Mialiko yote hushtusha sana na kuamsha hamasa kubwa.
Twajisikia ya kwamba ni ya muhimu sana, pia yatuhamasisha
kweli. Kwa maana hiyo basi, tuitikie na mwaliko huo wa
kwenda mbinguni kwa sala fupi kama ifuatavyo:
»BWANA YESU, nimeishi hadi leo kama wewe
haupo. Nimetambua sasa, wewe u nani na kwa saba-
bu hiyo naja kwako mara ya kwanza kwa sala. Najua
sasa ya kwamba kuna Mbingu na Jahanamu. Niokoe
na jahanamu, mahali ambapo kwa dhambi yangu na
kutoamini kwangu ningestahili kwenda. Ni hamu yangu,
kuwa pamoja nawe mbinguni milele. Najua ya kwamba
siwezi kufika mbinguni kwa matendo yangu mazuri,
bali kwa kukuamini wewe. Kwa sababu wewe hunipen-
da ukanifia msalabani na kubeba makosa yangu yote
na kunilipia. Nakushukuru kwa hayo. Waona dhambi
zangu, hata yale yote kuanzia ujana wangu. Kila dham-
bi mojamoja ya maisha yangu waijua – yote ninayo-
kumbuka na zile ambazo nalisahau. Wewe wanijua
kabisa. Waelewa hisia zote za moyo wangu, ikiwa ni
furaha au masikitiko, ustawi au kukata tamaa. Mimi
ni kama kitabu kilicho wazi mbele yako. Jinsi nilivyo
na jinsi maisha yangu yalivyo hadi sasa, siwezi kuis-hi nawe na MUNGU aliye hai na ningestahili kuikosa
mbingu. Kwa hiyo nakusihi, unisamehe dhambi zangu
zote. Nasikitika kwa ajili ya dhambi zangu. Tafadhali,
nisaidie kuvua yote yasiyo sawa mbele zako na unipatie
uadilifu unaoniwezesha kuishi chini ya baraka zako.
Nifungulie uelewo wa Neno lako la Biblia. Nisaidie
kuelewa unachotaka kuniambia, ili nipate nguvu mpya
na furaha ya maisha kutoka katika Neno lako. Wewe
ni BWANA wangu kuanzia sasa. Mimi ni mali yako na
ninataka kukufuata. Unionyeshe njia ambayo naweza
kwenda. Nakushukuru kwamba umenisikia. Naamini
ahadi yako ya kwamba kwa kukugeukia nimepata kuwa
mtoto wa MUNGU, ambaye atakuwa pamoja nawe mbin-
guni milele. Nafurahi sana kujua, mimi ni pamoja nawe
na wewe u kwa kila hali upande
wangu. Nisaidie kukutana na watu
wanaokuamini na niweze kushiri-
ki katika kanisa ambapo naweza
kupata kusikia na kulishwa Neno
lako daima. Amina.«
MUNGU akubariki sana na kwa ushauri na maombezi wasiliana nami kwa namba 0714252292.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
Maisha ya ushindi ministry

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12
Comments