WALAKA KWA FILEMONI *sehemu ya pili*

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe....
Haleluya....

Karibu katika fundisho hili zuri,ambalo leo ni siku ya pili ya fundisho.
Walaka huu wa Filemoni ulioandikwa na mtume Paulo ni moja ya walaka mgumu kueleweka ikiwa kama msomaji hukufundishwa dhima ya walaka huu. Tulijifunza kiundani dhima ya walaka huu kupitia fundisho lililopita na tukaishia kusoma walaka huu katika mstari wa tatu( Filemoni 1:3)
Leo tunaendelea...

"Namshukuru Mungu wangu siku zote,nikikukumbuka katika maombi yangu;nikisikia habari za upendo wako na imani uliyonayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote "Filemoni 1:4

Paulo anaanza kutufindisha KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO.
Wengi wamefeli somo la kushukuru,kushukuru ni mtindo wa maisha halisi ndani ya mwamini,maisha ya shukrani ni shule ngumu kuifaulu kwa kutumia akili za kawaida sababu neno shukrani linapaswa litoke moyoni;
na jambo la kushukuru litokalo moyoni huongozwa na Roho mtakatifu. Maisha ya shukrani yamewashinda watu wengi,japokuwa neno SHUKRANI linafundishwa kila siku iitwayo leo.
Hakuna jambo zuri chini ya jua kama kushukuru.

Maana katika kushukuru kuna hali ya koongezeka isiyo ya kawaida.
Chukulia tu, mfano wa mtu ambaye anakushukuru sana kwa jambo dogo ulilomtendea,ni rahisi kumuongezea mtu huyo jambo kubwa (mfano zawadi) hata kama hajakuomba.

Sasa angalia vizuri andiko tulilolisoma hapo juu(Filemoni 1:4) Mtume Paulo
anasema ;"Namshukuru Mungu wangu Siku zote"
neno "Kushukuru siku zote "linaonesha ni kushukuru muda wote,kushukuru kwa kila hali yoyote ile,yaani ni kwa kila aina ya tukio,liwe tukio baya au zuri.
Bali sisi yatupasa kumshukuru BWANA MUNGU maana maandiko yanatuambia;

" shukuruni kwa kila jambo" 1 Wathesalonike 5:18

Hajalishi ni mazingira gani unayopitia,Bali yakupasa kumshukuru Mungu kwa kila jambo,
Iwe ni njaa,
Iwe ni msiba,
Iwe ni ugonjwa,
Iwe ni furaha,
Au iwe hata kukataliwa na mchumba,
Iwe hali ngumu ya kiuchumi N.K
Bali wewe katika mazingira kama hayo,shukuru tu,
maana shukrani haiangalii mazingira yoyote ile.

Yapo mazingira ambayo ni magumu hata mtu kusema ASANTE mbele za Mungu hushindwa,watu wengi hushindwa kwa mazingira hayo.
Mfano ;
Chukulia mazingira kama hayo aliyokuwa nayo Paulo,mazingira ya kufungwa kwa ajili jina la Yesu Kristo,katika mazingira hayo ndiposa tunaona Paulo akimpokea
Onesmo na kumzaa kiroho,kisha akiamwandikia walaka ili ampelekee Filemoni,na bado Paulo akituonesha pendo lake kwa Filemoni.

Sikia sasa;
Ndiposa Paulo anasema anamshukuru Mungu katika mazingira magumu namna hiyo.
Ikumbukwe kwamba walaka huu uliandikwa na Paulo akiwa gerezani,hivyo Paulo alikuwa katika kipindi kigumu,lakini tunaona Paulo akijawa na shukrani pamoja na pendo juu ya Filemoni na kwake Onesmo maana mtume Paulo hakuangalia mazingira magumu aliyokuwa nayo . Mtume Paulo anamuandikia Filemoni kana kwamba yeye Paulo yupo huru.

Paulo anasema anamkumbuka Filemoni katika maombi yake,maana yake ni kwamba;
Paulo alikuwa akiendelea kumuomba Mungu kwa maisha ya Filemoni,hata kama Paulo alikuwa amefungwa lakini bado anazidi kumuombea Filemoni.
kumbe hata kama utakuwa umefungwa jera bado haikupasi kujiombea mwenyewe,Bali ombea wengine hata wasiofungwa.

Haleluya..

Ukitumia ufahamu wa kibinadamu wa kawaida- ni vigumu kumuombea mtu ambaye yupo huru hali wewe umefungwa jera.
maana yake unaweza kusema kwamba;
"wao wasiofungwa ndio waniombee mimi mfungwa"

lakini hali haikuwa hivyo kwa Paulo.Yeye hakujiombea kwa nafsi yake pekee.

Nalikuambia kuwa;
Walaka huu ulikuwa ni walaka wa kumuambia Filemoni ampokee Onesmo (Onesmo ambaye hapo awali alikuwa mtumwa wa Filemoni,lakini akatoloka)

Haleluya...

Sasa kitu kilichomsukuma Paulo kumuandika Filemoni walaka mzuri namna hii ni MAISHA YA FILEMONI YA UTII WA NENO LA MUNGU.

"Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndio maana nimekuandikia,nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemavyo." Filemoni 1:21

Oooh,kumbe!
Sababu kuu iliyopelekea kuandika kwa walaka huu ni UTII aliokuwa nao Filemoni.
Kwa lugha nyingine,ni kwamba kama Filemoni asingelikuwa na moyo wa utii,basi ni dhahili kabisa Paulo asingemuandikia walaka huu.
Siku ya leo tunafundishwa kuwapokea hata wale waliotukimbia kwa njia ya kutoloka kama vile Paulo alivyompokea Onesmo mtu ambaye alikuwa hafai kwa sababu alimtoloka Filemoni mtenda kazi pamoja na Paulo,Lakini sasa mtu yule Onesmo aliyekuwa hafai,sasa anafaa.

Haleluya....

Fundisho nyingine la msingi tunalolipata siku ya leo ni kwamba;
Filemoni alikuwa amejaa PENDO na IMANI kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote.(Filemoni 1:4)
tunafundishwa kwamba Mungu ni pendo,hivyo basi Filemoni alikuwa amemjaa Mungu,pia Filemoni alikuawa ni mtu wa imani.

Walaka kwa Filemoni unatugusa sisi sote,maana wengi wetu tumeshawahi kuwa na watumishi wa ndani ambao waliotutoloka.
Lakini kupitia walaka huu tunafundshwa,kuwapokea wale wakosaji wote kwa pendo lote kama vile Paulo anavyomsihi Filemoni ampokee Onesmo kwa pendo lote,mtu aliyekuwa mtumwa wake...

ITAENDELEA...

* Nakusihi usikose fundisho hili mahali hapa,umuambie na mwingine ajifunze fundisho hili.

*Kwa huduma ya maombi na maombezi,piga
0655-111149

UBARIKIWE.



 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments