BWANA YESU
asifiwe.
Ni neema ya
MUNGU kwamba tuko salama, ni makusudi ya MUNGU tuendelee kuishi katika Mwana wa
pendo lake, BWANA wetu YESU KRISTO.
Lengo kuu la
somo hili ninalokuletea mwana maisha ya ushindi mwenzangu ni kuwa tayari kwa
ujio wa BWANA YESU , ambapo wanadamu wote wanautarajia ujio huo.
Hakuna
ajuaye siku wala saa ila BWANA MUNGU mwenyewe, lakini kuwa tayari ni jukumu la
kila mwanadamu.
1
Thesalonike 4:16-17.( Kwa sababu BWANA mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja
na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya MUNGU; nao waliokufa
katika KRISTO watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia,
tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki BWANA hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na BWANA
milele. )
BWANA YESU
aliianzisha kazi hii muhimu ya kutufanya tuurithi uzima wa milele, na siku moja
atakuja kuimaliza ili waliotii wapate nafasi ya kufurahi na BWANA milele.
Yakobo
5:8-9(Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake BWANA
kunakaribia. Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi
amesimama mbele ya milango. ).
KWANINI TUWE TAYARI
KILA SAA?
Biblia
haijachagua kwamba tujitahidi kuwa tayari, kila mwaka, au kila mwezi au kila wiki, wala Biblia haisemi kwamba tuwe
tayari siku furahi tu bali kila saa inayotokea maishani mwetu.
Tuwe tayari
mpendwa, tuwe tayari maana tunaishi katika nyakati mbaya sana.
SABABU 7 ZA KWANINI TUWE TAYARI KILA SAA
KWA UJIO WA BWANA YESU.
1.
Kwa
sababu hatujui siku wala saa ya kuja BWANA.(Luka 12:40-Nanyi jiwekeni tayari,
kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.)
2.
Kwa
sababu dalili zote za siku za mwisho zimekwishatokea.(2 Timotheo 3:1-7-Lakini
ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu
watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye
kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda
wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali,
wasiopenda mema, wasaliti,
wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda MUNGU; wenye mfano wa
utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. Kwa maana katika hao wamo wale
wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye
mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; wakijifunza siku
zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.)
3.
Kwa
sababu BWANA YESU anatuandalia makao mbinguni na sisi hatutakiwi kukosa furaha
hiyo ya milele (Yohana 14:1-3-Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU,
niaminini na mimi. Nyumbani
mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda
kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena
niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.)
4.
Kuna
jehanamu ya moto kwa ambao hawakumpokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wao
kipindi wakiwa hai. 1 korintho 6:9-11-Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi
ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala
waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala
walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa
namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika
jina la BWANA YESU KRISTO, na katika Roho wa MUNGU wetu. ,
5.
Kwa
sababu tukishinda ya dunia kuna furaha
ya milele, Yohana 5:24-Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na
kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali
amepita kutoka mautini kuingia uzimani., Wagalatia 6:8-Maana yeye apandaye kwa
mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho,
katika Roho atavuna uzima wa milele. Hivyo tuutafute kwanza ufalme wa MUNGU
Mathayo 6:33-Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote
mtazidishiwa..
6.
Maisha
yajayo ya uzima wa milele, hakutakuwa na dhiki za dunia tena kama kifo, njaa,
mateso, magonjwa au uonevu wowote. Ufunuo 22:3-5-Wala hapatakuwa na laana yo
yote tena. Na kiti cha enzi cha MUNGU na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani
yake. Na watumwa wake watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina
lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. Wala hapatakuwa na usiku tena;
wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa BWANA MUNGU huwatia nuru,
nao watatawala hata milele na milele.
7.
Kwa
sababu kila mtu atavuna alichopanda maishani mwake akiwa duniani/ kwa sababu
kuna hukumu. Mathayo 13:49-50-Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia;
malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya
moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Tumejifunza
juu ya sababu za kuwa tayari kwa siku ya
BWANA,
Jambo
jingine muhimu linatokea hapa. Yaani nini cha kufanya cha kufanya wakati wa
kumngonjea BWANA YESU..
TUFANYENINI
WAKATI WA UTAYARI WETU WA KUMNGOJEA BWANA YESU?
2 Korintho
7:1- Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na
uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha MUNGU.
1.Tukae
ndani ya YESU KRISTO 1 Yohana 2:28 -Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi,
atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake..
2.Tujitakase
na kuishi maisha matakatifu.
3. Tufanye
kazi ya MUNGU.Wafilipi 2:13- Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda
kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema..
4.Tuzae
matunda mema kwa kuwaleta watu kwa
YESU.Yohana 15:16- Si
ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka
mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote
mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni.
5.Tumwabudu
MUNGU katika Roho na kweli.Yohana 4:24- MUNGU ni Roho, nao wamwabuduo yeye
imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
6. Tuharibu ufalme
wa shetani na tuujenge ufalme wa MUNGU. Yeremia 1:10- angalia, nimekuweka leo juu ya
mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza;
ili kujenga na kupanda.
7.Tuitumie
mamlaka ya KRISTO iliyoko ndani mwetu kuwaombea watu ili MUNGU awaponye na
awatenge na kamba zote za shetani ziliwafunga. Yakobo 5:15-16- Na kule kuomba
kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na BWANA atamwinua; hata ikiwa amefanya
dhambi, atasamehewa. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate
kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii..
BWANA YESU
asifiwe.
Tunapomngoja
BWANA si kwamba tutatakiwa kwenda sehemu
fulani kusubiri, bali tunamsubiri BWANA huku tukiishi duniani na tunakuwa
tunaendelea na Maisha kama kawaida, huku tukizingatia mambo hayo 7 hapo juu na
kuyatenda tungali hai..
Wokovu ni
sana ndugu, Wokovu si wa kukosa, BWANA YESU atarudi siku moja kuona umefanya
nini katika maisha haya.
Kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa
mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na
wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU
akubariki sana
Ni mimi
ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M
Mabula
Maisha ya
ushindi Ministry.
0714252292
Comments