UFAFANUZI WA KARAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU KWA KANISA.



BWANA YESU asifiwe
Karibu katika ufafanuzi juu ya karama 9 za ROHO MTAKATIFU kwa watu waliokombolewa kwa damu ya YESU KRISTO.
Karibu.
1 Kor 12:7 “Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.”

1. Neno la Hekima. Hili ni matamashi ya hekima yanyosemwa kupitia utendaji wa Roho Mtakatifu.Huleta ufunuo wa Neno la Mungu au hekima ya Roho Mtakatifu kwa tukio maalum au tatizo (Mdo 6:10; 15:13-22). Hata hivyo, si sawa na kuwa na hekima ya Mungu kwa ajili ya maisha ya kila siku. Neno la hekima linakuja kwa kulisoma Neno la Mungu kwa bidii na kutafakari njia za Mungu na Neno lake, na kwa kuomba (Yos 1:5-6).

2. Neno la Maarifa. Hili ni matamshiyaliyovuviwa na Roho Mtakatifu yanayoleta ufunuo wa ufahamu kuhusu watu, mazingira, au kweli ya Biblia. Mara nyingi limekuwa na uhusiano wakaribu na unabii (mdo 5:1-10;10:47-48;15:7-11;1Kor 14:24-25)

3.Imani. Hii sio imani inayookoa, lakini imani mahsusi inayatoka kwa Mungu na kuletwa na Roho Mtakatifu inayomwezesha Mkristo kumwamini Mungu matendo yasiyo ya kawaida ya miujiza . ni imani inayohamisha milima (1 Kor 13:2) na mara nyingi inaonekana ikitenda kazi pamoja na karama zingine kama vile uponyaji na matendo ya miujiza (taz. Mt 17:20, maelezo juu ya imani ya kweli;Mk 11:22-24;Lk 17:6)

4. Karama za Uponyaji. Karama hizi zinatolewa kwa kanisa ili kuweza kurejesha afya katika mwili kwa njia ya muujiza (Mt 4:23-25;10:1;Mdo 3:6-8;4:30).Ule wingi “karama “ unaashiria uponyaji wa magonjwa mbali mbali na kuonyesha kuwa kila tendo la uponyaji ni karama maalum kutoka kwa Mungu . Ijapokuwa karama ya uponyaji haitolewi kwa kila mmoja katika kanisa kwa njia maalum (ling 1Kor 12:11,30),waumini wote wanaweza kuombea wagonjwa. Mahali palipo na imani wagonjwa watapona (taz. Makala juu ya UPONYAJI WA KIMUNGU,UK.1502).Uponyaji unaweza kuja kama matokeo ya kutii maelekezo ya Yos 5:14-16(taz.Yos 5:14-16 maelezo).

5. Matendo ya Miujiza. Haya ni matendoyanayotoletwa na nguvu za Mungu mwenyewe yanayobadilisha mwenendo wa kawaida wa mambo ya asili. Ni pamoja na matendo ya nguvu za Mungu ambapo ufalme wa Mungu unadhihirishwa dhidi ya Shetani na pepo wabaya (taz. Yn 6:2, maelezo;taz. Makala juu ya UFALME WA MUNGU, uk.1510).

6. Unabii. Inatupasa kutofautisha kati ya unabii kama udhihirisho wa muda tu wa Roho.(1 Kor 12:10) na unabii kama karama na huduma ya kanisa(Efe 4:11).kama karama ya huduma, karama ya unabii inakirimiwa kwa baadhi ya waamini tu, ambao hawana budi kufanya kazi kama manabii ndani ya Kanisa (taz. Makala juu ya KARAMA ZA HUDUMA ZA KANISA,uk.1928) kama udhihirisho wa kiroho, unabii ni karama inayoweza kupatikana kwa kila Mkristo aliyejazwa Roho Mtakatifu (Mdo 2:17-18)

Kuhusu utabiri au unabii kama udhihirishowa kiroho:(a )unabii ni karama maalumu inayomwezesha kuleta neno la ufunuo moja kwa moja toka kwa Mungu kwa msukumo wa Roho Mtakatifu (1 Kor 14:24-25;29-31). Unabii hapa sio kuleta ujumbe au mahubiri yanyotayarishwa awali. (b) Katika Aj na Aj, unabii kimsingi si kutabiri mambo yajayo baadaye, lakini kuyatangaza mapenzi ya Mungu na kuwaonya na kuwatia moyo watu wa Mungu kuifuata haki, uaminifu na uvumilivu (14:3;taz. Makala juu ya NABII KATIKA AGANO LA KALE,uk.1054). (c)Ujumbe huu unawezakuweka wazi hali ya moyo wa mtu (14:25) au kuleta hali ya kuimarisha ,kutia moyo,kufariji,kuonya na hukumu(14:3’25-26’31).(d) kanisa halipaswi kupokea ujumbe wa unabii kuwa usio na mapungufu yoyote, kwqa sababu manabii wengi wa uongo wataingia katika kanisa(1Yoh4:1). Hivyo, unabii wote hauna budi kujaribiwa ili kuthibitisha uhalisi wake wa ukweli ( 1 kor 14:29,32;1 The 5:20-21)kwa kujiuliza kama unabii unalingana na Neno la Mungu (1 Yoh 4:1), iwapo unasisitiza maisha ya kumcha Mungu (1 Tim 6:3), na iwapo umesemwa na mtu anayeisha ya uaminifu katika Bwana Kristo (1 Kor 12:3). (e)unabii unatenda kazi katika mapenzi ya Mungu na si ,mapenzi ya wanadamu. Aj halioneshi kama lilijihusisha kwa bidii kutafuta ufunuo au uongozi kwa wale wanaodai kuwa manabii. Unabii ulitolewa kwa kanisa pale tu,Mungu alikua chanzo cha ujumbe huo (1Kor 12:11;2 Pet1:21).

7. Kupambanua Roho. Karama hii ni uwezo maalum uliotolewa na Roho ili kwa uhakika kuweza kutambua na kupima unabii na kupambanua iwapo unabii huo umetoka kwa Roho Mtakatifu au sivyo (taz.1 Kor 14:29, maelezo;1 Yoh 4:1).Wakati mwisho unakaribia watakapojitokeza walimu wa uongo wengi (taz.Mt 24:5, maelezo) na upotoshaji wa Ukristo unaofuata Biblia utongezeka sana (taz.1 Tim 4:1,maelezo), karama hii itakuwa ya muhimu sana kwa Kanisa.
8.a. Kunena kwa Lugha. Kwa habari ya “lugha” (Gk glossa,linalomaanishalugha)kama udhihirisho wa Roho,mambo yafuatayohayana budi kuzingatiwa:

b. Kunena kwa lugha kunaweza kuwa katika lugha kunaweza kuwa katika lugha zinazozungumzwa sasa (Mdo 2:4-6) au lugha isiyojulikana duniani, k.m lugha…za malaika” (1 Kor 13:1; taz.sura ya 14, maelezo;taz.makala juu ya KUONEKANA KWA LUGHA,uk.1734).Usemi wa jinsi hii hautokani na kujifunza na mara nyingi haueleweki kwake anenaye (14:14) na kwa wale wanaosikia (14:16).

c..Kunena kwa lugha hujumuisha roho ya binadamu na Roho wa Mungu kuingiliana ili mwumini aweze kuwasiliana na Mungu moja kwa moja (yaani, katika maombi,kusifu, Baraka au shukrani), kuonyesha au kutamka katika ya ngazi ya roho ya mtu badala ya akili ,(1Kor 14:2,14) na kujiombea mwenyewe au kuwaombea wengine kwa msukumo wa moja kwa moja wa roho Mtakatifu mbali ya shughuli zinazoendelea katika akili(ling.1Kor 14:2 ,15,28;Yuda 1:20)

d. Kunena kwa lugha katika kusanyiko ni lazima kuambatane na tafsiri iliyotolewa na Roho mwenyewe, ambayo inaleta yanayozungumzwa na maana ya matamshi yenyewe kwa jamii ya waaumini .( 1Kor 14:3,27-28). Ujumbe wake unaweza kuwa wa ufunuo,ufahamu, unabii au mafundisho kwa ajili ya kusanyiko(ling.1Kor 14:6)

e. Kunena kwa lugha katika kusanyiko lazima kufanyike kwa utaratibu. Anayenena hatakiwi “kutekwa na hisia” au “ kushindwa kujidhibiti”(1Kor 14:27-28;taz. Makala juu ya KUNENA KWA LUGHA,uk 1734).



9.Tafsiri ya lugha. Huu ni uwezo unaotolewana Roho mwenyewe wa kuelewa na kueleza maana ya maneno yayonenwa katika lugha . Pale yanapofasiriwa kwa ajili ya kusanyiko, lugha hufanya kazi ya kutoa mwongozo wa kuabudu na kuomba au kama unabii. Jumuiya ya waumini ndipo inaponewa kushiriki katika ufunuo huu uliovuviwa na Roho Mtakatifu. Lugha zilizofasiriwa zinaweza kuwa njia ya kujenga wakati kusanyiko zima linapopokea usemi huo (ling.14:6,13)Karama anaweza kupewa Yule anenaye kwa lugha au mtu mwingine. Wale wanenao kwa lugha inawapa pia kuomba karama ya utafsiri (1 Kor 14;:13)





 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments