WATALII WA KIKRISTO WAUWAWA KWENYE MLIPUKO WA BASI MISRI

Katika hali ambayo haikutarajiwa nchini misri, watalii 3 wa Kikristo kutoka nchini Korea ya Kusini wamefariki sanjari wa dereva wao wa nchini humo, na wengine wengi kujeruhiwa, wakati wakiwa katika mizunguko yao ya kutalii kutokea kanisa la Mtakatifu Catherine, ambalo ni eneo la kihistoria kwa mujibu wa UNESCO wakielekea Israel.

Kwa mujibu wa mashuhuda, basi ambalo watalii hao walikuwa wakisafiria, lilikuwa na jumla ya watalii 32, ambapo baada ya mlipuko huo kutokea maeneo ya Sinai, takriban kilomita yadi 250 kutoka mpakani mwa Israel.

Eneo ambalo mlipuko umetokea, ni eneo ambalo inaaminika Musa alipata amri kumi za Mungu kutoka hapo, 
Jincheon ni mji ambao wakorea hao wanatokea, ambako ndiko kanisa lao lilipo, na hata kufuatia tukio hilo,  shuhuda mmojawapo ambaye anasema ni mwanajeshi, anaeleza kuwa mlipuko huo utakuwa umesukwa na vikundi vya kigaidi, kwani ni wao pekee wana uwezo kufanya shambulizi la aina hiyo, ambapo bomu.

Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji wa kundi la waasi wa Muslim Brotherhood, ambacho kinafanya kazi zinachofanana na hii kimekataa kuhusika na shambulio hili moja kwa moja.
Tokea kuenguliwa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo, Mohamed Morsi, ambaye kwa sasa yuko mahakamani, kundi la Muslim Brotherhood, ambalo ndilo lilipelekea kuchaguliwa kwa kiongozi huyo, limekuwa likilipiza kisasi kwa wakristo nchini Misri kwa madai kuwa ni wao ndio waliopelekea kiongozi wao kuondoloewa madarakani.

Christian Post imeandika
 
 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments