Kutokutoa kwaajili ya Mungu/

v  kutokutunza familia

v  kutojijali kimwil wewe mwenyewe

v  Hamu ya kula inaweza ikapotea

v  Manung’uniko kila wakati kwa kila jambo unalofanyiwa

v  Kutomwamini mtu yeyote,

v  Unaweza ukasababisha Msongo wa Mawazo na ukajikuta unaongea peke yako

v  Unaweza kukonda sana au kunenepa kupita kawaida,

v  Unaweza kupoteza ujasiri wa kila jambo unalolifanya

v  Unaweza kuwa Mubishi wa kila jambo, na mengineyo mengi,

v  Roho ya Maombi kutokuwepo

Ø  Ukiomba Maombi yako hayatajibiwa,

Ø  Uzee wako hautashibishwa siku wala mema

Ø  Ujana wako hautaufurahia maana hautarejeshwa ,

Ø  Kutokusamehe kunaambatana na Roho ya mauti,

Unahitaji  Mema na usalama jifunze kusamehe na kusahau,

Kwanini Ujifunze kusamehe na kusahau,

Unajifunza kusamehe kwa sababu  ulivyoumbwa asili yako si uovu,wala mabaya bali  asili yako ni mema ,upendo unaotokana na Mungu kwakuwa  Kuzaliana ni amri iliyoagizwa na  Mungu

Hivyo ikiwa asili yetu ni upendo na Furaha ya Mungu mateso chuki Maovu yanatoka wapi ni kwa yule Muovu, kupitia Wazazi,jamii mazingira , sasa katika hayo yametufarakanisha na Mpango mzima wa Mungu, Mungu anataka akusamehe  leo na kukuponya kabla ya maombi jiulize swali hili uko tayari kusamehe,

Maandiko Matakatifu yanatufundisha nini juu ya kusamehe?

Mathayo 6:14-15

Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Kumbe tunasamehewa  na Mungu Makosa yetu  pale tunapokuwa tayari kusamehe waliyotukosea, bila kuzingatia kosa walilolitenda juu yetu, ni Hatari kubwa sana kutosamehe wanaotukosea,

 kuto kusamehe Kunaruhusu Roho ya mauti katika maisha yetu,Biashara,Masomo,uchumba,ndoa,Huduma, na mengineyo mengi, Jifunze leo,kusamehe na kusahau,

Warumi 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

kumbuka Mungu alitusamehe tangu awli kwa dhambi tulizotenda au kutendeshwa mwanzo kwakuwa malipo ya Dhambi tulizokuwa tumefanya tulitakiwa kulipwa kifo,

ila kwa Neema ya Mungu akakubali kulipa deni langu na lako, yeye  ili sisi tuishi, swali la kujiuliza kwanini unaishi, wengine unakuta anaomba kuongezwa miaka mingi umewahi kujiuliza Unaomba Uishi miaka mingapi na ya nini, kwa sababu gani,

Maana kama utaishi Miaka mingi kwa kumtumikia shetani  utakuwa umemchukiza Mungu  sana hivyo utaishi miaaka mingi ya Laana, ila ukimtumikia Mungu utaishi Miaka mingi ya Baraka, chaguwa leo baraka,au laana mbele yako Mimi ninakushahuri samehe leo na usahau kama uliwahi kutendewa hilo kosa,

Pamoja na Mateso yote aibu ya kila namna Bado yesu akasema Baba Uwasamehe kwakuwa Hawajui watendala , Luka 23:34a

Sifa za Mwenye Kusamehe  

Mtu mwenye uwezo wa kusamehe ni yule Mtu aliyekubali Yesu akawa Bwana na Mwokozi wake Yaani (Aliyeokoka) siyo anayejiita ameokoka  maana uwezo wakusamehe tunaupata ndani ya Yesu kristo, kipimo cha kujuwa kuwa huyu mtu ameokolewa au bado ni kuangalia kama anauwezo wa kusamehe,na kusahau

Maandiko Matakatifu yanatuhakikishia uwezo wa kusamehe unatoka kwa Mungu pekee,

Isaya 43:25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako

Unapotubu kwa makosa uliyoyafanya hakikisha wewe umeshawasamehe maana Mungu akisha futa makosa yako hakukumbushii tena vinginevyo tungekumbushiwa tungekimbiana,

Waibrania 8:12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena,Tatizo au kizuwizi kikubwa kinachotuzuwia  Sisi kusikia au kuuona uwepo wa Mungu katika Maisha yetu au katika kanisa la leo Hatujawa tayari kulipa Gharama ya Msamaha

Tunatamka kusamehe ila bado hatujakubali kulipa Gharama ya kusmehe,

Gharama ya kusamehe ni kubwa  Lakini ni lazima ilipwa,

ili kuwa huru kujipima kama umefungwa au lah! Kipimo ni kujichunguza kama huwa unasame na kusahau,

Kusamehe kunahitaji gharama ya kusahau Maana kutosahau kosa ni kidungo kwako na siku zote Mfungwa hana maamuzi yake mwenyewe, hivyo ile dhambi itakutumikisha tu,

 warumi 7;17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.

Kutofuta kosa ndani  ya moyo wako hauwezi kukuacha ukafanya unalotaka kulifanya ni sawa na mtu anayedaiwa anakuwa hana uhuru kwakuwa wakati wote akimuona mdai anakumbuka deni analodaiwa hata kama mdai hajaulizia Deni lake,

Hatari ya kutosamehe na kusahau,

Kutosamehe na kusahau kutakusababishia kulipiza kisasi, mara nyingi watu wanaopenda kulipiza kisasi ni wale watu wasiyoachilia maovu ndani ya miyoyo yao, kuka na kosa moyoni ni sawana kujitegea Bomu ambalo Muda wowote linaweza kulipuka, na usipokuwa Makini ukapata madhara hata wewe Mwenyewe, kuto kusamehe kunaambatana na Roho ya Mauti, narudia tena bali kusamehe kunaambatana na Roho ya uzima,

Kukaa na tatiza moyoni ni kama kujionganishia shoti ya umeme maana kila unapolikumbuka tatizo ulilokosewa unaumia siku zote fahamu hili anayeumia siyo aliyekosa bali ni wewe uliyekosewa kuwa Huru leo kwanzia sasa kwa kuanza kusamehe wote waliyokukosea, na jifunze leo kusahau,usije ukalipiza kisasi,

Mambo ya walawi 19:18 Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana.

Kuwa na kinyongo ni kukaa na Tatizo ndani ya moyo wako ambalo hutaki kuliachia juu ya mwenzako,

Kabila ya kufanya ibada ya Maombi hatua ya kwanza ni kusamehe na kusahau

Marko 11:25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.

Kitu kinachofanya watu waendelee kuteseka katika hali wanazopitia nikutofahamu kinachowaumiza ni yale matatizo waliyoyashikilia ndani yao, japo katika nyumba za ibada wanaenda  sadaka wanatoa kuimba wanaimba kusali wanasali ila wanasali kwa bidii wakati hawajawa tayari kusamehe na kusahau,

Sasa wanapotoka katika ibada tatizo linabaki pale pale,

Madhara ya ki-Roho Ya  kuto samehe na kusahau,

Ø  Kuto samehe ni kujifunga wewe mwenyewe kifungo asichoweza mtu mwingine kukufunguwa na kisichojulikana mwisho

Ø  Kuto kusamehe kuna kunyima msamaha wa Mungu

Ø  Kutokusamehe kunakucheleweshea baraka zako,

Ø  Kuto kusamehe kunakuongezea kukosea zaidi

Ø  Kuto kusamehe kunatesa nafsi sana

Ø  Kuto kusamehe kuna kutenga na Mungu

Ø  Kuto kusamehe kuna kutenga na jamii ya Mungu

Ø  Kunaweza kukukosesha Mbingu

Ø  Kuto kusamehe kunaweza kukubadilishia hatima yako bila kutarajia

Ø  Kuto kusamehe kunakunyima uwezo wa kukuwa ki-Roho au ki Huduma

Ø  Kuto kusamehe kunakunyima kibali mbele za wengine,

Ø  Kuto kusamehe kunaweza kukusababishia madhara ya kimwili pia

Ø  Kunaweza kukuondolea upendo(mathayo 24:12)Na kwasababu ya kuongezeka maasi upendo wa wengi utapoa

v  Unaweza kukosa Roho ya huruma kabisa

v  Unaweza kuwa Mchoyo kabisa, unaweza kufa ki-mwili na kiroho,

Waefeso 4:32 Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. -

Hitaji kuu la kanisa la leo ni kusamehe na kusahau

Mateso makubwa yanayotesa kanisa la leo ni ile Roho ya kuto samehe na kusahau  huu umegeuka kuwa  Mtihani kwa watu wa Mungu,

 iwe kwa waamini au wasiyoamini mtihani huu umewaangusha watu wengi sana unawafelisha watu wengi sana, bila kuiangalia kiwango cha kumjuwa Mungu, jifunze leo kusamehe na kusahau,

Nchi na Nchi zinapigana kwaajili ya kuto kukubali suluhu ya kusamehana na kusahau,

Watu wangine wamefungwa bila hatia kwasababu ya roho ya kisasi,watu wamenyimwa madaraka, wametengwa makanisani,katika huduma,watumishi kwa watumishi, matajiri kwa masikini

Majumba ya ibada ni hivyo hivyo Malumbano kila kukicha Malumbano hayo yote ni kuto kusamehana na kusahau Wanandoa watateseka  sana  kinacho watesa niyalemakosa yaliyopita siyo ya leo yaliyotendeka leo ni sababu tu, jifunze kusamehe na kusahau Ndoa yako itakuwa salama yote hayo ni kuto samehana na kusahau, watoto kwa wazazi  kutosamehana na kusahau

Kumewafarakanisha katika jamii, kupotezana, kutokusaidiana kutokuheshimiana,

Majirani jamii nzima kusameheana na kusahau, kumekuwa shida Dua yangu na Maombi Mungu atusaidie Sana,

Tufanye nini ili kusamehe na kusahau

Kwa kuwa si Mpango wa Mungu kuweka kisasi basi hayo yote tusimwangalie  Mwanadamu kama adui katika liletunalotendewa, Bali tumwangalie Muovu kwa Macho ya Rohoni, na tufahamu kuwa Kila uovu unaotendeka Malengo makubwa ya ibilisi ni kutuangamiza tu,

Hosea 4:6 watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa mithali 1:7 kumcha Mungu ni Chanzo cha maarifa

Wimbo ulio Bora 8:7 Dawa ya haya yote ni Upendo maana upendo hauhesabu maovu, pia maandiko yanatufundisha  hata Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.(kuchekwa)
            Watu wengi wanapenda kuuongelea upendo sana hata mara nyingine kufundisha ila anapokosewa upendo unayayuka ghafla kutamka kinywani neno lolote ni Rahisi sana, tena sana  kazi kuliishi lile unalolinena,

1wakorintho 13:1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.


Kutokusamehe na kusahau ni Roho ambayo inaweza kukaribisha Maroho Mengine mabaya zaidi na ili yakuuwe, yohana 10:10 kutokusamehe kunafunguwa mlango wa kuibiwa,kuchinjwa,kuharibiwa mali kuuwawa, shugulikia Roho ya kuto samehe na kusahau, roho ya mashitaka futa,

 

Hitimisho Maombi:

Baba ninaomba uniponye na matatizo yaliyoingia ndani yangu kwasababu ya kutokusamehe na kusahau  katika Jina la Yesu. Leo ninabadilika katika Jina la Yesu. Mimi ni mzima na nimeponywa katika Jina la Yesu…..

Futa hati zote  za mashitaka, alizotunza Ibilisi, ili usijekukumbushiwa na Ibilisi mengine tena

Ufunuo 12:10. "Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa Damu ya Mwanakondoo na kwa Neno la ushuhuda wao, ambao hawakupenda Maisha yao hata kufa,

Baba katika jina la Yesu ninafuta mashitaka yote yaliyoandikwa dhidi yangu, familia, biashara, uchumba, elimu,kazi, kwa Damu ya Mwanao wapekee Yesu kristo  kila shitaka lililokuwa limeifadhiwa Makitaba ya Ibilisi ninaifuta sasa hivi, katika jina la yesu,

1Petro 1:10

Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia;
2 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.


3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;
4 tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu.


5 Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.


8 Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,
9 katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu.
10 Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.

Somo hili ni maalumu maishani mwako pata DVD,CD,VCD, Utasaidika sana piga 0756 809 209 au 0653 29 42 19

Ila kuishinda Roho hii ni kuomba Mungu akupe Roho ya upendo

1wakoritho 13:4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;


Tufanye nini ili kuweza kusamehe na kusahau,

Nirahisi sana jichunguze Moyoni mwako yupo nani yupo muovu iblisi au Bwana yesu, ikiwa ndani yupo kristo Yesu yeye ni msingi wa upendo andoa shaka, omaba sasa kupitia Roho Mtakatifu akusaidie kukusanya kila ubaya wa Namna zote uliyokuwa umerundikana ukakusababishia kuto samehe

,waefeso 3:17 Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;


Hitimisho kwaajili ya wewe kuwa salama Baada ya kufanya sala ya toba maagizo Maalimu toka kwa bwana Mungu

Kumbu kumbu la Torati 6:5,11:1,mathayo 22:37 ,Marko 12;31,Luka 10:27   Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.


Yote ya yote Maagizo aliyoyaagiza Bwana yesu ambayo leo kanisa limeyaacha kabisa  ni haya maagizo hapa,

Mathayo 5:44,mathayo 10:36 , lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
sasa nakuomba

Mathayo 13;25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
Anza kushugulikia pando ambalo hakulipanda Baba wa Mbinguni na uanze pia kusamehe na kusahau kisha  uanze kuombea Adui zako Masamaha pia 

Wahoo somo Hili linapatikana pia katika DVD,VCD,CD

Yapo masomo mengine mengi yanayokufaa sana,

Ukihitaji Masomo mengine agiza utayapata,

v Siri kuu tatu za kutuza siri zako

v Upenyo wa kumiliki

v Nguvu ya kinywa

v Hatima iliyopindishwa

v Ushindi katikati ya vita

v Jifunze kusamehe na kusahau na mengineyo mengi, pia utapohitaji ushahuri au maombi umbali usikuzuwie kuhudumiwa piga simu kisha utapata nafasi ya kuongea live na Mtu wa Mungu Nabii Samson, piga sasa ni bure 0756 809 209 .0653 29 42 19 
 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments