LEO NI LEO UKUMBI WA PTA SABASABA DAR ES SALAAM

Askofu Kakobe
Leo ni leo katika ukumbi wa PTA uliopo viwanja vya Mwalimu JK Nyerere almaarufu kama viwanja vya sabasaba vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, wakati ambao waumini wa makanisa ya kipentecoste watakapokutana asubuhi ya leo kuhitimisha mfungo wa siku 40 ikiwa ni kuombea Taifa.
Askofu Gwajima

Kupitia tukio hilo, askofu Zachary Kakobe wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship pamoja na askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima wanatarajiwa kufundisha masomo tofauti ili kuwaweka sawa watu watakaohudhuria tukio hilo kabla ya kuingia kwenye kipindi cha maombi kwa Taifa. Viongozi wengine ni pamoja na mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste nchini askofu David Batenzi pamoja na katibu wake askofu David Mwasota wa Naioth Gospel Assembly na viongozi wengine wa makanisa ya Kiroho wanatarajiwa kuwepo siku ya leo.

Kwa taarifa hii mabayo mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste mjini Dar es Salaam, askofu Bruno Mwakibolwa, waamini wanatakiwa kufika kuanzia saa tatu asubuhi, na kisha ratiba ya mafundisho na kisha kuendelea na maombi, ikiwa ni siku ya hitimisho katika siku 40 ya maombi yalioanza mnamo Januari 6 2014. 
                             Na Gospel kitaa
 
 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments