WARAKA KWA FILEMONI.*sehemu ya kwanza*

Na Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
Nasema haleluya,haleluya...

Karibu sasa ujifunze maana Bwana yupo sasa kwa kukuhudumia,
Fungua tu moyo.
Siku ya leo nakuwekea msingi wa fundisho;

Walaka huu kwa Filemoni ni mojawapo ya nyaraka yenye nguvu iliyoandikwa na mtume Paulo kwenda kwa Filemoni. Lakini cha kushangaza ni kwamba;walaka huu hauzungumzwi sana na wakristo wa leo,kana kwamba hauna nguvu,au kana kwamba hauna mafunuo yoyote. Yaani ni vigumu hata humkute mkristo mmoja akiusoma walaka huu wa mtume Paulo kwa Filemoni, na hii ni kwa sababu ya kushindwa kuelewa ujumbe wa walaka huu,maana ni kweli kabisa,upo ugumu wa kuelewa walaka huu wa Paulo kwa Filemoni.
Hivyo mara nyingi walaka huu hausomwi kabisa.
Lakini kupitia mahali hapa,neema imefunguka,kwa maana siku ya leo naenda kukuwekea msingi wa fundisho hili kwa kujifunza yale mambo yaliyofichika ndani ya walaka huu.

Haleluya...

Walaka wa Paulo mtume kwa Filemoni ulikuwa ni walaka aliouandika Paulo alipokuwa kifungoni huko Rumi mnamo mwaka 61-63 B.K.Pia inasemekana kuwa nyalaka hii iliambatana na walaka kwa Wakolosai.

Paulo alikuwa kifungoni pamoja na Epafra,na Aristarko watenda kazi pamoja naye.
"Epafra,aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu,akusalimu"Felemoni 1:23

"Aristarko,aliyefungwa pamoja nami,awasalimu na Marko,mjomba wake Barnaba..."Wakolosai 4:10

Filemoni alikuwa mtendakazi pamoja na Paulo. Huko Kolosai ndipo Paulo alikuwa akihudumu na Filemoni.
Kutokana na wachambuzi wa biblia wanasema kwamba;
Paulo alikuwa akihudumu sehemu tofauti tofauti kulingana na maongozi ya Roho mtakatifu,pia akaja kuhudumu nyumbani kwa Filemoni ambapo ikatengenezeka fellowship ndogo nyumbani kwa Filemoni. Kupitia fellowship hiyo,hatimaye baadaye ikiwa kanisa.

Haleluya...

Filemoni mtenda kazi wa Paulo,alikuwa na mtumwa aitwae Onesmo. Onesmo alikuwa ni mtumwa wa kawaida tu. Onesmo alikuwa pia ni mtu wa mataifa.

Ilifika wakati ambapo Onesmo akamtoloka bwana wake Filemoni. Alipotoloka kwa Filemoni,Onesmo akajikuta anadondokea mikononi mwa Paulo aliyekuwa amefungwa huko Rumi.

Ndipo hapo sasa Paulo mtume,anamwandikia walaka Filemoni,akimsihi ampokee Onesmo ambaye hapo mwanzo alikuwa hamfai sababu Onesmo alitoloka (Filemoni 1:11)

Haleluya...
Jina la Bwana Yesu lisifiwe sana...

Mara tu baada ya Onesmo kufika kwa Paulo ilimbidi Paulo amuongoze Onesmo sala ya toba,sababu alikuwa ni mtu wa mataifa,lakini Bwana alikuwa ana haja naye.

Paulo mtume anaanza kumuandikia Filemoni akimwombea kwanza NEEMA na AMANI zitokazo kwa Mungu. (Filemoni 1:3)
Paulo mtume anaanza kutufundisha siku ya leo,namna itupasavyo kuwatakia NEEMA na AMANI hata kwa watu wale wakosaji mbele zetu na mbele za Mungu,maana Filemoni pia naye alikuwa mkosaji.

Kwa taratibu za kipindi kile,mtumwa yeyote yule akimtoroka bwana wake,basi bwana wake aweza hata kumuua pindi akimkamata. Filemoni naye hakuwa tayari kumpokea Onesmo kwa sababu ya sheria ya kipindi kile,hivyo pia Filemoni alikuwa ni mdhambi wa kawaida tu.
Lakini tazama sasa Paulo akianza kumtakia NEEMA na AMANI zitokazo kwa Mungu....

ITAENDELEA...

*Kwa huduma ya Maombi na maombezi piga;
0655-111149

Usikose neema hii ya mafunuo katika fundisho lijalo mahali hapa.

UBARIKIWE.


 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments