Mwl.
Sospeter Simon S. Ndabagoye.
New
Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
|
Mada Ndogo: Dalili 10
za mtu mwenye mapepo.
Lengo kuu: kuyajua
mapepo na kazi zake.
Lengo Mahsusi: Kila
mtu kuweza kumpinga pepo na kazi zake zote kwa Jina la Yesu.
Bwana Yesu asifiwe
sana,
Ndugu mpendwa,
katika sehemu tatu zilizotangulia,tumejifunza maana,asili/ chanzo cha ,mapepo. Natumai
umebarikiwa sana. Haleluya! Ndugu mpendwa, napenda kukukarisha katika
mwendelezo wa mafundisho yetu juu ya mapepo,ambapo kwasasa tutaangalia kwa kina
tabia/dalili za mtu aliyevamiwa na mapepo.
Ni muhimu sana
kujua hili. Tabibu mzuri, ni yule anaetibu ugonjwa anaoufahamu, hivyo ni muhimu
sana,kujifunza habari hizi,ili kuweza kukabiliana na kila hali kwa usahihi
wake.
Pamoja na dalili
nyingine ambazo sitazitaja; kwapamoja tuzichunguze hizi zifuatazo:-
(a) Kuwa na nguvu nyingi. Kwa hali
isiyo ya kawaida,mgonjwa aliyedhoofu na pengine kulala kwa muda mrefu akiwa
hajiwezi, huweza kuwa na nguvu nyingi sana na za ajabu. (Luka 8:28,Marko
5:3&4,Luka 8:29,Matendo 9:15&16). Mtu huyu, huweza kuwa mkali
sana,mgomvi na wakati mwingine huweza kuwa na uvutano kama umeme/shoti. Hujiamini
sana,na hukasirika zaidi anapowaona wanamaombi.
(b) Kujaa ujasili na kujiamini kupita kiasi. Mtu aliyevamiwa na pepo wachafu,hujiamini na kujiona shujaa; tukio
hili hulenga kumchosha mwili,kuwaumiza wanaomuuguza na yeye mwenyewe. Anaweza kujiangusha
bila sababu,kujiuma meno,kutafuna baadhi ya sehemu zake za mwili,kujipiga,kujiuma
meno,kujikatakata n.k. (Mathayo 17:15,Marko 5:5). Pia,mapepom hutumia njia hii
ili watu wamwogope washindwe namna ya kumsaidia mtu wa namna hii kwa kuhofia
usalama wao, na kubaki kumwonea huruma tu.
(c) Huonesha maumivu hata anapojiumiza mwenyewe ila
haachi kujiumiza. Hili hutokana na kuwa yeye
hajitawali,bali hutawaliwa na kuongozwa na pepo wabaya. Huumizwa sana ndani kwa
ndani,ila hulazimika kuendelea kufanya kile kitu kinachomuumiza. Mfano,
kujikatakata,kujiangusha, kurukaruka n.k. (Marko9:20-22).
(d) Kutokwa povu mdomoni na kuzirai.
Mtu aliye na mapepo,anakawaida ya kupoteza fahamu. Aghalabu, hutokwa povu
mdomoni anapokuwa hajitambui (Marko9:20). Tukio hili,huwa ni lakumfanyia
mazoezi mtu huyu katika maandalizi ya kumuua. Humhamisha kimazingara na kuanza
kumchezea, wakati wingine mtu huweza kufa mara moja. Kifo cha namna hii,huwa si
kifo halisi,bali huwa amahamishwa kimazingara/uchawi.
(e) Kunena/kuongea kupitia kinywa cha mgonjwa. Mapepo huweza kujitokeza na kunena hadharani,huku yakitoa amri au
maelekezo juu ya mahitaji yao. Mengine hudai yanataka damu,yametumwa damu na
baadhi ya mambo. (Mathayo 8:29-31,Marko5:5). Kitendo hiki cha
kuilaghai,hupelekea uchonganishi,uhasama miongoni mwa jamii na hata maamuzi
mabaya. Ndugu mpendwa,usimsikilize pepo,siku zote yeye ni mharibifu tu,hawezi
kusema ukweli, na usifuate maelekezo yake,daima msikilize MUNGU.
(f) Wanaweza kutumika kama walimu makanisani kwa
mafunuo,ndoto au maono. Hizi roho zinaweza kuleta mafunuo
yanayolenga kuwaaminisha maumini kuwa ni mafunuo ya ki Mungu,ili kutaka
kuwateka waumini na kuyaamini. Unapaswa kuwa makini sana katika hili. Kumbuka hata Sauli, alitoa unabii kipindi
anateswa na roho wabaya.(1Timotheo4:1-5). Jiepushe kuyasikilza maneno
yanayonenwa na mtu aliyepagawa na mapepo.
Nb: mapepo yanaweza kuongea habari juu
ya Yesu, ila tu,hayawezi kuongea habari sahihi juu yake.(Matendo
16:16&17,Marko1:24). Usikubali kuyasikiliza wala usiyahoji,yanadanganya tu,
kumbuka,hata Yesu aliyakemea yaondoke tu,hata yalipotaka kuongea jambo
lolote,yeye aliyaamuru yaondoke (Marko1:34)
(g) Humwamuru mtu kujitenga. Humtenga
mtu na watu wengine. Humpeleka maeneo yasiyoyakawaida. Mfano misituni,vichakani,mtoni,kwenye
maziwa na bahari,makaburini nk(Luka8:27). Lengo ni kutaka huyu huyu mtu
aendelee kuogopwa, lakini pia kumtenga na maeneo ambayo ibada na MUNGU wa kweli
hutajwa. Kumkimbuzia maeneo yaligubikwa na ibada za kipepo ili kuweka mikataba
zaidi na kuendelea kumfunga.
(h) Kufanya mambo ya ajabu na aibu. Humwondolea
utu wake na sitaha. Huishiwa ustaarabu, ndiyo maana anaweza kutembea
uchi,kujiasaidia hadharani,kula vyakula vichafu, kufanya mambo yasiyofaa kwa
furaha na kwa uhuru wote. Hii ni
kwasababu, anakuwa ametengwa na jamii (Luka 8:27) hivyo huwa si sehemu ya mila
na utamaduni wa jamii hiyo.
(i) Kuteswa kwa magonjwa ya mwili. Pepo
akishamaliza kuingia, mtu huweza kumtesa
kwa magonjwa ya kawaida kabisa ili kupumbaza wanaomuuguza mtu,wasijue chanzo
cha tatizo.pia hutafutia kisababu cha kumuua.
Mfano
wa baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na mapepo ni:-
Ububu
(Marko 9:17)
Uziwi
na ububu (Marko 9:25)
Upofu
na Ububu (Mathayo 12:22)
Kupooza/
uwete (Matendo 8:7)
Kifafa
(Marko 1:26,9:20, Luka 9:36) n.k. hufunga masikio kwa uziwi na kinywa kwa ububu
ili kutomfanya mtu aweze kujieleza au kukili imani ya wokovu,hii ni kinga kwa
mapepo ili kuendelea kumuweka chini ya himaya yao.
(j) Kuabudu miungu/ sanamu.(Walawi17:7,Torati
32:17,Ufunuo 9:20). Wakati mwingine,mtu alifungwa na mapepo, huweza kufundishwa
ibada za sanamu na kuanza kuzifanya. Wengine husema, anamizimu ya kiganga (Walawi
20”27), na kujenga uhusiano na mizimu (1Samweli 15:23) kitendo kinachoplekea
kuwa mchawi (Isaya 47:9-13,Matendo 19:18&19).
Ndugu yangu mpendwa, habari hizi ni nzito
sana,na unapaswa kuzijua ili kujiepushwa nazo wewe na uzao wako na kizazi chako
chote.
Swali
la kujiuliza ni je, kufukuza pepo ndiyo uponyaji, au kuna uponyaji bila ya
kufukuza pepo?
Kama
tulivyoona, mapepo husababisha magonjwa, hivyo ili mgonjwa apone sharti pepo
atoke.afukuzwe. kuna watu wanajidai eti
wanatuliza mapepo, hakuna jambo kama hilo, kikubwa ni kumkemea pepo kwa Jina la
Yesu, aondoke akae Roho Mtakatifu.
Mungu
aendelee kukubariki na kukufunulia zaidi.
Endelea
kujifunza pamoja nasi katika sehemu ya Tano, ili kujua hatua 8 katika
kuyafukuza mapepo.
Mwl.
Sospeter Simon S. Ndabagoye.
New
Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
+255 757 464 141
+255 784 464 141
+255 712 909 021
E-mail: sos.sesi@yahoo.com
+255 784 464 141
+255 712 909 021
E-mail: sos.sesi@yahoo.com

Comments