BWANA YESU
asifiwe ndugu
Karibu
katika fundisho hili muhimu linalohusu maombi.
1
Thesalonike 5:17-18. ombeni bila kukoma;
shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika KRISTO YESU.
Maombi ni
muhimu sana kwa kila mwamini.
Yeremia
17:14.Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.
Maombi ni
mahitaji ambayo mwanadamu anapeleka kwa muumba wake.
Maombi ni
maneno maalumu anayoyatamka mwamini kwa imani ili yaende kwa muumba wake,
ambaye siku zote yuko tayari kujibu maombi.
Maombi ni
maisha ya mwamini.
Zaburi 27:8.Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.
Maombi ni
njia ya mawasiliano kati ya MUNGU na
watoto wake waliosafishwa kwa damu ya mwanawe wa pekee YESU KRISTO.
Maombi ndio
mawasiliano kati yetu wanadamu na MUNGU Baba yetu.
Ili uhusiano
wetu na MUNGU uwe hai lazima tuwe
waombaji.
Zaburi 62:8. Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; MUNGU ndiye kimbilio letu.
MUNGU
huongea na sisi kwa njia ya neno lake kupitia kusoma kwetu Biblia na huongea na
sisi kupitia watumishi wake, na sisi tunaongea na MUNGU kwa njia ya maombi,
hivyo ili uhusiano wetu na MUNGU uwepo lazima tuwe na muda wa maombi.
KUNA MAOMBI
YA AINA NYINGI.
Wakolosai
4:2.Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;
,
tusome pia Yakobo 1:5.Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa MUNGU, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
1: Maombi ya
shukrani.- Tunamshukuru MUNGU na kumrudishia heshima kwa aliyo yafanya kwetu.
Mfano ametulinda, ametuokoa n.k
2: Maombi ya
kusihi- Tunamsihi MUNGU juu ya jambo Fulani tunalolihitaji, mfano MUNGU aponye
nchi yetu, awafungue ndugu zetu waliofungwa na dhambi au mambo mengine.
3: Maombi ya
kuomboleza- unaomboleza juu ya jambo baya lililokupata mfano ukimwi, au motto
wako kupatwa na kichaa n.k
4: Maombi ya
toba. - Haya ni muhimu sana na ni ya kwanza kabisa maana kutubu kwanza ndilo
jambo la muhimu sana kwa kila mwanamaombi. Kutubu ndio kumruhusu MUNGU
ashughurike na mahitaji yako. Maombi ni unyenyekevu.
5: Maombi ya
vita: - Haya ndio maombi muhimu zaidi, hata kama maombi yote ni muhimu sana. Hapa
unatumia mamlaka ya KRISTO iliyoko ndani yako kuharibu mipango ya shetani juu
ya maisha yako. N.k.
6: Maombi ya
kufunga: - Unafunga kuombea jambo Fulani na wakati wa kufunga unaweza ukahusika
na aina zote za maombi hapo juu.
Zaburi 34:4. Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.
-Aina zote
za maombi ni muhimu sana, na kwa kuomba maombi ya kweli ndio uhusiano wako na MUNGU unakua mzuri zaidi.
-Yapo mambo
mengi ukiyafanya yatakuweka katika uhusiano mzuri na MUNGU katika KRISTO. Mfano
kumtumikia, utakatifu, kumtii ROHO MTAKATIFU lakini mimi najua ya kwamba
haiwezekani kuyatimiza hayo yote bila kuwa mtu wa maombi, hivyo maombi ni
muhimu sana.
Zaburi
66:20. MUNGU kwetu sisi ni MUNGU wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA BWANA.
Sio kila
maombi yanajibiwa na sio kila mtu ana sifa za kuomba na akajibiwa.
Sifa ya
mwombaji anayeweza akaomba na akajibiwa ni kwanza kumpa BWANA YESU KRISTO
maisha yako, na kufanya toba ya kweli na kukaa ndani ya KRISTO. Yeye anasema
hivi katika Yohana 15:7 . Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Tena
waliompokea BWANA YESU yeye aliwafanya kuwa watoto wa MUNGU ndio wale waliaminio jina
lake(Yohana 1:12)
Tuombe
katika jina la YESU KRISTO.
Tuombe
katika ROHO MTAKATIFU.
Tuombe kwa
imani
Tuombe maana
MUNGU hujibu maombi.
Tena BWANA YESU anasema katikaYohana 14:14.kiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
Kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa
mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na
wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU
akubariki sana .
Ni mimi
ndugu yako
Peter M
Mabula
Maisha ya
Ushindi Ministry.
0714252292
Comments