Kanisa la KKKT Imani Makongoro Mwanza wazindua Jubilee ya miaka 25 na ufunguzi wa kanisa jipya

Kanisa la KKKT Imani Makongoro Mwanza jumapili iliyopita limezindua Jubilee ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, huku Watumishi wa Mungu na Wakristo mbalimbali wakihudhuria ibada hiyo ambayo imeongozwa na Askofu Andrew Gulle wa Dayosisi ya Mwanza. 
Uzinduzi huo  umekwenda sambamba na harambee kubwa ya kuchangisha Takribani kiasi cha  shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya  Imani Lutheran School. 

Kilele cha Maadhimisho hayo kinatarajiwa kufanyika tarehe 31.August 2014 ambapo miradi mbalimbali itazinduliwa na kuwekwa wakfu. 

 
Mgeni rasmi katika harambee hiyo alikua ni Askofu Mkuu wa Makanisa yaKKKT Tanzania Alex Malasusa  ambapo pamoja na pongezi kwa jubelee hiyo pia amewashukuru washarika wa Imani kwa moyo wa kumjengea Mungu kanisa zuri na la kifahari litakalowawezesha watu wengi kujumuika pamoja na kumuabudu Mungu.

picha za matukio hiyo ni kama zinavyoonekana hapa

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama wakiimba
Wapigaji wakipiga muziki wa Kijitonyama
 
 
Kwaya ya Imani kkkt Makongoro wakiimba
 
  Vitabu vya Mungu navyo vilikuwepo kama Biblia na vinginevyo kama inavyoonekana.
                      Mwonekano wa Kanisa la Kkkt Imani Makongoro Mwanza.
                             Chanzo: Mjap inc blog

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments