NI DHEHEBU GANI LA KIKRISTO LEO???


Na mtumishi wa MUNGU Sam Balele
Kanisa la kwanza lilihubiri Wokovu na watu Waliamini na Kuokolewa. Baada ya watu Kuamini Habari Njema ya Injili ya Yesu Kristo, watu Walibatizwa na kufanyika wanafunzi wa Yesu na kujiunga na wanafunzi wengine na kwa jinsi hiyo Kanisa liliongezeka. Kanisa la kwanza lilitembea katika Huduma (vipawa) zote Tano (Mitume, Manabii, Wainjilisti, Walimu na Wachungaji), Huduma zote Tano zilikuwepo. Kanisa la kwanza lilitembea katika Karama zote Tisa za Roho Mtakatifu, bila kubagua hata karama mojawapo na kutengeneza visingizio. Kanisa la kwanza lilitembea katika kutenda kazi zote. Kanisa la kwanza lilifanya sawasawa na Agizo la Bwana la kuhubiri Injili kwa kila kiumbe, Injili AMBAYO NI UWEZA WA NGUVU UULETAO WOKOVU KWA KILA AAMINIYE, na kisha kufundisha yale aliyoamuru Bwana Yesu. Kanisa la kwanza lilibatiza baada ya mtu kuamini Ujumbe wa Injili iletayo Wokovu kwake yeye aaminiye na kufanyika mwanafunzi, na kwa ubatizo huo, huyo mtu alikuwa anakiri kile alichoamini, na hivyo kufanyika kUwa wa YESU KRISTO. Kanisa la kwanza lilitembea katika Ishara zote alizosema Bwana Yesu kuwa wale wamwaminio wataambatana nazo na wala hakukuwa na longolongo. KAZI, HUDUMA, KARAMA, NA ISHARA VILITEMBEA NA KANISA LA KWANZA. LEO KUNA WAZIMU GANI NA UPUUZI GANI UNAENDELEA KATIKA MADHEHEBU YA KIKRISTO? JE HAYA MAMBO YAPO? NA KAMA YAPO JE YAPO KWA KIWANGO GANI? NA KAMA HAKUNA, JE NI NINI SABABU YA KUTOKUWEPO? DHEHEBU GANI LA KIKRISTO LEO LINAWEZA KUJILINGANISHA NA MTEMBEO WA KANISA LA KWANZA? NA KUSEMA LIKO KATIKA RAILTRACKS IZIPASAYO KANISA LA YESU KRISTO? ULE MWILI WA KRISTO AMBAO YESU ALIMUULIZA SAUL SAUL KWANINI UNANITESA....NI DHEHEBU GANI LEO LINA UJASIRI WA KUSEMA SISI NDIO WENYEWE? KWA KUJIFANANISHA NA MTEMBEO WA KANISA LA KWANZA, LA WALE WANAFUNZI WALIOITWA WAKRISTO PALE ANTIOKIA, NA TENA WAKAITWA WATU WA MADHEHEBU YA WANAZORAYO, HUKU MTUME PAULO AKINENWA KUWA KIONGOZI WAO....NI DHEHEBU GANI LA KIKRISTO LEO LINA UJASIRI? UJASIRI WA KUWEKA KELELE ZA MAFUNDISHO YAKE PEMBENI NA KUSEMA SISI NI KAMA WALE WA KANISA LA KWANZA, KWA KAZI LIFANYAZO, HUDUMA TANO NDANI YAKE, KARAMA TISA ZA ROHO MTAKATIFU NA UDHIHIRISHO WA ISHARA ALIZOSEMA BWANA YESU...NI DHEHEBU GANI LEO?
                              By Sam Balele


Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments