 |
Mchungaji Peter Mitimingi akinyanyua juu mkoba wa uchawi wa babu kwa makutano. |
Huduma ya sauti ya matumaini ama The Voice of Hope Ministries (VHM)
chini ya mkurugenzi wake mchungaji Peter Mitimingi imeendelea kumshinda
shetani na kurudisha mateka kwa Yesu safari hii ikiwa katika moja ya
vijiji wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Ambapo katika mkutano huo mmoja kati ya magwiji wa uchawi wilayani humo
mwenye umri wa miaka 80 amekabidhi mfuko wake wa uchawi na kumpa Kristo
maisha yake. Mzee huyo amesema amefanya shughuli za kichawi toka akiwa
mtoto mdogo ambapo ameshindwa kukabidhi mtu wa kurithi mikoba hiyo
kutokana nayeye kuwa mzee nguvu za mwili zinamuishia hali inayomfanya
ashindwe kutimiza majukumu yake inavyotakiwa na kuwakasirisha majini
yake ambayo humuangushia kipigo kutokana na ugoigoi wake.
Baada ya kusikia makomandoo wa Yesu VHM wapo kijijini kwake aliamua
kwenda kuroga na kukutana na mzinga wa nguvu za Mungu na kujikuta
akisalimisha mizigo yake yote ya uchawi kwa watumishi wa VHM ambao bado
wanapiga injili kijijini hapo.
Huduma ya VHM imekuwa ikijishughulisha na injili sehemu za vijijini na
mijini ambako kuna ugumu wa injili kufikika kwa urahisi hasa kutokana na
sifa za kuwepo nguvu za kishirikina ama kutowahi kusikika injili kabisa
na watu wamekuwa wakionewa na nguvu za giza. Ili kujua mengi kuhusu
huduma hii ama kutaka kuchangia huduma hii ofisi zao zipo Mwenge jijini
Dar es salaam karibu na hospitali ya mama Ngoma au wapigie simu ifuatayo
0713 183 939
 |
Muhubiri wa mkutano huo mwinjilisti Lonas Khiwele akiunyanyua juu mkoba wa uchawi wa babu mbele za watu. |
 |
Mkoba ukiwekwa sawa kuchomwa moto. |
 |
Umati wa watu mkutanoni hapo. |
 |
Wakati wa kumshambulia shetani. |
 |
Mfuko wa babu ukichomwa mbele ya umati wa watu. |
 |
Kwa Yesu ndiko kwenye usalama wa uhakika, umati ukikubali kumfuata Kristo.>>>> CHANZO CHA HABARI GOSPEL KITAA ( GK |
Comments