“KILA MTU AMEUMBWA KWA MAKUSUDI MAALUMU NA MUNGU”


Unajua kuna watu ambao huwa wanajilaumu kwa naman ambavyo wapo, kuna waschana wengine wanapowaona waschana wenzao ni wazuri zaidi yao basi hujiona kuwa wao hawastahili kabisa, kuwaepo katika ulimwengu wa Warembo, nipende kukuasa wewe Binti ambaye umeumbwa ukiwa na sura mbaya, mshukuru Mungu kwa kukuumba hivyo, maana amekuepusha na mambo mengi ambayo yangekunasa endapo tu kama ungepewa uzuri.
 Na Abel Suleiman Shiriwa
Maana wapo waschana ambao ni wazuri ambao wanautumia uzuri wao kufanya ukahaba kwa kuwa tu uzuri wao unawashawishi wanaume kuwahitaji, wapo ambao wana makalio makubwa hao ndo kabisa maana ukiwa nje na Kristo uzuri wako hauna thamani, wewe mwanamke uliye na sura mbaya, huwezi jua Mungu amekupa sura hiyo kwa kujua kuwa kama angekupa sura nzuri basi ungekuwa ni mtu wa kuringa sana, na ungelikuwa Malaya wa kutupwa, hivyo usimkufuru, pengine umeumbwa hivyo ili uweze kuifanya kazi ya Mungu kwa kweli, maana usiangalie utu wa nje bali utu wa ndani hivyo hupaswi kulegea katika kumtumikia Mungu, usijiulize mbona wewe hutongozwi sana kama Fulani….
2 Korintho 4:15 Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.
16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.

Na wewe mwanamke mzuri umepewa uzuri huo na Mungu kwa makusudi maalumu ya kuipeleka kazi yake mbele, maana kama wewe uliye na sura nzuri Shepu nzuri, ukiweza kumtumikia Mungu ka kweli, utawafanya hata wale ambao wana sura mbaya, wajione kuwa wao si kitu kwa kutokumtumikia Mungu, kwani watajiuliza kama wewe mzuri ambaye unakutana na vishawishi vingi vya kukutoa katika utaratibu wa Mungu, na umeweza kuvishinda, sasa ni vipi wao wabaya washindwe kumtumikia Mungu? Uzuri wako utakuwa ni moja ya kivituo kwa watu kuja kumtumikia Mungu kwa kweli, maana wengi hudhani binti mzuri hawezi kuwa mcha Mungu….. hivyo utumie uzuri wako kwa kazi ya Mungu, maana utakuja daiwa siku ile iliyo kuu siku ambayo watu tutakimbiana siku ambayo usiitamani kuikuta kwa wewe mwenye dhambi


                                         By Abel Suleiman Shiriwa

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments