Kongamano la Devine Heritage katika Taswira na mvuto wa kipekee ndani ya jiji la Mwanza



Wakifundisha kwa nyakati tofauti Watumishi hao wa Mungu wameelezea umuhimu wa kupata maarifa na ufahamu utakaomuwezesha mkristo kutambua haki zake za urithi toka kwa Mungu  na kuwa katika nafasi nzuri ya kupokea urithi huo ambao umekwisha andaliwa na Mungu ambao huambatana na baraka za rohoni na mwilin.

Kongamano kubwa la kiroho likiwa na kauli mbiu ya Urithi wa Kiungu (Devine Heritage) limefanyika jumapili hii jijini Mwanza na kuhudhuriwa na mamia ya watu toka kada mbalimbali  na kutoa mafundisho ya kiroho kwa makundi tofauti tofauti ya watu ikiwa ni pamoja na makundi ya vijana wazee na wasomi wa vyuo vikuu vya jiji la Mwanza


Kongamano hilo lililoanza mida ya saa tisa alasiri mpaka saa 12jioni awali lilitanguliwa na vikundi mbalimbali vya sifa na kuabudu ikiwa ni pamoja na Tafes Saut, CBCI Band, New Creation Band na mwimbaji binafsi Epafrodito 

Wazungumzaji wakuu ambao walipata fursa ya kuzungumza katika kongamano hilo ni pamoja na Mchungaji Goodluck Kyara kutoka kanisa la NVCC la jijini Mwanza, Mchungaji Denis Sebastian Kiandika kutoka kanisa la MICC -Mwanza, na na Mchungaji Bill Brown ambao kwa pamoja  waliweza kuzunguza na kuwasilisha jumbe mbalimbali za kiroho zikiwa na mafundisho ya kumjenga muamini katika kuuelewa urithi wa kimungu ndani ya Maisha ya Mwanadamu hususani katika kipindi hiki cha sasa. 
Mchungaji Bill Brown


Baadhi ya picha za kongamano hilo ni kama zinavyoonekana hapa chini  







 

 

katika kongamano hili binti huyu aitwaye Bahati aliama kujitokeza na kumpa Yesu maisha yake na kuokoka, katika picha hii akiongozwa sala ya toba na mchungaji Zakayo Nzogere wa kanisa la MICC Church
 

                                                         Chanzo: Mjap inc blog

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments