Baada ya agizo la kuwaua wakristo 33, Rais wa Korea kaskazini atoa kali tena kwa kuwaagiza wananchi wake kunyoa kiduku kama yeye.

Rais Kim Jong- un wa Korea Kaskazini
Rais Kim Jong- un wa Korea Kaskazini Baada ya Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kuagiza kunyongwa kwa wakristo wapatao 33 wa nchini humo ambao walidaiwa kupokea msaada wa kuendesha makanisa ya siri kutoka kwa mmisionary wa Korea ya Kusini Kim Jong Wook. kipindi hiki ameibuka na jambo jipya ambapo Wanaume Korea Kaskazini wanakabiliwa na mtihani mpya katika taifa lao; wa kunyoa nywele kwa mtindo ulioamuliwa na rais wao. 

Watake, wasitake kuanzia sasa kila mwanamume atalazimika kunyoa nywele zake kwa mtindo anaoupenda Rais Kim Jong- un. 

Kiongozi huyo kijana, aliyerithi wadhifa huo baada ya kifo cha baba yake, hana mzaha hasa kutokana na nia yake ya kujenga mfumo mpya wa utawala ambao matakwa yake tu ndiyo ya kufuatwa. Ni wiki mbili sasa tangu serikali ya nchi hiyo kutoa agizo linalowataka wanaume kunyoa kama rais wao, huku wanawake nao wakielekezwa kutengeneza nywele zao kwa aina 18 tofauti na si zaidi ya hapo. Hilo ni moja ya maagizo yenye utata kuwahi kutolewa chini ya utawala wake, ambapo amekuwa akifanya jitihada za kujijengea mizizi, ikiwamo kuwaondoa na kuwaadhibu wale waliokuwa katika utawala wa baba yake wanaoonekana kutokubaliana na aina yake ya uongozi.


                             Mapokezi tofauti 


Hata hivyo, japokuwa staili yake ya unyoaji wa nywele imekuwa sehemu ya utambulisho wake na inafahamika na kila mmoja, agizo hilo limekuwa na mapokeo tofauti.

 “Namna ya unyoaji wake wa nywele inavutia, kwa wanaoipenda. Lakini haiwezi kumpendeza kila mmoja atakayeiiga kwa kuwa maumbo ya vichwa yako tofauti kutokana na maumbile,” alieleza raia mmoja akinukuliwa na Radio Free Asia ya Korea Kusini.


 Raia mwingine wa Korea Kaskazini ambaye anaishi nchini China, alieleza kwamba aina hiyo ya unyoaji nywele kwa raia waliopo China inaweza kuonekana kama uhuni.

 “Hadi katikati ya miaka ya 2000 tulikuwa tukiitaja aina hiyo ya unyoaji wa nywele kama ‘mtindo wa wahuni wa China,” alisema raia huyu alipohojiwa na gazeti la Korea Times. 

Hadi sasa, wanaume wa Korea Kaskazini wana aina 10 za unyoaji zilizowahi kuamriwa na Serikali yao. 

 Wanaume wamekuwa wakitakiwa kuwa na nywele fupi za wastani zenye urefu wa inchi mbili na wametakiwa pia kuzipunguza kila baada ya siku 15. 

Kama hujaisoma habari ya rais huyo kuagiza kuuawa kwa Wakristo 33 FUNGUA HAPA

 OMBA KWA AJILI YA WAKRISTO KATIKA NCHI HII.

Comments