UWANJA UNAOWAUA WAHUBIRI TANZANIA WAPATA TIBA

Yawezekana umewahi kusikia maneno zamani au hata leo kwamba kuna eneo fulani haliingiliki kirahisi kwasababu ya matambiko ama nguvu za giza zilizoko katika eneo hilo ama mkoa huo. Moja ya maeneo hayo amabyo yamepata tiba ni Handeni huko mkoani Tanga ambako timu ya The Voice of Hope ministries chini ya mkurugenzi wake mchungaji Peter Mitimingi wanawasha moto wa injili.

Baadhi ya umati wa watu waliofika mbele kumkabidhi Yesu maisha yao.


Chini ni maelezo ya mchungaji Mitimingi akieleza kuhusiana na eneo wanapofanya mkutano kwamba wahubiri watatu waliaga dunia....
Hapa ni Handeni Tanga wa Wazigua
Uwanja huu unahistoria ya kuangusha wahubiri jukwaani na kufa.
Wameshakufa wahubiri 3 na maagano yamefanyika kwa miaka mingi kwamba hapa kijijini hakutakuwa na kuristo wala mtu yeyote kuhubiri na atakaye thubutu atakwenda chini futi 6. Tuliposikia hayo majigambo ya adui tukasema lazima tupeleke kikosi cha makomandoo wa Yesu kupitia VHM kwenda kumaliza mzizi wa fitina.
Tulipoanza tu wazee walitengeneza mvua ya radi uwanjani kumdondosha mwinjiristi lakini kama Bwana Aishivyo leo ni siku ya 9 tunakandamiza kwa kwenda mbela na mavuno sio ya kubahatisha HADONDOKI MTU HAPA WALA HAFI MTU HAPA WALA HAKUNA CHA MAFUA WALA NINI chezea nguvu za Yesu aliye hai.

Wakina mama wakimsifu Mungu licha ya mvua kubwa.

Makomandoo wa Yesu wakifanya kazi ya kumtukuza muumba wao.


Hata watoto hawakutaka kupitwa na neema ya neno la Mungu.


Mchungaji Peter Mitimingi akicheza mbele ya Mungu wake.



Moja ya hirizi iiliyosalimishwa na watu waliokuwa wakitenda vitendo vya kishirikina

                               Chanzo: gospel kitaa blog

Comments